Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Man City hata wasiponunua tayari wana timu ya kugombania ubingwa hata miaka 4 ijayo Pep anahitaji backup/replacement ya Fernandinho tu
GT Belo,umerudi tena pale pale kwenye mtazamo wangu wa kwa nini sipendelei man city abebe tena ubingwa msimu huu kwa sababu tayari hawa majirani kwa kikosi walichonacho wana uwezo wa kubeba ubingwa mara tatu mfululizo jambo ambalo litapelekea majirani zetu kuzidi kutukalia juu wakati ambao tunataka kujikwamua, vile vile kubeba kwao ubingwa ndio kutazidi kumfanya guardiola aonekane ni untouchable na ligi yetu pia ionekane ni ya upande mmoja.

Unadhani Liverpool wakichukua ubingwa ndio timu yao itakuwa weak ?
Football ya sasa ni pesa Klopp aliponda usajili wa Pogba baada ya mwaka akanunua GK & CB kuvunja rekodi na umeona hao wachezaji 2 ndio wameifikisha Liverpool ilipo.
milner, henderson, matip, lovren, origi, lalllana, clyne, sturidge, moreno, ings, gomez n.k
Don Clericuzio na washabiki wenzako wa liverpool FC naomba muwe wa kweli; hivi munafurahia kuona timu yenu imekusanya wachezaji niliowataja hapo juu kama ndio backup yenu na wengineo ndio first eleven?
kama munafurahia basi nitakuwa sipo sahihi kwa kile ninachokiamini

hata muda huu ambao bado hawajabeba ubingwa nawaona liverpool wakiwa ni dhaifu ukiwalinganisha na manchester city, timu inayoundwa na wachezaji hao niliowataja hapo juu kama ndio backup yao pindi linapotokezea tatizo kwenye timu kwa nini nisiwaite dhaifu.
timu ambayo ikitokezea virgil amepumzishwa nafasi yake inachukuliwa na lovren kwa nini isiwe dhaifu?

hata kama liverpool wataingia tena sokoni chini ya matajiri wa kimarekani kwa sera zao za matumizi naamini itawachukua tena miaka miwili ili waweze kuwaondoa wachezaji hao niliowataja na kuwaleta wengine wenye uwezo zaidi ya hao, kimtazamo wangu nawaona liverpool wanasumbuliwa zaidi na tatizo la ukosefu wa wachezaji wengi wenye ubora ukilinganisha na manchester city hata kama itatokezea atabeba ubingwa, na huo ndio udhaifu ambao nauona mimi kama ni faida kwetu sisi msimu ujao endapo kama tutafanya biashara sahihi.

lakini ukija kwa upande wa majirani zetu kwa nguvu yao ya usajili wana uwezo wa kutafuta mrithi wa fernandinho, david silva, vicent kompany kwa msimu mmoja tu bila hata ya guardiola kutakiwa auze kwanza mchezaji ili aongezewe fungu la usajili.

vile vile kwenye ishu ya matumizi sidhani kama liverpool wana uwezo wa kusimama na manchester united kama ilivyo sisi tusivyoweza kusimama na manchester city kimatumizi na si kwa kulinganisha thamani za klabu, hivyo kiupande wetu naamini kama tutafanya biashara sahihi kwa kuangalia zaidi udhaifu uliopo kwenye kikosi chetu upo uwezekano mkubwa wa kufikia level walioionyesha liverpool msimu huu hata kama na wao wataingia sokoni.

mimi naona kuna tofauti ndogo sana kati yetu na liverpool FC lakini kuna utofauti mkubwa kati ya kikosi chetu na kikosi cha manchester city ndio maana sipendelei man city abebe tena ubingwa.
bado akili ya josep guardiola haijachoshwa na maisha ya etihad.

kama sipo sahihi naomba nikosolewe kistaarabu ili ujinga uliomo kwenye ubongo wangu upungue.​
 
Unayoyaongea ni kweli

Inabidi tuingie sokoni tutafute no 10 wa kueleweka na Erisken naona ni mtu sahihi

No 7..hivi costa wa juve hatuwezi kumsajili??

No 6(replacement ya matic)..

Then tuje kuboresha defence line yetu..

