Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ninataka kusema hawezi kuongeza chochote kwa kulinganisha na watu ambao tayari wapo OT

Sent using Jamii Forums mobile app

Mjomba hakuna Striker pale OT ambae anafika level za Icardi sema labda hujamjua jamaa vizuri..Icardi walikuwa wanafukuzana na Higuain kipindi alvyokuwa Napoli na Juve na Mara nyingi amekuwa akimzidi magoli japo inter hawakuwa vzr kihvyo!
 
Na huyo Martial aangalie mpira hapa, kila mchezaji anapambana kivyake, Lukaku anasumbuka kule Mata anazunguka kote Rashford yuko moto...Yeye alizoea kukaa pale mbele kushoto anasubiria mipira!!!! na asipone kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ha ha ha ha ha yaani nikishaonaga tu avatar yako najua Martial hayuko salama. Alifanyaje ndugu? Ha ha ha ha ha
 

Umepotea njia mkuu!
 
Ishu ya Icardi kutokuitwa National timu haihusiani kabisa na Technical ability ya jamaa hyo inahusiana na swala la nidhamu,Icardi shida yake ndo hyo ila kiuwezo yupo level za kina Aguero na anamzidi Higuain!

Alihusika kwenye kuharibu ndoa ya Rafiki/Team mate wake Maxi Lopez kwa kulala na mke wake na baadae kumuoa kabsa alivyo achana na Lopez..kitendo hicho kiliwakera sana wa Argentina wengi na ndo maana Messi akatoa mapendekezo kama Captain jamaa asiitwe ili kuwe na amani kwenye timu!
 

Mkuu kumbuka tunashinda ila hatuna ubavu wa kumiliki mpira yaani hatufichi kabisa mpira


Ila sina mashaka na kocha suala la kuifumua timu lipo palepale ashley young si namba 3 wa kutegemewa ujue tunaweza kulaumu wakina smalling na jones kuna watu magarasa lukaku hata mata na sanchez angalia hizo namba nilizotaja zipate watu sahihi kwa mwendo wa ole watu watakimbia humu
 
Mjomba hakuna Striker pale OT ambae anafika level za Icardi sema labda hujamjua jamaa vizuri..Icardi walikuwa wanafukuzana na Higuain kipindi alvyokuwa Napoli na Juve na Mara nyingi amekuwa akimzidi magoli japo inter hawakuwa vzr kihvyo!

Mkuu naheshimu sana mawazo yako kumchukua icard ni sawa na kuwa na lukaku tu
 


Hyu dogo "Joao Felix" nilianza kusikia habari zake na kumfatilia akiwa bado kwenye Academy ya Benfica, trust me huyu dogo atakuja kuwa mchezaji mzuri sana (worldclass level) akiendelea hvyo hvyo, toka alivyoingizwa kwenye first timu amekuwa na mchango mkubwa sana ni either atoe assist au afunge bao ningependa sana kama United watafanya michakato dogo aje maana wakina Mata umri nao unasogea sahv na hao madogo ndo future!

Pia nimekuwa impressed sana na kinda Wetu "Mason Greenwood" hyu dogo ni hatari SANA aisee.. amekuwa akifanya vizuri kuliko hata wakina Rashford walivyokuwa Academy na Technically nadhani atakuwa bora zaidi ya Rashford, hebu ngoja tusubiri tuone atafikia wapi...
 
Mkuu naheshimu sana mawazo yako kumchukua icard ni sawa na kuwa na lukaku tu

Yaani unamfananisha Icardi na Lukaku duuh...nway Kila mtu na mtizamo wake aisee!

Eleza kidogo,

Binafsi naeleza ninachokiona mimi sio wanachozungumza watu!
Martial bado mtoto sana kulinganisha na Lukaku ktk hii field!
Ndo kwanza Martial anajitafuta bado hata hajui anataka nini hasa kwa Career yake!!

Kujibu hili swali ni ngumu sababu mambo yako mengi sema ntafupisha..

Kwanza ngoja niseme ni kweli Lukaku sio mchezaji mbaya sema sahv hayupo kwenye form, ila pamoja na hayo ana weakness nyingi sana kwenye game yake kuliko Martial na kumbuka Martial ni mdgo kwake hvyo anaweza improve zaidi,Lukaku ni Pure n.o 9 wakati Martial ni Complete Forward (anaweza cheza kokote mbele) sababu; ( technically Martial ni bora zaidi).

1.Martial anaweza kudribble (kukimbia na mpira kwa kasi na kufanya skills) vizuri zaidi ya Lukaku

2.First touch ya Martial ni bora kuliko Lukaku (kitu muhimu sana kwa striker anavyopokea pasi; fundi wa hii alikuwa Berbatov)

3.Martial ni Mtulivu zaidi akipata chance ya kufunga kuliko Lukaku

4.Martial anaweza kutengeneza Chances/Assist nyingi kuliko Lukaku

5.Martial anaweza kuhold mpira na kucheza pass/one twos) na wenzake vizuri zaidi ya Lukaku.

Kiufupia Lukaku ameshafikia prime age ya kushine lakin tunaona anazingua wakati Martial bdo mdogo lakin anafanya makubwa na hapo anafanya kwa kurelax je akianza kukaza itakuwaje?
 
Pamoja ndugu
 
Ahsante kwa maelezo, nimekuelewa Bro.

Umeeleza vizuri sana.
 
Kwa kutumia historia Lukaku bora zaidi ya Martial ila kwa hivi karibuni na sasa kwa ujumla Martial ni zaidi ya Lukaku kabisa bila ubishi
 
Kwa kutumia historia Lukaku bora zaidi ya Martial ila kwa hivi karibuni na sasa kwa ujumla Martial ni zaidi ya Lukaku kabisa bila ubishi

Alikuwa bora kwa kipimo kipi magoli au? kama ni swala la magoli hapo tutakuwa tunamuonea Martial sababu alivyokuwa Monaco
kulikuwa na wachezaji wakubwa waliokuwa wanafanya asipate n.o (kama striker) mfululizo mfano Falcao na Berbatov hvyo mara nyingi alikuwa anakaa benchi au anachezeshwa kama winger.

Wakati Lukaku yeye alipelekwa mkopo na chelsea na alipewa nafasi ya kucheza Westbrom na Everton sababu walikuwa hawana striker mzuri, hvyo kila siku alikuwa anacheza na alikuwa anacheza kama striker! so sidhani kama magoli ni kipimo kizuri sababu inategemea na muda uliopewa kucheza na unachezea eneo gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…