Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Jinsi ya kutamka jina la PAUL POGBA
20181231_120528_rmscr-1.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Kiasi kikubwa yamepungua Kama Sio kuisha yote.

Tatizo lilikuwa uwepo wa Mourihno.

Licha ya kutupa Kombe la UEFA Ndogo na kuturudisha Katika nne bora kushiriki kucheza UEFA.

Soka lililochezwa uwanjani halikuwa la kuvutia, timu ilicheza Mpira mbovu mno, haikuwa Man United tuliyoizoea Au kuitegemea.

Wachezaji walilalamika, Mashabiki tulilalamika, binafsi sikuwa Mpenzi wa soka la Mourihno hata Kidogo.

Tulipishana Katika Falsafa, Mi ni muumini wa soka la Ufundi na uwazi, la kushambulia kwa Kasi na wachezaji kuwa huru kuonyesha uwezo wao binafsi.

Soka la Mourihno lilijaa mbinu ngumu mno, Falsafa ya kukaba Muda wote Ndio iliyotaka kuwapoteza wachezaji wazuri.

Mikhtaryan ameflopy kwa sababu ya Mou, Rashford alilazimika kutumia Nguvu nyingi kuliko akili uwanjani, Martial ye yalimshinda akaanza kulalama sambamba na Pogba.

Tatizo lilikuwa kwa Kocha (Mourihno), wachezaji walilalamika kuhusu Mbinu zakena mifumo aliyotumia uwanjani.

Tuliowaona hata Ma legend wa timu wakikosoa Mbinu zake.

Alitengeneza uwadui kwa Wachezaji na kwa Ma Boss wa Timu, vyombo vya Habari.

Mourihno alikuwa kivuruge Kweli Kweli pale Carrington na Old T.

Alitunyima radha ya kuwa shabiki wa Man United.

Zaidi hakutaka kuziishi Falsafa za Man United, kuwa pale Old T inaanza Man United kisha SAF.

Alitaka kuwa zaidi ya Klabu.

Alitumia zaidi ya pound 400m kukisuka kikosi chake.

Hakuwa Manager Mzuri kote alipopita, Pale Real Madrid pia ilikuwa hivihivi.

Hizi ni timu kubwa zenye mashabiki wa kutisha zenye Falsafa zake.

Alishindwa kutofautisha Kati ya Man United/Rwal Madrid na Chelsea.

Na hata alipokuwa Darajani alikumbana na matatizo ya namna hii.

Sio Muumini wa wachezaji wenye vipaji/Makinda na Sio Muumini wa wachezaji Mastaa, alishindwa kubalance timu/Club.

Kuondoka kwa Mourihno pale Man United kumekuwa na Kheri kubwa kuliko angeendelea kuwa Kocha wetu.

Huyu Mourihno Ndio aliyetaka kutuaminisha hawa akina Mata, Lukaku, Salah, De Burnye, Sterrling kuwa Sio wachezaji wazuri.

Kwangu naamini kumfukuza Mou Klabu imeshusha Mzigo mkubwa sana.

Chini ya OGS hatuwezi kushinda match zote lakini match ambazo tunatakiwa kushinda nina uhakika tutashinda kwa Kishindo Sio kwa kinyonge kwa soka tunalocheza sasa.

Tulianza kufungwa na wajinga wajinga tena hapa hapa Old T.

Tukaanza kuvihofia hata hivi vitimu vidogo, tufungwe na timu Ndogo lakini iwe kwa bahati mbaya, tulikuwa tunafungwa kwa Shida hata Kama hatuchukui ubingwa.

Tulianza kudharaulika, lakini Sasa nina imani hata PSG wataanza kutuchukulia kwa umakini.

#Kheri ya Mwaka Mpya.

Matatizo ya United hayajaisha ingawa kuna improvement kubwa on the pitch ndio maana still kuna proposal ya kuwa na position ya Director of Football kupunguza confusion between executive(CEO+Owner) na technical (manager+players) to allign club philosophy which was missing since post SAF era .Makocha wote waliopewa timu baada ya SAF hawakuanza vibaya so its too early kuanza kushangilia mistake aliyoifanya Woodward ni kumpa kazi Mourinho akidhani labda atabadilika na biggest mistake ilikuwa ni kumuongezea mkataba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka wewe ndo ulianzisha kampeni ya Pogba aondoke..

Ukadai kwamba hawezi kuwa juu ya timu.

Leo unamkubali tena???!!

Huu ni ushabiki wa kinafiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nitatoa mifano

1. Kuna washabiki wa Arsenal walimsifu kwa nyimbo na mapambio Van Persie na Fabrigas lakini baada ya kwenda United waligeuka kuwa Arsenal enemy namba 1

2. Kuna Mashabiki wa United walimdisi Jose akiwa Chelsea (nikiwepo Mimi) lakini alipokuja United walimpenda kama kocha wa timu yetu. Hivyo hivyo mashabiki wa Chelsea walimpenda sana Jose akiwa Chelsea lakini baada ya kwenda United walimdisi sana

3. Tabia za Pogba nje ya uwanja hazifurahishi, tabia ya kujiona yupo juu ya timu inakera, lakini hakuna mwenye wasiwasi juu ya uwezo wake. Hata hivyo, haimaanishi hawezi kusifiwa akifanya jambo jema kwa timu tunayoipenda.