McTominay,Perreira,Fellaini..hawa bado sijaona nafasi yao pale united..personally naona hivo

Mkuu embu jaribu hata kumzungumzia Anthony Martial kidogo..tuendelee kumtegemea kwenye left flank??..unazungumziaje attitude zake,ari yake je??

kwa wale tunaoamini uwepo wa Mungu kama ndio muweza wa vyote acha tuendelee kumshukuru na kumshangaa kwa uwezo wake mkubwa alionao, jaribu kufikiria ni yeye peke yake ndio aliyetuumba halafu ametujaalia tuwe na uwezo tofauti wa kufikiri na ukienda mbali zaidi unaweza kusema huyu Mungu amejawa na ubaguzi kwenye maamuzi yake.
nimeanza kwa kujilinda ya kwamba binadamu tuna utofauti mkubwa sana wa kuelewa mambo hivyo basi ni matumaini yangu sitokutana na comment zenye kuudhi zaidi bali nitakutana na comment zitakazonifuta ujinga wangu uliojaa kwenye ubongo wangu.

nimekuwa nikifuatilia dirisha la usajili kuanzia mwezi Agosti na January kwa umakini kabisa nikiwa na mategemeo ya kuwashuhudia wachezaji bora wakisajiliwa na manchester united, si lengo langu kuwazungumzia wachezaji tuliowasajili bali dhumuni langu kuu ni kuangazia hii ishu ya usajili wa mlinzi wa kati ambayo ndio imekuwa iki trend zaidi kiupande wetu.

hivi ni kweli jose mourinho ameondoka manchester united au ameng'atuka tu kama marehemu bwana yule?
nikisema kilichoondoka ni kiwiliwili cha mourinho lakini fikra zake zimebaki vile vile nitakuwa nakosea?

tokea jose mourinho yupo na ameondoka, amekuja mwengine lakini bado nashangazwa kuona tunaendelea kucheza mdundo wa mourinho kuanzia mashabiki, wapiga kelele, lengends wanaoheshimika, viongozi wa ndani wa klabu na hata vyombo vya habari.
leo hii tetesi zetu zote zinahusu usajili wa beki wa kati kama kipaombele chetu kikubwa, kwa udhaifu wangu wa kuelewa mambo nimebaki najiuliza:

tutakapofanikiwa kusajili walinzi aina ya koulibally na van virgil ndio tutakuwa na timu yenye uwezo wa kusimama na wapinzani wetu wakubwa barani ulaya?

ed woodward amekuwa na tabia za kusajili wachezaji kwa sababu ya mdundo wa muziki, wasiwasi wangu mkubwa msimu ujao atatafuta walinzi wakati kama kawaida yake kwa gharama halafu atatia pamba masikioni, kwa nini asitie pamba masikioni wakati sote tunaimba wimbo mmoja tu aliouanzisha jose mourinho wa kutafuta mlinzi wa kati?

  • hivi jamani tumeridhika namba 7 wetu aendelee kuwa juan mata peke yake msimu ujao?
  • tuna uhakika gani kama alex sanchez atarudi kwenye ubora wake na kuleta upinzani kwa huyu mchezaji wa siku anthony martial?
  • tumeridhika namba 6 wetu aendelee kuwa nemanja matic msimu ujao bila ya kuwa na mpinzani?
  • wakati huu ambao fred haeleweki ina maana tumeridhika kumuona ander herrera mpinzani wake mkubwa akiwa ni scott mctominay?
kuna hii ishu ya jesse lingard ambayo nayo imekuwa ikileta mjadala mkubwa kwa wafuatiliaji wa mpira wa manchester united, wapo mashabiki wanaomchukulia lingard kama ni mchezaji underrated pale klabuni lakini kazi yake anayoifanya ni kubwa sana na wapo wengine wanamchukulia ni mchezaji wa mechi maalum.
pande zote naziona zipo sahihi kihoja zao kwa sababu tulishawahi kuwa na mchezaji mwenye sifa za lingard ambaye ni ji sung park hivyo basi hakuna ajabu kwa lingard kuwepo klabuni.

lakini siamini kama ji sung park aliwahi kucheza mechi tano mfululizo nyakati za SAF na hii inatokana zaidi tulikuwa na wachezaji kama vile giggs, nani, ronaldo ambao walikuwa ni bora zaidi kimfumo. Cha ajabu nyakati hizi mchezaji kama jesse lingard amekuwa ni tegemeo kwenye mechi yoyote na hakuna anayeonekana kujali, na kama yupo anayejali mbona sikutani na tetesi za usajili wa kiungo mshambuliaji?
kwa mtazamo wangu ndani ya klabu yetu tunamuhitaji namba 10 atakayetupa faida ya waziwazi zaidi ya hii anayotupa jesse lingard nyakati hizi za OGS.

