Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ila Hazard bhana...Moja haikai, Mbili haikai...... Soma hii mpya.

Eden Hazard ameweka wazi majuto yake ya jinsi gani muda wake na Jose Mourinho ulivyoisha na kuthibitisha kwamba anataka kufanya kazi tena na kocha huyo wa Man United.

Akifanya mahojiano na gazeti moja la nchini Ubeligiji HLN, hapo jana , Hazard alisema:

"Katika miaka 12 nilikuwa na msimu mmoja tu ambao mbaya, miezi sita ya mwisho chini ya Mourinho na kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni kosa langu . Baada ya kutwaa Ubingwa tulimuomba Mourinho kuongeza muda wa mapumziko . Nilirudi klabu nikiwa ovyo kabisa kimwili."

"Msimu wa mwisho chini ya Mourinho hakuwa wa furaha . Hatukuwa tunashinda. Tulikuwa tunafanya mazoezi bila kufurahia, ni ilikuwa kitu kizuri kwa pande zote mbili tuachane ( Klabu Vs Mourinho ) . Lakini kama nikiulizwa sasa hivi ni kocha gani natamani nifanye naye tena kazi , nitasema Mourinho."

" Sijutii vitu vingi sana katika maisha yangu ya soka , lakini moja ambalo najutia ni kutofanya kazi tena na Mourinho pale Chelsea. Tulikuwa na timu ambayo ingeweza kutwaa mataji mengi zaidi . Tuliishia kwenye mzunguko hasi ."

" Nilimtumia ujumbe wa simu kumuomba msamaha baada ya kufukuzwa , sikuonesha kiwango kizuri sana, tulifurahia mafanikio pamoja, nilikuwa mchezaji bora wa mwaka , halafu msimu uliofuata sikuonesha kiwango kizuri."

Hazard ameongeza kwa kutetea staili ya uchezaji wa Mourinho kwa kusema:

" Picha ya Mourinho ambayo watu wengi wanaamini ni kocha wa kujihami sana sio sahihi. Sio wa kucheza sana soka la kushambulia kama Pep Guardiola , lakini ule msimu ambao tulikuwa mabingwa , tulifunga magoli mengi sana na tulicheza mechi nzuri sana."

" Kama matokeo yakianza kuwa mabaya , lazima atakosoa wachezaji wake, lakini nilishaanza kuzoea na kukubali kwasababu ndio alivyo hivyo huwezi kumbadilisha."

" Lakini ukiwa unashinda mechi, Mourinho anakuwa kocha mzuri sana huwezi kuamini, anakuwa rafiki yako , unaweza kufanya chochote unachotaka , ukitaka siku moja ya kupumzika , anakupa mbili."
Amemwelezea vizuri mourinho kwa kweli ndivyo alivyo mourinho siku zote
Man united pogba, martial, na wengine inabidi wamzoee
Lakini atakutana nae tarehe ishirini amemsifia ili aache kupaki basi ili amfunge vizuri
 
Ukisoma alichosema hazard kaanza kutoa siri jinsi mourinho alivyomwambia ajitume lakin kwa unafik wao walikuwa hawatak wanataka kocha atoke tuwe makini na wachezaj kuna muda hawatak kujituma

Ndo mana zlatan kasema kuna watu wanafik matatizo yao wanayaficha nyuma ya migongo ya wenzao
Chuki ilikuwa kubwa sana baina ya mourinho na hazard
Na ishu ilianzia wakati kale kadokta ketu ka kike kanawahi kwenda kumtibu uwanjani
Inasemekana kale kadokta kanachua vizuri kwa hiyo wachezaji walikuwa wanajifanyisha kuumia ili aingie uwanjani kuwananiliu
Mourinho akashtukia mchezo hapo ndipo walipoanza kumgomea jumla
 