OPINIONS CHANGE WITH TIME, OPINIONS CHANGE WITH CIRCUMSTANCES AS LONG AS PEOPLE ARE DYNAMIC CREATURES

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Matatizo ya United hayajaisha ingawa kuna improvement kubwa on the pitch ndio maana still kuna proposal ya kuwa na position ya Director of Football kupunguza confusion between executive(CEO+Owner) na technical (manager+players) to allign club philosophy which was missing since post SAF era .Makocha wote waliopewa timu baada ya SAF hawakuanza vibaya so its too early kuanza kushangilia mistake aliyoifanya Woodward ni kumpa kazi Mourinho akidhani labda atabadilika na biggest mistake ilikuwa ni kumuongezea mkataba.
Umenena vyema mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kabisa hakuna kitu iliniuma kama kuwauzia arsenal mikhitarian wetu. Na mpk sasa kinaniuma hivi daah. Basi tuu.
Mourinho anapenda sana battles. Pamoja na hayo pia sikua nafurahishwa na tabia ya pogba kuwa na kiburi nankutaka kuwa mkubwa zaidi ya club. Anaamini kwamba ni mchezaji mkubwa sana ila kiukweli bado sana. Hajaarchieve bado mengi. He should kwep the low key.

Ila fresh tuu. Nafurahia attacking football. Nasubiria tucheze big match na giants wenzetu nione kama itakua same spirit

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jose Mourinho thank you for buying Pobga, Bailly, Linderlof, Fred. Matic, Dalot, Lukaku
Mourinho thank you for keeping De Gea, Ander Herrera, Young . Pereira
Mourinho thank you for believing in Lingard when no one believed in him and also for believing in Rashford when everyone said he wasn't qualified to be a man united player and for the boldstep to hand him the number 10 shirt.

I could see Rashford running and putting pressure on the the opposition when we lose the ball . Thank you mourinho for that and also Luke Shaw defending so well.

Also thanks for the trophies and for
making man united to be considered a title contender for the first time since Sir Alex left. All this Without a Director of football.

Ed Wood. Thank you for sacking mourinho and bringing in Ole and thanks for the fund you provided to mourinho, it seems he didn't really waste the fund.

Ole thank you for bringing joy,
football and happiness back at Old Trafford

Man united for life
 
Ni ngumu kwa Man United kushinda Ubingwa wa Ligi kwa Hatua tukiyopo Sasa, na Kama itatokoea itakuwa ni miujiza ya Karne, Sio rahisi hata kidogo.

Lakini kuingia Top 4 sina Shaka napo hata Kidogo, tuna kikosi kizuri mno chanye mchanganyiko mzuri.

Tumeachwa point nyingi na kupoteza point nyingi.

Tuone round ya Pili itakuwaje.

Klopp Sio mzuri Katika kumaliza Ligi Au kushinda Fainal anajua madhaifu yake kitu Ambacho hataki Sasa kitokee.

Liver inaweza kupoteza michezo kadhaa lakini Sio saba.

Kwangu naamini bingwa Safari Hii ni Kati ya Liverpoo, Man City Au Chelsea lolote linaweza kutokea.

Man United sina wasiwasi na kuingia Katika Top 4, Pochetino Sio mzuri Katika kumaliza Ligi licha ya kuanza vizuri.

Asernal Sio timu ya kushindana ina mapungufu Mengi Katika wachezaji iliyonao, hawana kikosi kipana sana, wanazidiwa hata na Totenham.
Unazungumzia gape la point 19, maana yake kati ya michezo 18 iliyobaki Liverpool apoteze 7 na Man Utd ashinde yote 18.

Ukumbuke hapo unazungumzia timu ambayo haijapoteza mchezo hata mmoja vs timu iliyopoteza michezo 5.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NEMANJA MATIC " THE TOWER"
Kila nikijaribu kufumba macho naona utamu wa magoli ya pogba na nakshi nakshi kwa pass zake murua achana na ile shangilia yake ubora wa man utd unachangiwa kwa kiasi kikubwa sana na role kubwa inayofanywa na nemanja matic eneo la kati mi binafsi namwita the tower au mnara kwa kiswahili Jamaa ndio connector wa mipango ya man utd kuanzia eneo la ulinzi kuja juu kwenye final third kwa haraka haraka na macho mawili huwezi kuona Kazi kubwa inayofanywa na matic ila kwa jicho la tatu utaona nachokimaanisha achana na ule mpasi kwenda kwa martial then martial kwa rashford mpira kambani uwezo na utulivu wa matic kwa kushirikiana na Herrera unamfanya pogba acheze in a free role nadiriki kusema pogba ni miongoni mwa wachezaji watatu hatari zaidi ndani ya EPL endapo utamwacha acheze free waswahili wanasema chumvi haina sifa kwenye chakula hadi izidi au ipungue kwang Mimi matic ni chumvi iliyokolea kabisa kwenye kiungo cha man utd maybe siku ikipungua wengi mtagundua ni kwa kiasi gani Jamaa anachangia tabasamu usoni mwetu all over the world

