kwa nini awe ander herrera na si marouanne fellaini?
kama mourinho ataendelea kushinikiza kumuongezea mkataba fellaini nitamuona ni mwanadamu wa ajabu sana.
tunahitaji wachezaji ambao wana uwezo wa kucheza kwenye hali ya kiwango cha juu kwa msimu mzima hapo ndio tutaweza kupambana na manchester city, na bahati mbaya fellaini hawezi kukupa huduma hiyo
kwenye timu yetu tuna wachezaji wawili tu ambao wana uwezo wakucheza kwa kiwango bora kwa msimu mzima ambao ni david degea na nemanja matic.
wachezaji wote waliobakia ni homa ya vipindi kwa kuanzia mchezaji wetu ghali paul pogba ambaye hajawahi kucheza kwenye kiwango cha juu kwa mechi 10 mfululizo.