Ng'wanza Madaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2008
- 2,268
- 338
Poleni watani,hii ni aibu kubwa sana kutokea ndani ya OLD TRAFORD nina imani mta bounce back, Kila la heri. Ila mpunguze kuongea sana.
Kwa kweli tatizo kubwa kwa Man Utd ni kiungo (No. 6) mwenye nguvu ya kukaba na pumzi ya kupeleka mashambulizi mbele, Anderson anaweza kukaba na kushambulia lakini hana pumzi ya kutosha kupanda na kushuka, Fletcher hana nguvu za kutosha, Carrick Mpole sana, Cleverly mwepesi kupanda na kushuka lakini hana nguvu. So lazima babu atafute kiungo aina ya Roy Kean mwenye kumudu vurugu za katikati lakini kwa kipindi hichi cha mpito inabidi Phill Johns achezeshwe kama kiungo mkabaji hasa kwenye mechi ngumu.
man 6 hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee! imenikumbusha mwaka 1930.ddk za nyongeza mlipigwa bao ngapi jana jamani humu? kweli jana ilikuwa siku nzuri kwetu arsenal adui muombee njaa
Mkuu kile kibano cha jana, tena nyumbani kilikuwa kibaya sana. Sielewi ilikuwaje wachezaji wetu wakachoka kiasi kile!! Yani noisy neighbours walikuwa wakitengeneza shambulizi hadi wavu utikisike??
Pamoja na kutokuwa na kiungo shupavu wa ukabaji lakini bado utaona kwamba jana timu yetu ilikuwa na performance ya chini sana. Hata kiungo cha ushambuliaji hakukuwa na kitu uwanjani hadi rooney na welbeck wakalazimika kurudi kucheza deep na kwahivyo kutokuwepo mashambulizi ya kueleweka. Rio ndo kabisaaa choka mbaya, sijui kwa nini SAF haoni hilo!
We nawe haujatolewa out leo?
Yani umekataa kutolewa out na wanaume ili ushangilie ushindi wa man city!!
Khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee mkuu mashoga wako OT au unatafuta mafioso wakuuzie unga, hao utawapata kwenye cowshed wakiuza unga si ulichikia jana Chelsick JT aliwapa unga mara mbili zaidi hapa naona umepotea njia.
![]()
Na hawa ati wanajiita wanaune phew!
Nenda muulize mod wenu atakuelekeza kwa kuwapata mimi na mashonga mbali mbali khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Inauma sana lakini nashangaa vibonde wetu Arse8 wanapiga kelele sipati picha kama wao ndio wangetufunga ingekuwajie.Wao tulishawafunga 6 then 8 still wanapiga kelele ngoja tusubiri wao watakavyocheza na hao wanaowashangiliaPOLENI WATANI....
huwa waswahili wanasema kuti la mazoea humuangussha mgema........ at least you didnt lose to a juvenile club like asenane
Duuhh poleni sana mashetani Belo, Belinda, Eqylipz na wengine........hiki kipigo ni kitakatifu......defence yenu leo ilikuwa mbendembende.......yule Evans hafai kabisa kuwa defender wa ManU..........