umetukumbusha mbali sana brother, ile mechi kama naiona kwenye mfumo wangu wa ufahamu muda huu.
nakumbuka kipindi cha pili SAF alimuingiza anderson na tom cleverley eneo la kiungo na pembeni alikuwepo luis nani pamoja na ashley young akiwa kwenye ubora wake mechi za mwanzoni kabla hajapata majeruhi nyakati hizo ndio tunamsajili kutoka aston villa.
ile come back ilikuwa ni noma sana.
yaya toure baada ya kuingiziwa mjinga mwenziwe anderson anayejua kutembea na mipira aliomba mpira umalizike si unajua jamaa akikutana na box to box wenzake anakuwa mnyonge sana.
kwa mfano anapokutana na watu kama ramirez yule wa chelsea au moussa dembele mjomba toure utamuonea huruma.
mwanzoni mwa ligi tulianza vizuri sana lakini majeruhi ya anderso, cleverley, nani, jones yakaturudisha nyuma mpaka tukachukua mzigo wa goli 6 kwa majirani.
huwezi amini mwisho wa msimu man city walichukua ubingwa kwa tofauti sijui ya magoli au pointi 1?
fergie akaona kumbe timu tatizo ni striker rooney na wenzake wameanza kuchoka.
ok ngoja nimsajili robin van persie anirudishie ubingwa wangu halafu niwaachie balaa lenu si munasema nimekuwa mbahili siku hizi.
hehheheheheeee
dah yule mzee sijui alikuwa ni mchawi?