nimeona mechi hizi OGS anajenga utatu mtakatifu pale mbele kwa kumweka martial, lingard na rashford, kwa utatu huu kama tusipotafuta namba 10 mwenye uwezo zaidi ya jesse lingard kwenye eneo la juu basi tutaendelea kuwa under dog kwa wapinzani wetu wakubwa barani ulaya, jamani kuna utofauti mkubwa sana unapoziangalia movement za robert firmino halafu ukageuza kioo ukaziangallia movement za jesse lingard pale juu.

nguvu hii tunayoitumia kwa ajili ya kumpigia kampeni ed woodward atuletee koulibally pia tuitumie kwa dhumuni la kumpigia kampeni mwanadamu mwenye sifa za christian ericksen atue manchester united.
tunamhitaji eriksen kuliko yeye anavyohitaji kuishi uwanja wa matofali, tusipokuwa makini majirani zetu watambeba ili akazibe pengo la david silva.

tusihadaliwe na kiza kifupi tukafanya haja zetu njiani tukitegemea hakuna atakayefanikiwa kukiona kinyesi chetu, ni suala la muda tu kila mpita njia atakiona kinyesi chetu tulichokiweka njiani usiku wa jana.

nasubiri comment za kukosolewa kistaarabu zaidi ili na mimi nitolewe ujinga
View attachment 1002065

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GT Belo,umerudi tena pale pale kwenye mtazamo wangu wa kwa nini sipendelei man city abebe tena ubingwa msimu huu kwa sababu tayari hawa majirani kwa kikosi walichonacho wana uwezo wa kubeba ubingwa mara tatu mfululizo jambo ambalo litapelekea majirani zetu kuzidi kutukalia juu wakati ambao tunataka kujikwamua, vile vile kubeba kwao ubingwa ndio kutazidi kumfanya guardiola aonekane ni untouchable na ligi yetu pia ionekane ni ya upande mmoja.

milner, henderson, matip, lovren, origi, lalllana, clyne, sturidge, moreno, ings, gomez n.k
Don Clericuzio na washabiki wenzako wa liverpool FC naomba muwe wa kweli; hivi munafurahia kuona timu yenu imekusanya wachezaji niliowataja hapo juu kama ndio backup yenu na wengineo ndio first eleven?
kama munafurahia basi nitakuwa sipo sahihi kwa kile ninachokiamini

hata muda huu ambao bado hawajabeba ubingwa nawaona liverpool wakiwa ni dhaifu ukiwalinganisha na manchester city, timu inayoundwa na wachezaji hao niliowataja hapo juu kama ndio backup yao pindi linapotokezea tatizo kwenye timu kwa nini nisiwaite dhaifu.
timu ambayo ikitokezea virgil amepumzishwa nafasi yake inachukuliwa na lovren kwa nini isiwe dhaifu?

hata kama liverpool wataingia tena sokoni chini ya matajiri wa kimarekani kwa sera zao za matumizi naamini itawachukua tena miaka miwili ili waweze kuwaondoa wachezaji hao niliowataja na kuwaleta wengine wenye uwezo zaidi ya hao, kimtazamo wangu nawaona liverpool wanasumbuliwa zaidi na tatizo la ukosefu wa wachezaji wengi wenye ubora ukilinganisha na manchester city hata kama itatokezea atabeba ubingwa, na huo ndio udhaifu ambao nauona mimi kama ni faida kwetu sisi msimu ujao endapo kama tutafanya biashara sahihi.

lakini ukija kwa upande wa majirani zetu kwa nguvu yao ya usajili wana uwezo wa kutafuta mrithi wa fernandinho, david silva, vicent kompany kwa msimu mmoja tu bila hata ya guardiola kutakiwa auze kwanza mchezaji ili aongezewe fungu la usajili.

vile vile kwenye ishu ya matumizi sidhani kama liverpool wana uwezo wa kusimama na manchester united kama ilivyo sisi tusivyoweza kusimama na manchester city kimatumizi na si kwa kulinganisha thamani za klabu, hivyo kiupande wetu naamini kama tutafanya biashara sahihi kwa kuangalia zaidi udhaifu uliopo kwenye kikosi chetu upo uwezekano mkubwa wa kufikia level walioionyesha liverpool msimu huu hata kama na wao wataingia sokoni.

mimi naona kuna tofauti ndogo sana kati yetu na liverpool FC lakini kuna utofauti mkubwa kati ya kikosi chetu na kikosi cha manchester city ndio maana sipendelei man city abebe tena ubingwa.
bado akili ya josep guardiola haijachoshwa na maisha ya etihad.

kama sipo sahihi naomba nikosolewe kistaarabu ili ujinga uliomo kwenye ubongo wangu upungue.​
Unafikiri why mashabiki wa Liverpool timu ambayo hawaipendi kuliko zote ni Manchester United ?

