Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

RB yupo Dalot, ni kweli verrati ni ngumu kumchomoa PSG ila inawezekana kama mchezaji mwenyewe atakuwa tayari.
Kumtegemea Rashford na Greenwood kwenye CF kwa team kama Man u ni kuwaonea bado hawajakomaa
Mkuu sorry, umeongea kama hao wachezaji wako academy ya man u.

Marco verrati si rahisi PSG kumuachia, muda huu ambao wanamuhitaji sana.na hata wakimuachia itakuwa ni kwa pesa ndefu sana, so sizani kitu kaa hicho kinaweza tokea. Lakini ni kweli angetufaa sana nazani kucheza eneo la matic pia.

Christian Eriksen, sawa tatizo levy, jamaa yule ni mgumu sana kudeal nae,

Harry Maguire sina neno,

Harry Kane, hii kitu ni ngumu sana, nazani ni 150+£, club yetu haiwez kuspend hivyo , wakati kuna maeneo mengine yanaitaji additions, pia kwanni tulete CF wakti kuna Rashford na Greenwood wanakuja.

Rabiot, huyu atapatikana free, lakini huyu ni more attacking, means ukimueka pamoja na pogba unahitaji DM mzuri sana(sio huyu matic aliyeanza kuchoka)
Ila naamin kocha mzuri anaweza kuwatumia vzr tuu.
Rabiot, mama yake ndiye agent wake, ni wasumbufu kiana.

Anyway cha mhimu tupate RW, Deep playmaker, CB, Na RB.

Sent using simu mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Damn..hao wachezaji utaenda kuwachukua tu kama unachota maji baharini??
Kwanini Man Utd tushindwe kuwanunua hawa?

Kama Juventus wameweka mpunga kumtaka Mohamed Sallah. Sisi tunashindwa vipi kuwachukua kina Mbappe nk?

Man City ataingia sokoni atawanunua na kuwatumia. Tutabaki kupiga story zilezile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini Man Utd tushindwe kuwanunua hawa?

Kama Juventus wameweka mpunga kumtaka Mohamed Sallah. Sisi tunashindwa vipi kuwachukua kina Mbappe nk?

Man City ataingia sokoni atawanunua na kuwatumia. Tutabaki kupiga story zilezile.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijasema tunashindwa..lakini sio rahisi kama tunavyodhani..spurs wamuachie erisken,psg watupe verrati,,mara reus..sio rahisi kihivyo
 
RB yupo Dalot, ni kweli verrati ni ngumu kumchomoa PSG ila inawezekana kama mchezaji mwenyewe atakuwa tayari.
Kumtegemea Rashford na Greenwood kwenye CF kwa team kama Man u ni kuwaonea bado hawajakomaa

Sent using Jamii Forums mobile app
huyo diogo dalot itamchukua tena miaka miwili ndio afikie uwezo wa ashley young huyu tunayemshuhudia kila wiki, timu yetu bado haina mlinzi wa kulia anayekwenda na mdundo wa kisasa na kitendo cha ashley young kupewa mkataba mpya ni dalili iliowazi ya kwamba klabu haina mpango wa kutafuta mlinzi mwengine wa kulia ambaye uwezo wake unalingana na wachezaji kama kyle walker, thomas meunir, benjamin parvard, dani carvajal n.k

kwenye ishu ya kuzungumza ukweli ndipo nilipokuwa nikimpendea jose mourinho, sijui kama kocha ajaye atakuwa mkweli au ahsante bwana.
ngoja tuone kwa atakayekuwa hai​
 
hebu ongeza nondo mkuu... It's a joy kusoma article zako kuhusu mwenendo wa timu hasa sporting director, usajili na kocha mpya... Unaelezea vitu vingi muhimu

Kama ingekuwa ivyo basi mungezaja wakina mess apo OT. Cr7 alikacha kwa sababu aliona miyeyusho tu apo..

Sent using Jamii Forums mobile app
Unauhakika Ronny alikacha kurudi Man u akitokea Madrid? Mkuu unaongea kwa mihemko na inawezekana hata Man United hatukumlist kwenye target zetu kabla hajaenda juventus....

Wenzetu mnauwezo wa kumsajili nani kwa hali hiI ya Sorry ball? unaangalia.mechi za Dortmund lakini? kuona jinsi Pulisic anavyoleta wasiwasi hahahahaha inawezekana asifanikiwe akawa flop, time will tell...

