ole ole ole ulikuwepo wapi nyakati zile tunateseka?
ni takribani wiki 9 tokea uanze kazi pale AON cha ajabu umetufanya tuonekane na wapinzani wetu tumefanya usajili wa timu nzima kumbe ndio wale wale wa kila siku.
tokea uanze kazi mimi lofa na wenzangu tunashangazwa kuona morali yetu na nidhamu ya kupambana imeongezeka sana ukilinganisha na makocha wote waliopita, nyakati zile arsenal wanasawazisha goli moja naamini kama tungelikuwa bado tupo kwenye utawala wa bwana yule tungelishuhudia khofu kubwa ikitawala kuanzia wachezaji hadi mashabiki lakini tulichokishuhudia jana ni tofauti kabisa na tulichozoweshwa kwa miaka 3.
ole umeturudisha nyakati zile nilizokuwa napendelea kuangalia mechi zetu kila wiki, nakumbuka nyakati zile ni wachezaji wachache walikuwa na uhakika wa kucheza kila wiki huku tukiwapa nafasi wachezaji wengineo (rotation) wakuze viwango vyao, tokea awasili ole gunnar kama nitakuwa sikosei ni
antonio valencia, smalling, na marcos rojo ndio wachezaji waliosafiri na kikosi mara chache, ni matumaini yangu wiki ijayo atampa tena nafasi
fred apate kujisahihisha.
umetufanya kwa muda mfupi tusahau anguko letu huku tukijawa na morali ya kurudi tena pale tulipofikia msimu uliopita, najua siku moja tutapoteza pambano japokuwa siombei tupoteze mechi yoyote chini yake, sina wasiwasi kwa jinsi unavyozungumza kupitia mahojiano yako ya kila wiki ni matumaini yangu utakuja na sababu za msingi za kufungwa kwetu tofauti na bwana yule anayesukumia mizigo wachezaji wake hata kama tatizo ni yeye.
ili defence yetu izidi kupata mapumziko ya mara kwa mara tunahitaji midfield yetu ifanye kazi zaidi ya sasa kwa kumiliki mpira zaidi (ball retention) huku tukishambulia kwa haraka zaidi kama alivyokuwa akifanya paul pogba dakika 30 za mwisho, ninapowaangalia liverpool na manchester city wakicheza hushuhudia utofauti mkubwa sana wa kiuchezaji dhidi yetu, nitafurahi sana endapo tutakapokutana tena na timu kubwa na nyenginezo sisi ndio tuwe bora zaidi eneo la midfield kuliko wapinzani wetu, naamini hii ndio solution nyengine itakayosaidia kupunguza kuonekanwa madhaifu ya defence yetu ukiondoa solution ya usajili ambayo kwa sasa kuna uwezekano mdogo wa kuingiza mlinzi mpya.
dirsha lijalo kama tutapata mwanadamu mwengine mgumu kama
herrera (tackle and break up) na wakati huo huo akawa na uwezo wa kucheza na mpira (ball playing midfield) ) kama herrera yule wa miaka ya mwanzoni basi tutakuwa tumeua ndege wawili kwa jiwe moja kuliko kusajili wachezaji wawili kwa eneo moja, nimeanza kuwachukia barcelona kwa tabia yao ya kukusanya midfield 11 kwa wakati mmoja huku wakituache wengine tukihangaika sokoni.
kumbe huyu romelu lukuku akitokea pembeni anakuwa hatari zaidi kuliko anaposimama kati kati, sijui kwa nini amenyimwa skills na speed.
kiupande wangu man of the match kwa siku ya jana alikuwa ni
ander herrera.
happy birthday jose mourinho