Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

vibaya mno tumekuwa na timu ya uoga sana

Mou ni muongeaji sana lakini maneno yake sio dawa uwanjani

bora apatiwe giggs hii timu tuone enzi za SAF zikijirudia napenda mpira wa kushambulia na mpira wa kulazimisha matokeo positive
kiukweli mou amepambana juu ya hili lakini ameshindwa
Giggs Apewe mkoba tu
Kwa kweli Mou anatudhalilisha sana
 
Habari zenu wadau wa Soka

Hivi Manchester united kutolewa kwenye mashindano kombe la ligi na timu ndogo namna hii tena wao Manchester wakiwa kama mabingwa wa tetezi. Inamaanisha Manchester imeshuka kiwango, morinyo ameishiwa mbinu au Manchester wanaikimbia Chelsea?



Kwa hiyo hapo madrid alikuwa anataka kumkimbia barcelona?
Screenshot_2017-12-21-15-51-21.png
 
Nimegundua kwa nn msimu uliopita zile suluhu zilitokana na nini huyu ibra ni tatizo kubwa mno waliokuwa wakimponda Lukaku watie akilini hawez hata kuwaangushia mipira wakina martial na rashford lakin lukaku unaona anavyorahisisha maisha ya lingard,rashford na martial.
ktk usajili tuliofanikiwa ni wa Lukaku hakika nawaambia.
Nashangaa timu kama MUFC imekuja kuwa ya wazee kuja kumalizia soka lao..
 
Tetesi
Manchester United wanamsaka kwa udi na uvumba kinda wa miaka 19 wa Borussia Dortmundand na Marekani Christian Pulisic. (Daily Mail)
 
Tetesi
Manchester United wanamsaka kwa udi na uvumba kinda wa miaka 19 wa Borussia Dortmundand na Marekani Christian Pulisic. (Daily Mail)
Hivi scouting ya Manchester iliyokuwa chini ya ndugu yake Sir Alex Ferguson makali yake yamepotelea wapi??


Tunahusishwa na wachezaji Wa hivyo hovyo.
 
ManUTD are losing from city to city, from man city to Bristol City and now they are heading to Leicester city

Kindly guess the scoreline
 
" Niliwashauri wawasajili Mbappe na G.Jesus " - Giggs.

Winga wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs amesema kwamba aliiambia klabu kuwasajili Kylian Mbappe na Gabriel Jesus mwaka mmoja kabla ya kuibuka kwenye ramani ya ulimwengu wa soka.

Giggs ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Manchester United chini ya Utawala wa Louis van Gaal kuanzia 2014-2016 amekiri kwamba alitofautiana na mdachi huyo kuhusu Sera ya usajili ndani ya klabu.

Giggs amekiri kwamba aliwaskauti wachezaji hao wawili Mbappe na Jesus chini ya utawala wa Van Gaal na kuishauri klabu kuwasajili vijana hao kabla hawajawa nyota wakubwa Duniani.

Mbappe,19 alijiunga na PSG kwa mkopo kutoka Monaco mwezi Agosti kukiwa na kipengele cha kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu kwa dau la Pauni Milioni 166 majira yajayo ya kiangazi baada ya kuonyesha kiwango bora sana msimu uliopita.

Huku , Jesus mwenye umri wa miaka 20 tayari ameshafunga magoli 15 kwa mahasimu wa United, Manchester City tangu aliphamia hapo mwezi januari kutoka Palmeiras kwa dau la Pauni Milioni 27.

" Nilimuangalia Gabriel Jesus akicheza miaka mitatu iliyopita . Nilimuangalia Mbappe kwa mwaka mzima . Nilikuwa nawaangalia nikiwa na skauti na ilikuwa wazi kabisa kuhusu vipaji vyao." Amesema Giggs kwenye mahojiano na The Times.

" Ilikuwa kama kusema, ' nenda wachukueni'. Ingeweza kuwa Pauni Milioni 5 au zaidi kidogo tu , wanunue halafu warudisheni kwa mkopo - na hapo ndio idara ya usajili ilitakuwa kufanya kazi nzuri."

United walifanya usajili mkubwa pindi Van Gaal alipokuwa madarakani , usajili wa wachezaji Angel Di Maria, Memphis Depay, Anthony Martial, Morgan Schneiderlin na Radamel Falcao.

Licha ya usajili mkubwa wa klabu , Giggs alihisi kwamba wachezaji waliosajili walikuwa hawana utambulisho wa mchezaji wa Man United - sababu ambayo ilileta kombe moja ndani ya miaka miwili ya utawala wa Van Gaal.

" Najua mchezaji wa Manchester United anavyoonekana ." Ameongeza Giggs.

" Kumekuwa na wachezaji wengi walioingia ndani ya United ambao hawana sifa ya kuwa mchezaji wa Man United na pia wachezaji ambao walikuwa na sifa ya Man United kuruhusiwa kuondoka."

" Naongea kuhusu Rafael [Da Silva], Danny [Welbeck], na Jonny Evans wachezaji ambao wana damu ya Man United , wanaocheza mpaka filimbi ya mwisho ."

" Ilikuwa ngumu kwasababu Louis alikuwa na mitazamo yake mwenyewe na unalazimika kuheshimu hilo lakini ni kweli
tuliwahi kuwa na mahojiano kuhusu baadhi ya wachezaji. Alinielewa kwasababu niliwahi kucheza na hao wachezaji , lakini hawakuwa chaguo lake."

" Baadhi yao kama Welbeck alikuwa anataka kucheza mara kwa mara , Jonny alikuwa na majeraha kadhaa muda ule , kwahiyo ulikuwa unaweza kuelewa kwa hilo - lakini idara ya usajili chini ya Van Gaal haikufanya kazi nzuri sana kwa daraja la sifa ya United."
 
Back
Top Bottom