Alafu Man United ukiachana na financial power, timu ina mashabiki wengi kukukomoa unavyodhanu, tukichanga dollar 1 tunaweza kununua first eleven ya Chelsea yote...this is Manchester

Sent using Jamii Forums mobile app
 
baada ya kuiangalia hii video kwa umakini nimefanikiwa kujifunza mambo yafuatayo:
  1. thomas tuchel anaonekana kama ni mwandamu mwenye sura ya kitoto lakini ni muuaji wa mechi kuliko mungu wetu mwenye sura ya kitoto, ndani ya dakika 90 amebadilisha mifumo takribani mara tatu lakini kwetu ilikuwa ni tofauti, tulivyoanzia na 4-1-4-1 ndivyo tulivyoamua kumalizia bila ya kuangalia athari zinazotukumba, hapo ndipo unapomkumbuka yule mwanadamu asiyeamini demokrasia kwenye kuongoza (jose mourinho).
  2. wapinzani wetu wanatulazimisha tuamini ya kwamba PSG walikuwa pungufu kwa sababu ya kutokuwepo kwa wachezaji wao watatu muhimu, baada ya kuiangalia hii video nimegundua madai yao ni batili na yanahatarisha usalama wa klabu yetu pendwa ya manchester united, wavumishaji wote wa taarifa hizi wanapaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ili iwe ni fundisho kwa wabwatukaji wengineo.
  3. ukweli ni kwamba sisi manchester united ndio tulikuwa pungufu ukilinganisha na PSG, kuna gape kubwa sana la wachezaji na kiuchezaji kati yetu na watakatifu wa paris na cha ajabu zaidi gape hili limetanuka zaidi ndani ya miaka mitatu, sijui imewezekana vipi ndani ya miaka mitatu PSG wawe na timu kubwa kuliko sisi tunaojisifu tuna uwezo wa kumng'oa mchezaji yoyote duniani, ndani ya dakika 90 za mchezo wachezaji wa PSG wakiongozwa na kimpembe, silva, maquinhos, veratti wametufanya tumjaribu gianluigi buffon mara moja tu tena baada ya kujisahu kumdhibiti rashford.
  4. jambo moja linalonipa matumaini mpaka sasa ni kwamba ni rahisi kwa mwalimu na benchi lake la ufundi kuja na mkakati mwengine ulio bora wa kuwakabili PSG mechi inayofuata, lakini mikakati bora bila ya kuwa na dhana bora zitakazokuwezesha kutekeleza mpango wako uliokusudia ni kazi bure na hili ndio tatizo letu.
  5. ukweli ni kwamba man utd hatujajiandaa kuishi bila ya paul pogba ambaye juzi alifichwa na marquinhos kwa dakika 90, huu ni msimu wa tatu mfululizo klabu yetu imeelekeza nguvu zake zaidi upande wa kushoto kimashambulizi dhidi ya wapinzani na hapo ndipo psg walipofanyia kazi udhaifu wetu huku wakitudanganya na stori za neymar na cavani kumbe wanafukuza mwizi kimya kimya.
  6. Tunakwenda kupambana na hawa jamaa bila ya paul pogba ambaye ndiye engine yetu upande wa kushoto, tunakwenda kupambana na hawa jamaa huku mbappe akitegemewa kurudi upande wa kushoto ambao mechi ya juzi tukiwa nyumbani hatukuwatishia psg kwa lolote, tunakwenda kupambana na hawa jamaa sisi tukihitaji magoli matatu, na kwa mujibu wa hii video kwa dakika zote 90 ole gunnar solskjaer aliwaruhusu herrera na pogba wasogee mbele zaidi kwa lengo la kutengeneza nafasi huku wakimuacha nemanja matic akiwa peke yake nyuma akiwalinda walinzi wanne jambo ambalo liliwapa mwanya psg watushambulie kwa counter attacks kila upande kwa sababu nafasi tuliokuwa tukiiwacha ilikuwa ni kubwa sana jambo lililopelekea kutoa uhuru mkubwa sana wa kufanya maamuzi wachezaji wa psg wasiokuwa kwenye kiwango wakiongozwa na angel dimaria, draxler na dani alves, kama mkakati huu ulikuwa ni majanga kiupande wetu je ni mkakati gani utakaotupa faida mechi yetu ya pili bila ya pogba aliyedhibitiwa hapo juzi, au tusubirie set piece kama mwaka 1999 lakini mkubwa fellaini hayupo.
ahsante sana nouman huko uliko kwa uchambuzi, ahsante sana Belo kwa kushare nasi hii video nasubiri mchango wako utakapopata muda unitoe ujinga na wenzangu.
 
hebu ongeza nondo mkuu... It's a joy kusoma article zako kuhusu mwenendo wa timu hasa sporting director, usajili na kocha mpya... Unaelezea vitu vingi muhimu

