Mie nimeiona kazi ya fundi herrera kuwakata pumzi city kwa kukaa na mipira mguuni hivyo kusababisha wapanic. Nadhani ndio mchezaji anayeongoza kwa kuchezewa faulo nyingi kwenye derby ya leo.
GGMU.
Sawa sawa na amewapa yellow card 2 kama sio 3
 
Hivi Wewe Huwezi Kupost Kitu kwenye Uzi Wenu Bila ya Kuihusisha Liverpool?

Huu Ni Uzi Wa Man U, Na Liverpool tuna Uzi wetu! Kama unataka Kuiongelea Liverpool basi Njoo Kwenye Uzi Wetu Wa Liverpool ili members wote wazione post Zako ujumbe uwafike.

Mkuu Liverpool sio iliyokuzuia Mafanikio ya Ubingwa Msimu huu! Kwahiyo huna haja ya Kuilalamikia.
Nani aende kwenye uzi wa wazee
 
Nani aende kwenye uzi wa wazee


Tukiwita nyinyi Ni Watoto huwa Munabisha! Nashukuru Umeacknowledge Kuwa sisi Ni Wazee.
We have matured enough kuliko Nyinyi Ndiyo Mana Since 2006 hatujapata Mshabiki Mpya hasa wale Watoto U17 kama Wewe.
 
First time since 2010-11 Manchester United have won against every single opposition in a Premier League season.
30264823_1866139896779312_4911166064978558976_n.jpg
 
Manchester United imewaduwza Manchester City baada ya kutoka nyuma kutoka 2-0 hadi kuibuka na kushinda mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Etihad.

Man United iliyokuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi mapumziko ilibadilika kipindi cha pili baada ya Paul Pobga kufunga mabao mawili ndani ya dakika mbili na kufanya matokeo 2-2 na kufuta yale ya City Vincent Kompany na Ilkay Gundogan.

Beki Chris Smalling aligeuka shujaa baada ya kufunga bao la tatu akiunganisha kwa umakini krosi iliyopigwa na Alexis Sanchez na kuwapa ushindi muhimu Manchester United.

Historia ya miaka sita iliyopita ilijirudia wakati Kompany alipofunga bao la kichwa akiunganisha kona Leroy Sane.

Kama ilivyokuwa Aprili 2012, Kompany amefunga bao la kichwa kwenye Uwanja wa Etihad dhidi ya Man United akiwa nakabwa na mtu yuleyule Smalling na kufunga bao la kuongoza kwa wenyeji katika dakika 25.

Wakati Man United wakijiweka vizuri na mchezo huo kiungo Ilkay Gundogan alifunga bao la pili kwa Man City baada ya kupokea pasi Raheem Sterling na kupiga shuti la chini lilomshinda kipa David De Gea na kujaa wavuni.

Kipindi cha pili Manchester United waliamka na kutawala mpira na dakika 52, Pogba alifunga akimalizia kazi Alexis Sanchez aliyetoa pasi kwa Ander Herrera, aliyemgongea Pogba aliyeusukuma mpira wavuni na kumwacha kipa Ederson asijue la kufanya.

Dakika moja baada Sanchez alipitisha krosi ndefu iliyomkuta Pogba aliyeunganisha kwa kichwa na kufanya matokea kuwa 2-2 jambo lililozima shangwe za mashabiki wa City kwenye Uwanja wa Etihad.

Beki Smalling alifunga bao la tatu na kuhakikishia Man United ushindi mnono wa mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Etihad.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Back
Top Bottom