Mbio za top 4 kwa United
Msimu uliopita Man Utd alikuwa nafasi ya 2 akiwa na points 81, Spurs nafasi ya 3 kwa points 77 na Liverpool nafasi ya 4 kwa points 75
Man Utd kwa sasa ana points 55, kama akishinda mechi zote anamaliza ligi akiwa na points 85. Ina maana akipoteza points 10 kati ya mechi 10 zilizobaki (jambo ambalo ni gumu kutokea) atakuwa na points 75, sawa na za aliyeshika nafasi ya 4 msimu uliopita.
United ana mechi ngumu na City. Mechi ya Chelsea na Arsenal ni ngumu lakini si sana (Na hizi mechi ni 6 pointer).
Endapo katika mechi zilizobaki akipoteza points 4, ataweza kumaliza ligi akiwa na points sawa na za msimu uliopita ambapo tulikuwa washindi wa pili. Swali je jumla ya points za mshindi wa pili wa msimu wa 2017/2018 hazitatosha kumfanya amalize top four? Vipi kuhusu points za mshindi wa tatu ambaye alipata 77? Kiufupi United anayo nafasi kubwa ya kumaliza ligi akiwa wa nne au hata wa tatu.
Katika mechi zilizobaki zipo ambazo tutakutana na wale wapinzani wetu kwenye top 4. Kuwafunga ni kama kupata points 6 dhidi yao, maana umeongeza points zako 3 na umempoka yeye points 3.
Hapo hatujaongelea fixtures zao wenzetu. Mfano Chelsea ana mechi na Liverpool na Man Utd ugenini, ana Wolves na Leicester timu sumbufu kwa vigogo. Sijamsahau Burnley.
Ukija kwa Arsenal ana United, ana Spurs, ana Wolves, Cristal Palace, ana Leicester. Pia yupo Burnley.
Kwanini kwa mazingira hayo United asimalize msimu akiwa top 4?
Sent using
Jamii Forums mobile app