Nakumbuka kipindi cha David Moyes hawa hawakufungua mdomo mpaka Moyes anatimuliwa. Lakini alivyokuja Van Gaala walianza kumponda sana na Mourinho na yeye wanamponda, ukiangalia wachezaji wetu wanaopondwa ni wawili au watatu.
Pogba, Lukaku na Martial, sijawasikia Rashford akipondwa kwa kukosa nafasi za wazi.
Nakumbuka 2012 Gary Neville aliletewa noma na Babu baada ya kumpiga mdomo David De Gea, pia Roy Keane alitimuliwa na Babu baada ya kuwapiga mdomo wachezaji wenzake.
Man United haina tabia ya kumvumilia yeyote anaepiga wachezaji wake mdomo, timu iko kulinda wachezaji wake.
Halafu hawa jamaa wana hasira sana baada ya Ed Woodward kuwakataa kwenye timu, Scholes alitaka kuwa kocha wa under 23’s lakini alikataliwa, Giggs alitaka kuwa kocha mkuu lakini alikataliwa tokea hapo ni mara chache sana anaiongelea Man United vizuri.