Amemwelezea vizuri mourinho kwa kweli ndivyo alivyo mourinho siku zote
Man united pogba, martial, na wengine inabidi wamzoee
Lakini atakutana nae tarehe ishirini amemsifia ili aache kupaki basi ili amfunge vizuri
Hapana mourinho hawez kuacha kupak bus hiyo ndo style yake hazard roho imemsuta kweli alikuwa hovyo sana kipind kile baada ya kubeba ndoo saiv kafunguka baada ya kurud kwenye kiwango chake anafuraha lakin kipind kile alifukuzwa had kocha lakin bado hakuwa mzur mkuu eden kimario hazard kachukua uchezaj bora mkiwa na huo mfumo migomo ya wachezaj ni mibaya
 
mkuu ahsante kwa majibu yako yenye kujitosheleza ila kupitia majibu yako nimebaki najiuliza swali ambalo mpaka muda huu sijapata majibu sahihi kupitia maarifa yangu madogo nilionayo
hivi hizi comment zako umedhamiria kumsifia romelu lukaku au umedhamiria kumponda romelu lukaku kinyume nyume?

kuhusu utengenezaji wa nafasi za kufunga kwenye klabu yetu ni ukweli ulio wazi ya kwamba wachezaji wetu kwa kiasi kikubwa wanapoteza umakini wanapofika maeneo ya adui jambo linalochangia zaidi kuwa na takwimu zisizoridhisha za utengenezaji wa nafasi za kufunga kwa romelu lukaku, hata hivyo unakuta kwa kiasi kikubwa nafasi hizo chache zinazotengenezwa romelu lukaku anazipoteza hususani zile anazobaki na mtu mmoja pamoja na goli kipa, jaribu kurejea mechi ya tottenham hostpurs, burnley, west ham, wattford na wolves.

manchester united amecheza mechi 42 amefunga magoli 20
everton amecheza mechi 141 amefunga magoli 68
belgium amecheza mechi 78 amefunga magoli 45

wastani wa goli 1 kwa mechi 2.

umesema jana ametengenezewa nafasi tano amefunga magoli mawili.
hahahahahaaaaaa.
ahsante sana mkuu kwa hili jiwe ulilonirushia
mvumilieni lukaku
 
Hapana mourinho hawez kuacha kupak bus hiyo ndo style yake hazard roho imemsuta kweli alikuwa hovyo sana kipind kile baada ya kubeba ndoo saiv kafunguka baada ya kurud kwenye kiwango chake anafuraha lakin kipind kile alifukuzwa had kocha lakin bado hakuwa mzur mkuu eden kimario hazard kachukua uchezaj bora mkiwa na huo mfumo migomo ya wachezaj ni mibaya
Nakubaliana na wewe lakini pia amemwelezea mourinho kwa usahihi kabisa
 
Jamaa kaongea point chelsea ya sasa inategemea nguvu ya hazard maana willian na pedro bado hawapo vizur siku huyu asipokuwa vizur basi timu inalala angalia gem anazotekea banch au asipocheza mnapata tabu sana
Nyie mnamtegemea Nani..?
 
Kupanga ni kuchagua
FB_IMG_1539501978864.jpeg
 
Hahahahaha!! Kimoyo kimefanya fyaaaaa!!! Nitatoka salama halafu utashangaaje nimetokaje tokaje?nimewezaje wezaje? Wakati vigezo vyote unavyo? Hahahahaha......game tamu sana hilo can't wait it....!!!
Ha ha ha ha....

Uwanja mzima utaenea moshi wa masigara wa Sarri....

Hautoki nakwambia.... Yani yani Baba yako Mourinho ata pata tabu sana.

Niambie best, upo poa?
 
Tunaye Dalot tayari pamoja na Matteo Darmian
Matteo Damian mbona alisema wazi anataka kuondoka Man United ila Mourinho akambakiza kwa lazima na ndio maana jamaa hachezi juve, inter, fiorentina zilikuwa zinamhitaji
 
Back
Top Bottom