I wonder there are United fans who pray for Liverpool to win EPL over City
Ryan Giggs has more trophy than Manchester City,If Pep win at least 2 Champions league with City they will be threat to overtake us ,Jose Mourinho came to England and win back to back EPL with Chelsea but still The Blues are below United

Kuhusu fedha soma hii articles nobody alitegemea Liverpool ingenunua wachezaji 3 kwa kwa almost £200m na kwenye usajili issue sio kutumia fedha nyingi but ni ku-identify players ambao watasaidia ku-improve timu Robertson,Fabinho,Shaqiri hawajanunuliwa kwa fedha kubwa but wameleta impact kubwa sana kwenye timu

Liverpool set to post record profit that could pass £100m

Kwa United kurudi kwenye mafanikio lazima wazifanyie kazi weakness zao kwanza ambazo zinajulikana
 
yeyote atakayechukua ubingwa kiupande wetu maumivu ndio yale yale kinachobaki ni ule upinzani wa mijadala eti yupi ni mume bora kwenye mechi wakati wote wanarusha bakora za hatari.
😎😎😎😛
usiwe na wasi wasi mkuu msimamo wangu hautobadilika haijalishi kama nitakuwa peke yangu, naomba ubebe ubingwa msimu huu tupate kufukazana tena kama bwana yule na mzee wa hard talk.
Mkuu kwenye hilo la kuomba liverpool abebe ubigwa tuko pamoja, mi najua city akichukua vyombo vya habari vitasema sana, utaambiwa "city ni timu kutoka safari nyingine," "PEP sio binadamu wa kawaida".

Lakini pia tukimruhusu City abebe Mara mbili mfurulizo, wataanza kuamini kumbe wanaweza kuifanya EPL kuwa kama Seria A.

mkuu nafahamu vizuri sana upinzani wa kihistoria uliopo kati ya mji wa liverpool na manchester tokea nyakati za mapinduzi ya viwanda, upinzani wao ukafukua mizizi ya chuki mpaka kwenye muziki ambapo wakaazi wa liverpool walivutiwa zaidi na the beatles na wakaazi wa manchester walivutiwa zaidi na Oasis pamoja The Stone Roses japokuwa bendi hizi ziliperform nyakati tofauti.

upinzani huu ulihamia kwenye soka huku kila upande ukiendelea kujijisifia ubora zaidi ya mwenzake kimafanikio jambo ambalo linazidi kuendeleza upinzani kadri muda unavyozidi kusonga mbele.

lakini kiupande wangu siwezi kuwa mtumwa wa historia zao walizopitia hao watoto wa bepari muingereza japokuwa nayafahamu maumivu yatakayotokezea endapo liverpool atafanikiwa kubeba ubingwa msimu huu.

kuna watu wanajificha kwenye kivuli cha historia huku wakijisahaulisha ubora walionao manchester city dhidi yetu kwa miaka 6 hii iliopita.
kuna watu wanajificha kwenye kivuli cha kihistoria wakitulazimisha tuamini ya kwamba liverpool hii ni adui wetu mkubwa kuliko manchester city hii isiyoleta mzaha kwenye uwekezaji wao kwa miaka 10 iliopita.

niwe muwazi nawaogopa manchester city kuliko ninavyowachukia liverpool lakini kwa hali hii inayotukumba nyakati hizi kwangu namuona liverpool ni bora kuliko matajiri wa etihad kwa sababu majirani zetu wametuacha mbali sana kiubora ukilinganisha na liverpool kwa kuangalia mchezaji mmoja mmoja.

Neville: Picking Liverpool or City to win the title is like choosing between two blokes to nick your wife.

tutafanyaje sheikh gary neville wakati mourinho na bosi wake ndio wametufikisha hapa?
 
