Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Daah sema na City nao kuchukua PL mara mbili mfululizo hyo nayo dharau ujue,mi wote siwapendi,Gary Neville kama sikosei alivyoulizwa kuchagua kati ya Liverpool au City akasema kujibu hilo swali ni sawa na kuchagua nani alale na Mke wako kati ya adui zako wawili...
Hahahaha Neville kama kazaliwa mbagala vile...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lukaku toka mech ya liverpool kawa vizur sana
Falsafa ya Morinho iliharibu wachezaji wengi sana Lukaku akiwa mmoja wapo.

Morinho alipoondoka, michango ya wachezaji binafsi kama kina Herrera, Pogba, Rashford n.k imeonekana.

Si ajabu hata kiwango kibovu kinachooneshwa na Fred kimetoka enzi za Mou.

Naamini Lukaku ni striker hatari sana pale EPL.

Tumuamini, msimu ujao atatushangaza wengi sana na lazima awe mfungaji bora.

Lukaku is deadly and lethal. I believe in him.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatuwezi toboa mkuu wao wakipata goli moja tu ss tunatakiwa kushinda kwa goli nne na kwa majeruhi tulionao ntashangaa tukipata hata hilo goli moja.

Tunapata tena vizur tu kuwa na imani mpira ni mchezo wa makosa juve tumepiga akiwa na rekod nzur ya kutofungwa kwake mechi za makundi toka 2009 pale kwake
 
Kiukweli hata yeye akijitathmini nahisi anapata msongo wa mawazo...ndo wachezaji wa Mou hao,akiona timu zingine zinamuulizia anakimbilia kununua...kuna wakati namuangalia anavyocheza naamini kuna wachezaji zaidi ya mia kwenye ndondo cup wanaocheza vizuri zaidi yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
hahahahahaaaaaaaa comment yako imenichekesha sana kuliko tukio la edo kurudi nyumbani bila ya mkia.

siamini ya kwamba klabu ilimnunua fred kwa ajili ya kuwabania manchester city wasimsajili bali klabu ilishamuona fred kama ni potential midfield ambaye atatusaidia kwenye harakati za kurudisha heshima iliopotea kwa takribani miaka 6 ila kwenye ishu ya dau ni kweli shakhtar wametufanyia uhuni kiupande fulani.

wapo wachezaji wanaposajiliwa kwenye klabu mpya msimu wao wa kwanza wanarudisha fadhila za kusajiliwa kwao lakini wapo wengine wanastruggle sana na hii inatokana na changamoto za kimazingira na kimfumo, cha msingi ni kuendelea kuomba fred awepo kwenye hili kundi la pili kama ilivyokuwa kwa victor lindeloff na si lile la tatu (flop player kama bebe).

nyakati fulani jose mourinho aliwahi kuulizwa na waandishi wa habari kwa sababu gani hampi nafasi fred?
jose akajibu ni sababu za kimfumo na alilezea ya kwamba klabu ina tatizo la kiulinzi ndio maana tunaruhusu kufungwa hivyo basi kwa style ya fred uchezaji wake hauleti balance kwenye eneo la ulinzi, jose alikuwa anatuaminisha ya kwamba ili fred apate nafasi ya kucheza ni lazima defence ionyeshe mabadiliko.

Na hapo ndipo tatizo kuu la performance isioridhisha kwa fred ndipo lilipoanzia kwa sababu jose hakutaka kumpa game mara kwa mara ili kuonyesha improvement ya kiuchezaji (match fitness).
Hata nyakati zile tulizoshuhudia vita ya maneno kati ya jose mourinho dhidi ya paul pogba tulishuhudia jose mourinho akiendeleza tabia ya kumweka nje fred haliyakuwa kiucheza ndiye mchezaji pekee ndani ya timu yetu mwenye uwezo wa kuziba nafasi ya paul pogba kwa ufasaha zaidi, hatimaye jose mourinho alimuona marouanne fellaini kama ni mtu sahihi kuziba nafasi ya pogba pamoja na mctominay.

ujio wa solskjaer ametuletea falsafa ya 4-3-3 kwenye mechi zake takribani zote alizocheza, kwa hali ya timu yetu ilivyo hata kama mimi ndiye solskjaer basi ningeendelea kumbatiza kwa moto wa gesi fred the red.

hivi ni kweli perreira na mc tominay ni wachezaji mahodari kuliko fred?
kwa mtazamo wangu si kweli, sababu kubwa inayopelekea wawili hao wapewe nafasi mbele ya fred ni kwa sababu mpira baadhi ya nyakati hatuangalii chenga na rangi bali balance na impact inayoletwa na mchezaji akiwa uwanjani pindi unapokutana adui mwenye sifa kama za kwako.
ina maana sababu ile ile iliopelekea mourinho amweke nje fred ndiyo anayoendelea kuitumia ole gunnar solskjaer nyakati hizi nayo ni sababu ya balance kwa sababu bado defence yetu haijawa katika kiwango cha juu ukilinganisha na kuta za timu nyengine kama atletico madrid, liverpool. timu zote tunazozifahamu basi hazikosi wachezaji wenye mindset, form, uzoefu na uwezo wa kucontrol game na hapa ndipo anapozidiwa fred na vingo tulionao ndani ya klabu.

  • kwa mujibu wa timu yetu anapoumia matic nafasi yake inapaswa izibwe na mctominay kwa sababu ni defensively solid player dhidi ya fred.
  • anapoumia herrera nafasi yake inapaswa izibwe na perreira kwa sababu ndiye mwenye uwezo wa kuleta balance halafu pia ni rahisi kufanya naye mawasiliano kwa sababu anaweza kuzungumza lugha ya kiingereza.
  • ina maana kwa mpira anaocheza fred eneo pekee ambalo ataufurahia mpira wake ni nafasi ya paul pogba, wakati huu tunaowania kuwepo top 4 je unaweza kumfanyia rotation pogba kwa ajili ya fred?
changamoto anazokutana nazo fred ni tofauti kabisa na changamoto alizokutana nazo victor lindeloff msimu uliopita na mwanzoni mwa msimu huu, wapinzani wa lindelof ambao ni smalling, bailly na jones wote kwa pamoja ni rahisi kupambana nao kwa sababu ya viwango vyao na hata takwimu zao za majeruhi.

lakini kwa fred hali ni tofauti kwa sababu matic, herrera na pogba tayari wameshajijenga kama ni nguzo muhimu ndani ya timu yetu hivyo basi fred anahitajika kuutumia msimu ujao kwa kufanya bidii kubwa sana ili amuondoe mmoja wapo huku akiombea klabu ifanye usajili wa kumleta mlinzi hodari atakayemuwezesha kumpunguzia majukumu ya kulinda.

tumpe muda na nafasi ya kudhihirisha thamani yake, nataka niendelee kuamini ya kwamba fred hakuja uingereza kujifunza lugha ya malikia iliomchukua miaka mingi carlos tevez kuifahamu bali amekwenda uingereza kufanya kazi.
 
Back
Top Bottom