ANDER HERRERA,JICHO LA SIR BOBBY CHARLTON, ANAYEOZEA KWENYE MBAO ZA OLD TRAFFORD:-
Imeandikwa Na Doct WA Man Utd Ilikua usiku wa tarehe 8 mwezi Mach 2012, round ya 16 kwenye mashindano ya Europa league. Manchester United wakiwa Old Trafford chini ya Sir Alex fergeson,wakiwakalibisha Athletic Bilabao . Karibu wachambuzi wote waliamini ubora wa kikosi cha united kuliko Athletic Balbao, Wengi waliamini United ni kama wamepata mchekea na watapita kwa urahisi . Baada ya dikika 90 kila mtu hakuamini kwa kile kilichotokea ,Manchester akiwa Old Trafford alikutana na kipigo cha mabao 3 -2, tena kwa kuchezewa mpira mkubwa mno . Kikosi cha Ferg kilionekana ni cha kawaida mbele ya vijana wa Bilbao, Ander Herrera ,De Marcos ,I Munian ,Martinez pamoja na Liorente kijana katika ubora wake, walikua moto zaidi mbele ya mkongwe Ryan Giggs , Michael Carrick ,Rooney ,chicharito ,Luis Nani . Huu ndio mchezo ulionifanya nimjue kiungo fundi wa mpira Ande Herrera ,michezo yote miwili aliweza kuwafunika viungo wa Man united . Alicheza kama kiungo wa kati muda mwingine alikua akicheza kama kiungo mshambuliaji nyuma ya Liorente . Herrera alionyesha ubunifu na uwezo wa kusoma mchezo kwa haraka , na zaidi karibu mipango yote ya kimfumo ya Ferg iliishia kwa Herrera . Baada ya hapo nikaanza kuifutilia A. Bilabo kwenye michezo ya La liga ,na ndipo nilipomjua zaidi Herrera . kiuhalisia Ander Herrera ni kiungo mchezeshaji au wa kati,anauwezo wa kupiga chenga ,anauwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kukokota na vile vile anauwezo mkubwa wa kupiga mipira mirefu . Kipaji maridha cha Herrera ndicho kilichomshawishi sir boby Charlton aushawishi uongozi kumsajili..... ndio.. huyu huyu Legend wa Manchester United . Unaweza kuwa unajiuliza sir Bobby Charlton ni nani ...Acha nikwambie kidogo kuhusu legend. Historia inavyotuambia kuwa ni moja ya viungo washambulaji bora kabisa kuwahi kutokea Dunian ,alifanya makubwa sana miaka ya 1960 na aliwahi kuchukua tuzo za Balloon de or, piah alikuepo kwenye kikosi cha uingereza kilichobeba world cup 1966 . Miaka hiyo ya giza aliwahi kuwa mchezaji bora wa dunia mbele ya Eusebio. huyu ndiye Bobby Charlton kwa ufupi. Tuendelee na mada yetu . Baada ya Manchester united chini ya David Moyes kuwa na matekeo mabovu, ndipo Sir Bobby Charlton akatoa ushauri au akapendekeza kuwa, ili united irudi kwenye ubora wake inamuhitaji kiungo kama Ander Herrera ,mwenye nguvu,kasi na ubunifu mwenye uwezo wa kuunganisha kwa usahihi eneo la kati na ushambuliaji . Kumbuka kipindi hicho United ina Shinji kagawa pamoja na Wayne Rooney ambao walionekana kushindwa kufanya kile ambacho timu ilikua inakosa .. Ndipo Bobby Charlton akapendekaza kwa kuuwambiau uongozi,kuna kijana yupo Athletic Bilbao anafaa sana na amemfuatilia siku nyingi . kutokana na heshima aliyonayo mzee ndani ya klabu , Uongozi ulikubali mara moja wazo lake na kulifanyia kazi , mwezi November 2013 klabu ya Manchester united ilipeleka ofa ya £23 million kwa Athletic Bilbao , lakini uongozi wa klabu haukuwa tayari kumuachia Herrera na matokeo yake ofa ile ikakataliwa . Baada ya mkumkosa herera ndipo klabu ya Manchester united ikahamia kwa Juan Mata na kumsajili kutokea Chelsea . Baada ya msimu kuisha Manchester united iliachana na kocha wake david Moyes . Sir Bobby Charlton bado aliendelea kuushawishi uongozi juu ya usajili wa Ander Herrera japo United walikua wameshampata Juan Mata ,sijui ni kitu gani ambacho Legend huyu alikiona kwa Herrera, lakini kiuhalisia Herrera wa A.Bilbao alikua ni fundi hasa . Baada ya United kuachana na Moyes walimtangaza Luis Van gaal kuwa kocha mkuu . kipindi van gal yupo na timu ya taifa ya Holland akiendelea na majukum yake, klabu ya Manchester united ilikua ikifanya mawasiliano na Ander Herrera . 