Ubora wa City haukuja kwa miujiza ni kuwa na plan nzuri na kusimamia utekelezaji wake,Sheikh Mansour baada ya kununua timu alijua challenge iliyopo kupambana na United,Chelsea, Arsenal, Liverpool aliwaleta Txiki na Soriano toka Barca ambao Laporta aliwatumia kutengeneza their greatest team (Barcelona ya Guardiola) so walijua itakuwa easy kumshawishi Pep Guardiola na Messi watue Man City

Pep alivyotua akawaambia nataka defence mpya (Hart,Clichy,Sagna,Kolarov,Zabaleta) wakauzwa sababu wanajua wanachokitaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata wakati wa fergie,scholes alishauri aletwe modric kama mbadala wake dhidi ya schneider na nasri lakini babu aliziba masikio na balaa lake tukaliona. Tusipomchukua majira haya ya joto tusahau tena kuhusu huyu bwana,ataichagua real dhidi yetu endapo ushindani utatokea.
Babu hakuziba masikio kwamba hataki ushauri

Babu alimhanya Levy, chairman wa spurs

Katika deals ambazo United amefanya na Spurs hususani ya Berbatov na Carrick Levy zikikuwa ni ngumu sana. Nakumbuka Fergie alisema maumivu ya kufanya Negotiation na Levy huko nyumba yalimpa maumivu makali kuliko maumivu aliyoyapata alipofanyiwa operation ya hips yake.

So, ukweli ni kwamba SAF alimtaka sana Modric lakini alijua mazungumzo na Levy kumsajili Luka ni almost impossible

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingawa tunasafari ndefu Sana ya kurudi kwenye ubora wetu naimani director of football atasaidia sana sisi kufanya sajili positive na mikataba tutatoa kwa wachezaji wanaostahili tu.... nadhani timu yetu ilipaswa kumpa kibarua mapema director of football kuanzia sasa mpaka March ili aanze kutafuta wachezaji wanaostahili kuja klabuni... Pia kwa rebuild yetu bado naamini Pochettino anatufaa kuliko solskjaer kwani tunakazi kubwa sana ya kurudi on top

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bado Mbappe...Anajua ndy kwaher hivy ndy mana alilia jana
20190124_104902_rmscr-1.jpeg
 
Babu hakuziba masikio kwamba hataki ushauri

Babu alimhanya Levy, chairman wa spurs

Katika deals ambazo United amefanya na Spurs hususani ya Berbatov na Carrick Levy zikikuwa ni ngumu sana. Nakumbuka Fergie alisema maumivu ya kufanya Negotiation na Levy huko nyumba yalimpa maumivu makali kuliko maumivu aliyoyapata alipofanyiwa operation ya hips yake.

So, ukweli ni kwamba SAF alimtaka sana Modric lakini alijua mazungumzo na Levy kumsajili Luka ni almost impossible

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaani huyo Daniel Levy simpendi hadi natamani atoweke tu
 
Neymar jana aliumia kweny mech na aliumia sehem ile ile ya ankle aliyoumia kabla ya kombe la dunia kuanzia..jana alipokua anatoka uwanjan alikua akilia na bado siku kama 20 hiv Psg wakipige na Man U Uefa
Anapenda sana kukaa na mpira aonyeshe madoido kuumia kwake hakuepukiki. Jana kalipiga jamaa kanzu yake ya kunyanyulia mpira nyuma likampiga shuzi hadi mimi mtazamaji nikahisi maumivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani huyo Daniel Levy simpendi hadi natamani atoweke tu
Hahahahahaha

Jamaa ni chizi, angalia mwaka jana alitaka atuuzie Alderwered mwenye miaka 29 kwa £ 75 milioni sawa na VVD wa Liverpool

Unaambiwa akiona mchezaji wa spurs ni mzuri sana na analazimisha aondoke, bora amuuze nje ya uingereza lakini si kuongezea wapinzani wake silaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Neymar jana aliumia kweny mech na aliumia sehem ile ile ya ankle aliyoumia kabla ya kombe la dunia kuanzia..jana alipokua anatoka uwanjan alikua akilia na bado siku kama 20 hiv Psg wakipige na Man U Uefa
Verati naye majeruhi

Rabiot ndio anakula benchi kama adhabu ya kukataa kusaini mkataba mpya (kuna makocha wendawazimu!!)

Sijui kati atapangwa nani hiyo Feb 12

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom