Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Jamani Mimi @King_Ngwaba Niambieni Ninaishi Sayari Gani???
Manake Katika Sayari ya Earth (Dunia) Sitegemei Kama Naweza Sikia Vituko Kama Hivi!!!

ههههههههههههههه
Mkuu, si ya kushangaa hayo... Mashabiki wa arsenal si unawajua kwa kujipa mataji na ushindi ulokuwa si wao. Hao jamaa subiri next season ianze, watakwambia walikuwa kwenye champions league 2017-2018 season 😀
 
Jose Mourinho amemshutumu nyota wa zamani wa Manchester United Paul Scholes baada yake kumkosoa mara kwa mara kiungo wa kati kutoka Ufaransa Paul Pogba.
Akizungumza baada ya sare ya 0-0 kati ya klabu hiyo na Southampton Jumamosi, Scholes alisema: "Haonekani kama mchezaji ambaye atakusaidia kushinda mechi - mchezaji kama huyo ndiye unafaa kutoa £90m mfukoni kwa sababu yake."
Baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Everton Jumatatu, Mourinho alisema: "Jambo pekee analofanya Scholes ni kukosoa tu.
"Scholes atakumbukwa kwenye historia kama mchezaji stadi. Si kama mchambuzi mahiri wa soka.

Tamko la Scholes mwishoni mwa wiki alilitoa baada ya United kutoka sare mechi ya tatu mtawalia.
Mchezaji huyo wa zamani wa England ambaye sasa ana miaka 43 amekuwa akifanya kazi kama mchambuzi katika runinga ya BT Sport na alikosoa mtazamo wa Pogba na kudokeza kwamba huenda pia hayuko sawa kimwili kucheza.

'Anazurura' tu wakati wa mechi," alisema Scholes.
"Pogba haonekani kuwa sawa kucheza, nashangaa iwapo anafanya mazoezi vyema.
"Hakuna yeyote England anafaa kuwa akifika karibu naye, lakini anatakiwa kufanya majukumu ambayo hapendezwi nayo.
"Inabidi useme kwamba meneja anafaa kulaumiwa kwa hilo."

Pogba, 24, alicheza zaidi safu ya mashambulizi dhidi ya Everton zaidi ya alivyocheza dhidi ya Southampton, na alisaidia mabao yaliyofungwa na Anthony Martial na Jesse Lingard waliposhinda 2-0.
Mourinho alisema: "Sifikiri yeye (Shcoles) huwa anatoa maoni. Yeye hukosoa - ambalo ni jambo tofauti.
"Si kila mtu anaweza kuwa stadi kama alivyokuwa. Alipokuwa mchezaji alikuwa hodari ajabu, lakini haina maana kwamba sote twafaa kuwa kama yeye.
"Wakati mwingine Pogba hucheza vyema, wakati mwingine hucheza vyema na wakati mwingine huwa hachezi vyema. Pogba hutia bidii kila wakati.

Si kosa lake Paul kwamba ameunda pesa nyingi zaidi ya Paul Scholes. Si kosa la Paul Pogba, ni vile tu soka ilivyo."
Mourinho aliongeza pia kwamba iwapo Scholes atakuwa meneja siku moja, "ningependa sana awe na ufanisi angalau 25% ya ufanisi wangu."
 
Bado kuna watu watakwambia kuwa hatuna wachezaji ambao watawezesha united kucheza mpira mzuri..jana naamini mmeona tulivokuwa tunacheza kama timu inayojielewa..tunaitaji wachezaji wachache tu kusajiliwa ili kuboresha kikosi chetu..na wachache kuondoka kwenda kutafuta nafasi sehemu nyingine(blind,darmian,zlatan na mikhitaryan)

Lukaku ndo anayefanya tucheze mpira kama watu tusiokuwa na uwezo kwa kuwa akiwepo uwanjani yeye ndo anakuwa target,kross za ajabu ajabu na pia hata akipata mpira akiwa katikati first touch zake ni za ovyo ovyo.

We must try martial upfront,kwa sababu timu inacheza kwa kutokuwa na focal point,kitu kinachofanya kutokuzoeleka wakati wa kuattack kwani wale front three wanakuwa wanainterchange..naamini mliona mipira ilivokuwa inatembea vizuri,no hoofball anymore,na mipira ya juu na mirefu kulikuwa hamna kabisa.