Sent using Jamii Forums mobile app
hivi vyeo unavyonipa ni vikubwa kuliko cv ya vyeo aliokuwa nayo iddi amini dada, nahofia hivi vyeo vitanigeuza tabia zangu na kuwa shetani muandika upumbavu humu ndani.

kama tuna mpango wa kumpa ajira ya moja kwa moja OGS basi si vibaya kuchelewesha upatikanaji wa DOF kwa sababu OGS na benchi lake la ufundi wanaweza kuifanya kazi ipasavyo ya kufanya tathmini ya kikosi chetu huku wakimsubiri DOF achaguliwe mwanzoni mwa msimu, kama OGS ni kocha wa kupita halafu kocha ajaye ndiye mwenye mikakati yote ya usajili basi huu ni muda muafaka wa kumtangaza DOF ili apate kufanya kazi yake ya kufanya tathimini ya kina kwa timu na kuandaa mikakati ya usajili ili kocha ajaye ajuwe wapi pakuanzia.

kama tunamsubiri kocha mpya na DOF wafanye kazi kwa pamoja pindi watakapotangazwa ifikapo mwezi July basi tutakuwa tumepoteza muda wetu bure, ukiziangalia timu kama barcelona, juventus na bayern munich tayari wameshaanza kufanya maandalizi ya msimu ujao kwa kutafuta target zao muhimu wanazozihitaji kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao lakini kiupande wetu bado tunasukumuwa zaidi na ishu ya kocha, tetesi za DOF na tetesi nyingi za wachezaji.
ndivyo ninavyojiaminisha kiupande wangu sijui wewe una mtazamo upi.​

kuhusu tetesi za DOF kila siku wagombeaji nafasi wanazidi kumiminika kwa mujibu wa magazeti ya uingereza na hii ni kwa sababu magazeti wameshaona fursa ya kupiga hela ila mwenye maamuzi ya mwisho ni ed woodward na mabosi wake.
  1. Jordi Cruyff = ana ukaribu sana na OGS
  2. Tony Whelan, John Murtagh, Matt Judge : wote wamefanya kazi manchester united.
  3. eric cantona
  4. Sven Mislintat
  5. monchi
wapo wengi lakini nimempenda Sven Mislintat kwa jicho lake kali akifanya kazi kama recruitment pale dortmund akiwa pamoja na director michael zorc na hata arsenal pia alifanya kazi nzuri kabla ya kuondoka miezi michache iliopita.
mara nyingi nafuatilia thread hii kwa ajili ya kufuatilia hii ishu na kupata kusoma michango ya wadau mbali mbali.
Man Utd set to appoint Director of Football | Expected before next manager hired
Manchester United Forum
1550240725869.png
 
Lakini pia mapungufu ya Man u yako katika maeneo mengi sana.

Kwa upande wangu Mimi siyaoni mapungufu makubwa kwenye full backs japo tulionao huwezi kuwalinganisha na team zingine kama Man city, juventus, real Madrid na Bayern Munichen lakini mapungufu ya maeneo mengine ya team yatapunguza udhaifu wa full backs.

Attacking midfield ya man u siyo creative kiasi hicho ndiyo maana team inatengeneza chances chache sana za magoli.

Striking force ya man u haiko sawa sawa pia unaweza kuona kwa msimu huu kila striker yuko below ten goals na kwa mfumo tunaotumia unategemea striking force ifunge magoli zaidi siyo kama ya man city.

Central defence ya Man u iko na mapungufu makubwa sana pia inashindwa kusahihisha makosa ya defence midfield tunaadhibiwa kizembe ni kutokana na central defenders wengi tulionao kuwa bang average players.

Bado na defense midfield ya man u inaperform kwa vipindi haina consistent na haina uelewano mzuri kama team zingine kama man city PSG , Juventus na Bayern
huyo diogo dalot itamchukua tena miaka miwili ndio afikie uwezo wa ashley young huyu tunayemshuhudia kila wiki, timu yetu bado haina mlinzi wa kulia anayekwenda na mdundo wa kisasa na kitendo cha ashley young kupewa mkataba mpya ni dalili iliowazi ya kwamba klabu haina mpango wa kutafuta mlinzi mwengine wa kulia ambaye uwezo wake unalingana na wachezaji kama kyle walker, thomas meunir, benjamin parvard, dani carvajal n.k

kwenye ishu ya kuzungumza ukweli ndipo nilipokuwa nikimpendea jose mourinho, sijui kama kocha ajaye atakuwa mkweli au ahsante bwana.
ngoja tuone kwa atakayekuwa hai​

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Club yake toka ianzishwe hajatokea hata Balloon D or winner

Back
Top Bottom