Narudia Tena na Tena Ikibidi tunzeni haya maneno ,
Manchester United chini ya Mourinho haiwezi kufika popote, Mbinu za mourinho zipo outdated.
malizia huko chini kwenye maelezo yake yeye,bodi na mkurugenzi.
hapo nshamaliza labda uhamie city ukamuunge mkono pep
" Siondoki United " - Mourinho
Jose Mourinho amesema kwamba amejikita Manchester United na anataka kubaki Man United kwa zaidi ya mkataba wake wa sasa.
Mourinho kwa sasa yupo katikati ya mkataba wake wa miaka mitatu ambao aliusaini mwaka 2016 kuchukua nafasi ya Louis van Gaal.
Mazungumzo kuhusu kuongeza mkataba yalianza mwezi Oktoba baina ya wakala wa Mourinho , Jorge Mendes na Man United.
Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, Mourinho alizielezea taarifa za kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu huu kuwa ni ' Takataka ' na ni juu ya Man United kuamua kubaki kwake Old Trafford.
" Kama unataka kuniuliza mimi moja kwa moja kama najiona kuwa Man United msimu ujao , basi nasema kwamba najiona kuwepo hapa msimu ujao ."
" Kama nilivyosema nilipowasili hapa , nitaondoka pindi klabu itakapotaka niondoke, kwasababu sina nia ya kuondoka hata kidogo."
" Lengo langu ni kubaki na kufanya kazi na kuboresha na kuirejesha klabu pale inapostahili."
" Na nataka kubaki, sioni sababu yoyote ya kutotaka kubaki. Bado nina mkataba. Na ndio kwanza nipo katikati ya mkataba wangu. Sipo katika miezi michache ya mwisho."
" Matamanio yangu ni kubaki mpaka pale Wamiliki na Bodi wakiwa na furaha na kazi yangu."
" Nipo katikati ya mkataba wangu. Kama nitasaini mkataba mpya bila shaka hiyo inategemea na klabu, lakini kujikita kwangu ndani ya klabu ni asilimia mia na nataka kubaki."
Pindi alipoulizwa kama anataka kubaki United zaidi ya mkataba wake wa sasa, Mourino alisema," Ndio najiona kubaki hapa zaidi."
" Ni swala la Wamiliki, Bodi ya Wakurugenzi na Ndugu Woodward wana furaha na mchango wangu na wanataka mimi kubaki zaidi ya mkataba wangu wa sasa . Lakini ndio nataka kubaki."