baada ya takribani wiki mbili za majonzi na dhihaka kupita angalau jana pro mourinho walilalala kwa furaha na amani iliojaa kwenye nafsi zao wakiongozwa na manahodha wao
radika na
Cole Williams ambao wameonyesha msimamo usiyoyumba kwa kile wanachokiamini, hahahahahaaaaaa hongereni sana pro jose mourinho ila musisahau vita hii ngumu ndio kwanza inaendelea na kwa wale tunaopuliza pande zote mbili acha tuendelee kufurahia comeback ya ukweli ilio onyeshwa na vijana kwa siku ya jana.
Nafahamu ya kwamba muda huu anti mourinho wote wamekata moto kwa kiwango fulani lakini musiwe na khofu wiki mbili zijazo kuna balaa la chelsea, juventus na manchester city. Kama atachomoa mechi hizi tatu basi wapinzani wa jose mourinho nyote kwa pamoja mutalazimika kumtafuta haraka haraka wa jose mourinho anayepatikana humu JF kwa dhumuni la kuunga mkono juhudi za jose mourinho.
Naamini pande zote mbili muda huu zinasubiri kwa hamu ifike January 2019 kwa sababu:-
- ed woodward atafanya kila njia ajiondoe kwenye huu mtego alionasa uliowekwa na jose mourinho na wafuasi wake ambao hadi jana pia tuliwaona uwanjani wakimponda, hivyo basi atahakikisha dirisha dogo la usajili anatafuta japo wachezaji wawili.
- jose mourinho kiupande wake itakapofika mwezi january hizi kelele zinazoendelea zinazotaka afukuzwe zitazimika ghafla kama mshumaa pindi upepo unapovuma, pengine huenda ikifika mwezi january tutakuwa tupo nafasi angalau ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu (tuombe hivyo inshaallah) jambo hili litazidi kuchochea kushuka kwa presha inayomkabili mourinho na wachezaji wote muda huu.
nadhani njia pekee itakayoweza kuondoa mvutano uliopo kati ya pande mbili hizi ni kuhakikisha tunamaliza nafasi ya nne ya msimamo wa ligi kuu ili tupate nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao tupate kujipanga na msimu unaofuata bila ya hivyo jose mourinho atawajibika na hata ed woodward atapaswa kuwajibika.Tukiachana na vita ya wenyewe kwa wenyewe inayoendelea muda huu kwenye klabu turudi tena kwenye mechi ya jana
hivi hili suala la wachezaji wetu kupoteza mipira ovyo wanapofika kwenye maeneo ya adui tatizo ni mbinu za kocha au wachezaji wetu kukosa ubunifu wa kutosha?
- ukiziangalia timu kama barcelona, manchester city, liverpool na hata real madrid ya msimu uliopita wanapofanya mashambulizi ni nadra sana kukuta wanapoteza mipira ovyo haijalishi timu pinzani wameweka ukuta wa chuma lakini kwetu sisi ni tofauti kabisa, ndio maana imekuwa vigumu sana kiupande wetu kuifunga timu pinzani magoli zaidi ya matatu kwenye mechi kwa kukosa kwetu umakini. marcus rashford, romelu lukaku, martial, alex sanchez hawa watu inafika nyakati wanakufanya utamani kuangalia mbio za farasi kuliko mpira wa manchester united, kasi yetu ya ufungaji wa magoli inazidi kupungua siku hadi siku.
waheshimiwa mumeionaje formation ya 1- 2 - 4- 3
kwa mtazamo wangu mimi nadhani ni bora zaidi kutumia formation hii tunapocheza na hizi timu ndogo zisizokuwa na viungo wabunifu hususani tukiwa uwanjani kwetu kuliko kutumia formation ya kujaza walinzi 6 kama alivyofanya jose mourinho kwenye hizi mechi tatu za mwisho.Timu nyingi za uingereza ukizichezea mpira wa kushambulia kidogo tu zinachanganyikiwa na hatimaye huishia kujilinda, makocha kama guardiola, sarri ball na klopp kwa kiasi kikubwa wameutumia udhaifu huu wa timu za uingereza kwa kuhakikisha wanaweka nguvu kubwa kwenye kushambulia kuliko kujilinda zaidi.
unapocheza na hawa wazembe kama mark noble, shelvey, lallana, gana idris na huku unajilinda ni ujinga zaidi ya kulala na kahaba bila ya kinga
shaw + matic + pogba + fred / fellaini / herrera + martial + mata fundi + sanchez = sexy football
waliokaribu na jose mourinho wajaribu kumwagia angalau ndoo 50 za maji baridi ili aondokane na huu usingizi mzito wa kujilida ovyo
- They [the board] gave me a contract until July 2020. I have a contract to 2020, I didn't point a pistol at them. They give me the contract because they wanted to give it me."
- As a friend of mine was saying to me this morning, if tomorrow it rains in London it is my fault
- If there are some difficulties with the agreements of Brexit, it is my fault
- You can win, you can lose, but that dignity must always be there.
One Life, One Love, One Club.
Glory Glory Manchester United.