Naamini ili pogba awe katika ubora wake ni lazima awe na jukumu kubwa tu la kuattack,na solution ni kucheza na three midfielders..kama kuna holding midfielder mwingine mzuri sokoni inabidi asajiliwe acheze na matic huku pogba akiwa free kufanya yake akitoke left side..hata gemu za mwanzo ambazo pogba alifanya vizuri,ilikuwa ni baada ya fellaini kuwa ameingia akicheza na matic..kiungo kama granit xhaka wa arsenal ni mzuri sana eneo hili..

Lingard is our best attacking player so far..ana football brain.

Nitashangaa sana mourinho akirudi kwenye fomesheni yake ya 4-2-3-1 ili aweze kumaccomodate lukaku..Mi naona ni vizuri tucheze 4-3-3..baadhi ya gemu lukaku aanzie benchi huku martial akianza upfront..mtu gani hawekwi benchi bana..

De gea
Lindelof rojo jones shaw
Herrera matic pogba
Mata martial Lingard
Hii ni kwa kipindi hiki cha injuries..

De gea
Valencia BaillyJonesShaw
Herrera Matic Pogba
Mata RL/Martial lingard
Hii ni tukiwa hatuna injuries..
Acha roho mbaya na Lukaku, game 10 za mwanzo mbona hukuongea hizo pumba
 
Acha roho mbaya na Lukaku, game 10 za mwanzo mbona hukuongea hizo pumba
Plastic fan huyo achana nae mimi huwa naamini kama Pogboom akicheza kama free prayer kwenye DM wakikaa Matic na Herrera basi Lukaku atafunga sana. Lukaku mfumo ulikua unamtesa sana muda mwingine inapgwa counter attack anakimbia kutafuta position akifika anakua hoi bin taabani lakini anajituma hachoki kabisa mbona Lacazett hajafunga kitambo na wale mashabiki wenye presha hawasemi (aseno fans) kazi kuja huku kumkaba koo Lukaku. Kama kweli wewe mshabiki wa manchester united na unaangalia games tulizocheza msimu huu pasi na shaka utakubaliana nami kwamba Lukaku ana umuhimu wake kabisa. Huku Lingardinho, hapa Pogba, pale Mata, kati herment (her+mat), nguzo tatu Jini De gea huku Shaw kwenye ubora wake na Rojo akisawazisha mambo kwanini mambo yasiwe sawia tuwe na subira kama mashabiki wa liverpool sie tumekosa Epl miaka kadhaa ina makwapa mengine tunayo wenzetu hata Vikombe vya mbuzi vya kuhesabu.
#GGMU#
 
Acha mambo ya kishamba mkuu..Plastic fan!!!...kwahiyo unajiona wewe ndo shabiki bora wa united kuliko wengine,mi nimefanya analysis yangu kwa mawazo yangu,mambo ya kuniita plastic fan ni ya kishamba...
 
ukitoa mechi kubwa, mechi ndogo lukaku zote anacheza vizuri, hadi ambazo hatujashinda. na zile mechi ngumu tunazocheza na timu ngumu ndogo lukaku ndio anatuokoa, refer mechi ya southampton, west brom, etc kigoli kimoja cha kichwa mechi inaisha.

kuna watu walifurahi lukaku kuumia, ila naamini mechi ya southampton marudio angekuepo lukaku matokeo yasingekuwa vile, kifupi mechi ndogo lukaku akiwa ndani kwenye ligi hatutoki kapa bila kufunga goli, kwa mara ya kwanza tumetoka kapa alivyoumia yeye.

hata jana tumeshinda ila unaona kabisa pengo lake, hakuna mishe mishe ndani ya box, ikabidi man U watumie Plan B kupiga mashuti ya mbali, zaidi ya nusu ya attempts za jana ni nje ya box, na magoli yote mawili yametoka huko.
 
Sawa kiongozi ubarikiwe sana
 
Kweli kabisa Lukaku anapiga sana kazi pale mbele
 
Lile jukwaa lina stress sana unaweza jikuta unatuka mtu ukaishia kulamba ban! nimepigwa ban karibu mara tatu na zote nimezitolea huko!
tatizo kule watu wamejitoa ufahamu hawajali uhalisia wa mambo,vitu au matukio ni ushabiki wa kijinga uliopitiliza hadi inakera. Ni mahaba niue baina ya ccm na chadema. Ni kichefuchefu kule MABWANA JUHA wengi sana mule kila mtu mjuaji.
 
Back
Top Bottom