16 mwezi June 2014 timu ya taifa ya Holland chini ya Van gaal ikatolewa nusu final na Argentina ya akina Messi, baada ya siku 2 klabu ya Athleti Bilbao wakatangaza kuafikiana na klabu ya Manchester united juu ya usajili wa Herrera ( £28.85:Mil), kisha 26 June akatangazwa rasmi . Watu wengi wanatambua kuwa usajili wa kwanza wa kocha luis Van gaal ni wa Herrera, lakini kiukweli Herrera wakati anatua United Van gaal alikua haajanza majukumu rasmi na United. Kwa Ufupi unaweza kusema usajili wa Herrera ni wa Bobby Charlton ,aliona Herrera anakitu cha kuja kuisaidia Man utd. hakuishia hapo Bobby Charlton. Alihakikisha taratibu zote usajili alizisimamia yeye . Kwake Sir Bobby Charlton alikua amekamilisha kile alichokua anakitaka juu ya kijana huyo fundi kutoka Spain , kazi ilikua kwa Herrera kuonyesha kile ambacho viungozi hawakujua nyuma ya pazia ... Mechi yake ya kwanza ilikua dhidi ya La galaxy kwenye mchezo wa kirafiki nchini marekani , na aliweza kutoa assist tatu kwenye ushindi wa mabao 7-1, ilikua mnamo 26 July 2014. Pamoja na uwezo aliokua akioonyesha akiwa kama kiungo mshambulaji lakini bado Van gaal hakumuamini sana, na matoeko yake alikua akianzia bench. Mpaka Van gaal anaondoka herera hakua na uhakika wa namba maalumu kwnye kikosi cha united . Akaja Josse Mourinho ,Herrera akafufuka tena na kuwa mchezaji muhimu katika kikosi ,safari hii sio tena Harrera yule mwenye sura ya Bilbao ,mpikaji wa mabao ,mwenye maalifa . Herrera wa Mourinho alikua kiungo mkabaji yaani mkata umeme .... Japo alicheza namba ambayo hakuizoea sana, lakini unaona Herrera alijitolea,kijituma kwasababu ya timu .. Alicheza kwa kiwango kile kile karibu msimu mzima ,alikua anakaba ,aliilinda vyema safu ya ulinzi ,ananzisha mashambulizi na alikua anatoa msaada wa kufunga ,huyu ndiye Herrera mchezaji bora wa mwaka ndani ya klabu ya Manchester united msimu ulioisha . Lakini msimu huu hana uhakika wa namba . karibu michezo yote ambayo Herrera amecheza msimu huu ,kacheza vizuri mno kwa kiwango bora ,lakini bado Mourinho hampangi . Pengo la Herrera lipo na linaonekana kwa uwazi , lakini hapangwi .. jiulize kwanini ..?! Manchester united ya sasa haina kiungo halisi mkabaji, yule matic sio kiungo mkabaji japo anajitahidi ,hata Herrera sio kiungo halisi mlinzi, lakini nafasi hiyo anaiweza zaidi kiliko Matic . Lakini kwanini Mourinho anaendelea kumuamini Matic na ilihali Matic akicheza pacha na Herrera huwa yupo huru sana... Herrera bado ni mchezaji muhimu kwa kikosi hichi chini ya Mourinho ,lakini Mourinho inaoenekana ameshindwa kumuamini na matokeo yake anaozea kwnye mbao za Old Trafford. Herrera ameshindwa kupewa heshima yake ile ambayo Sir Bobby Charlton alikua halali akimuwaza . kuna kitu Manchester united imekipoteza kwa Herrera ,ni kama imedhurumu kipaji chake . Lakini Herrera hajali hilo ,uso wake unaonyesha hivyo ,Moyoni anaipenda sana Manchester united ,lakini ni kama makocha wameshindwa kumuamini . Muda mwingine inauma sana,kuona mchezji mwnye kipaji kama Herrera hana uhakika wa namba kwenye eneo la kiungo kwa Manchester hii ..!!!! Inashangaza sana . Kipaji alichokina Legend, sasa kinaozea kwenye mbao za Old Trafford . Pole sana Ander Herrera.