Sent using Jamii Forums mobile app
Naunga mkono hoja

Ila kuwa makini, kuna watu watakuita pro Jose humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakumbuka wakati timu imepoteana chini ya mou,kila idara ilionekana inahitaji marekebisho na hadi kufikia baadhi ya watu kutaka aina flan ya wachezaji wauzwe hawana hadhi ya kuichezea united. Lakini leo hii timu iko vizuri hao hao wachezaji wanaonekana mou alikuwa anawafuja kwa mbinu zake,sasa wanadeliver.
Herrera chini ya mou alionekana wa kawaida au mchezaji wa kumlinda mtu mmoja dakika zote 90,lakini leo hii anazurura uwanja mzima na maajabu yake sitaki kuyaongelea zaidi.
Kwa sasa timu inapata matokeo ya goli 3+ bila clean sheet tunajiaminisha kuwa defence yetu bado,lakini tungepata clean sheet walau 2 kati ya hizo game 3 usingeona ukosoaji humu. Ninachotaka kuwauliza mashabiki wenzangu humu,defence ya city,Chelsea na Liverpool inakipi cha ajabu kuliko united? Ederson,keppa na becker wanakutana na michomo mingi na kutokea pembe zote kama ilivyo kwa de gea,sema bahati yetu haijafika tu kupata clean sheet.
Nina imani kama ilivyo kwa safu yetu ya ushambuliaji kuwa kwenye wakati mzuri,itafikia zamu ya ulinzi pia kwa uimara zaidi ya huu aidha kwa mwalimu kuongeza mbinu au kujitoa kasoro ndogo walizo nazo wao wenyewe.
Tangu zama za mou,defence ilikuwa mbovu sababu tulikuwa tunaruhusu kushambuliwa zaidi tena karibu na lango letu.
Tumpe muda huyu jamaa aseme mwenyewe kama anataka striker,kiungo au beki. Siye tupate matokeo mazuri na burudani toka kwa solskjaer hayo mengine ni zaida tu
GGMU
 
Nitatoa mifano

1. Kuna washabiki wa Arsenal walimsifu kwa nyimbo na mapambio Van Persie na Fabrigas lakini baada ya kwenda United waligeuka kuwa Arsenal enemy namba 1

2. Kuna Mashabiki wa United walimdisi Jose akiwa Chelsea (nikiwepo Mimi) lakini alipokuja United walimpenda kama kocha wa timu yetu. Hivyo hivyo mashabiki wa Chelsea walimpenda sana Jose akiwa Chelsea lakini baada ya kwenda United walimdisi sana

3. Tabia za Pogba nje ya uwanja hazifurahishi, tabia ya kujiona yupo juu ya timu inakera, lakini hakuna mwenye wasiwasi juu ya uwezo wake. Hata hivyo, haimaanishi hawezi kusifiwa akifanya jambo jema kwa timu tunayoipenda.

OPINIONS CHANGE WITH TIME, OPINIONS CHANGE WITH CIRCUMSTANCES AS LONG AS PEOPLE ARE DYNAMIC CREATURES

Sent using Jamii Forums mobile app
At least kwa mbali saana nimekuelewa na sio radika ana andika andika pumba tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni ngumu kwa Man United kushinda Ubingwa wa Ligi kwa Hatua tukiyopo Sasa, na Kama itatokoea itakuwa ni miujiza ya Karne, Sio rahisi hata kidogo.

Lakini kuingia Top 4 sina Shaka napo hata Kidogo, tuna kikosi kizuri mno chanye mchanganyiko mzuri.

Tumeachwa point nyingi na kupoteza point nyingi.

Tuone round ya Pili itakuwaje.

Klopp Sio mzuri Katika kumaliza Ligi Au kushinda Fainal anajua madhaifu yake kitu Ambacho hataki Sasa kitokee.

Liver inaweza kupoteza michezo kadhaa lakini Sio saba.

Kwangu naamini bingwa Safari Hii ni Kati ya Liverpoo, Man City Au Chelsea lolote linaweza kutokea.

Man United sina wasiwasi na kuingia Katika Top 4, Pochetino Sio mzuri Katika kumaliza Ligi licha ya kuanza vizuri.

Asernal Sio timu ya kushindana ina mapungufu Mengi Katika wachezaji iliyonao, hawana kikosi kipana sana, wanazidiwa hata na Totenham.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hapa umeongea kisoka kabisa.

Maana baadhi yenu mumeanza na kudai ubingwa ni wenu. Hahaha hata top four bado mna wakati mgumu japo mkipambna sana mnaweza kufua dafu.

Kazi mliyonayo kqa sasa ni kutengeneza kombinesheni nzuri maana Josee alivuruga timu kabisa, angalia kama uwezo wa Matic kushuka, Rashford, lingad ..yani Man united hakuna hata haja ya usajili maana mna kikosi kipana sana ..pengine kuliko timu yeyote Ingilandi.

Mlikosa uongozi bora tu ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom