Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

" Niliwashauri wawasajili Mbappe na G.Jesus " - Giggs.

Winga wa zamani wa Manchester United Ryan Giggs amesema kwamba aliiambia klabu kuwasajili Kylian Mbappe na Gabriel Jesus mwaka mmoja kabla ya kuibuka kwenye ramani ya ulimwengu wa soka.

Giggs ambaye aliwahi kuwa kocha msaidizi wa Manchester United chini ya Utawala wa Louis van Gaal kuanzia 2014-2016 amekiri kwamba alitofautiana na mdachi huyo kuhusu Sera ya usajili ndani ya klabu.

Giggs amekiri kwamba aliwaskauti wachezaji hao wawili Mbappe na Jesus chini ya utawala wa Van Gaal na kuishauri klabu kuwasajili vijana hao kabla hawajawa nyota wakubwa Duniani.

Mbappe,19 alijiunga na PSG kwa mkopo kutoka Monaco mwezi Agosti kukiwa na kipengele cha kufanya uhamisho huo kuwa wa kudumu kwa dau la Pauni Milioni 166 majira yajayo ya kiangazi baada ya kuonyesha kiwango bora sana msimu uliopita.

Huku , Jesus mwenye umri wa miaka 20 tayari ameshafunga magoli 15 kwa mahasimu wa United, Manchester City tangu aliphamia hapo mwezi januari kutoka Palmeiras kwa dau la Pauni Milioni 27.

" Nilimuangalia Gabriel Jesus akicheza miaka mitatu iliyopita . Nilimuangalia Mbappe kwa mwaka mzima . Nilikuwa nawaangalia nikiwa na skauti na ilikuwa wazi kabisa kuhusu vipaji vyao." Amesema Giggs kwenye mahojiano na The Times.

" Ilikuwa kama kusema, ' nenda wachukueni'. Ingeweza kuwa Pauni Milioni 5 au zaidi kidogo tu , wanunue halafu warudisheni kwa mkopo - na hapo ndio idara ya usajili ilitakuwa kufanya kazi nzuri."

United walifanya usajili mkubwa pindi Van Gaal alipokuwa madarakani , usajili wa wachezaji Angel Di Maria, Memphis Depay, Anthony Martial, Morgan Schneiderlin na Radamel Falcao.

Licha ya usajili mkubwa wa klabu , Giggs alihisi kwamba wachezaji waliosajili walikuwa hawana utambulisho wa mchezaji wa Man United - sababu ambayo ilileta kombe moja ndani ya miaka miwili ya utawala wa Van Gaal.

" Najua mchezaji wa Manchester United anavyoonekana ." Ameongeza Giggs.

" Kumekuwa na wachezaji wengi walioingia ndani ya United ambao hawana sifa ya kuwa mchezaji wa Man United na pia wachezaji ambao walikuwa na sifa ya Man United kuruhusiwa kuondoka."

" Naongea kuhusu Rafael [Da Silva], Danny [Welbeck], na Jonny Evans wachezaji ambao wana damu ya Man United , wanaocheza mpaka filimbi ya mwisho ."

" Ilikuwa ngumu kwasababu Louis alikuwa na mitazamo yake mwenyewe na unalazimika kuheshimu hilo lakini ni kweli
tuliwahi kuwa na mahojiano kuhusu baadhi ya wachezaji. Alinielewa kwasababu niliwahi kucheza na hao wachezaji , lakini hawakuwa chaguo lake."

" Baadhi yao kama Welbeck alikuwa anataka kucheza mara kwa mara , Jonny alikuwa na majeraha kadhaa muda ule , kwahiyo ulikuwa unaweza kuelewa kwa hilo - lakini idara ya usajili chini ya Van Gaal haikufanya kazi nzuri sana kwa daraja la sifa ya United."
mbape angeenda man u kiwango chake kingeshuka
 
Nashangaa timu kama MUFC imekuja kuwa ya wazee kuja kumalizia soka lao..
Bila shaka utakuwa ulikuja MUFC na Moyes kama sio LVG, maana kama ungalikuwa ulikuwapo enzi za Fergie sidhani kama ungeona kitu cha ajabu. Refer Michael Owen, Larsson, RVP na wengine wengi tu.
 
Bila shaka utakuwa ulikuja MUFC na Moyes kama sio LVG, maana kama ungalikuwa ulikuwapo enzi za Fergie sidhani kama ungeona kitu cha ajabu. Refer Michael Owen, Larsson, RVP na wengine wengi tu.
Mara nyingi huwa nawashangaa pia mashabiki wa aina yako wanaojiona walizaliwa na timu wanazozishabikia..

Mkuu, tufanye nilianza kuishabikia UNITED juzi baada ya ujio wa Mou!

Umemzungumzia Owen(30) Larsson(35) ambaye hata sijui aliifungia united goli ngapi kwa muda wake mfupi alioichezea..

Ajabu la mwisho ni kuniwekea RVP katika hiyo list yako, hivi RVP wakati anatua OT akiwa na 29yrs alikuwa amekwisha? Hivi RVP ndo unataka kusema alikuwa sawa na Ibra huyu anacheza hataki hata kuanguka? Kujituma sifuri kabisa..

Halafu nikizungumzia "kumalizia soka" namaanisha hakuna kitu tena, ni tia maji tia maji!
 
RVP kacheza misimu mingapi united kabla ya kuonekana gharasa na babu hatimaye kuuzwa?
Ibra hadi sasa ana misimu mingapi united???
 
RVP kacheza misimu mingapi united kabla ya kuonekana gharasa na babu hatimaye kuuzwa?
Ibra hadi sasa ana misimu mingapi united???
Kwa hiki ulichoandika hapa hata sijui kama ulielewa mantiki ya mchango wangu..

Unaposema "kabla ya kuonekana" unamaanisha alikuja akiwa moto wa kuotea mbali, tofauti kabisa na alivyokuja Ibra ambaye kimsingi hadi sasa kinachomuweka pale OT ni kocha kupenda miili mikubwa lakini kuzungumzia kiwango kwa sasa ni sifuri na wala huwezi kumtegemea kama mshambuliaji wa akiba!
 
Ingawa ni ngumu kukuelewa, lakini nakuelewa hivo hivo. Hiki ulichoandika saa hizi mantiki yake ni tofauti na ulichoandika mwanzo.

Nashangaa timu kama MUFC imekuja kuwa ya wazee kuja kumalizia soka lao..

Nafikiri hiki ndicho kilicholeta mjadala, sio hoja yako mpya hapo juu.
 
Ingawa ni ngumu kukuelewa, lakini nakuelewa hivo hivo. Hiki ulichoandika saa hizi mantiki yake ni tofauti na ulichoandika mwanzo.

Nafikiri hiki ndicho kilicholeta mjadala, sio hoja yako mpya hapo juu.
Hapo nafikiri umenielewa..

Tunaambiwa kwamba wakati Ibra anapanga kwenda MUFC Mou alimwambia kama anaenda United "kumalizia soka lake" asiende, ila kama anaenda kupambana ni sahihi..

Sasa sijui wewe "kumalizia soka" umeelewa vipi.
 
IMG_20171223_214645.jpeg
 
Hapo nafikiri umenielewa..

Tunaambiwa kwamba wakati Ibra anapanga kwenda MUFC Mou alimwambia kama anaenda United "kumalizia soka lake" asiende, ila kama anaenda kupambana ni sahihi..

Sasa sijui wewe "kumalizia soka" umeelewa vipi.

So kumbe Ibra hakuja United kumalizia soka lake, ila kupambana. Sasa why ulipost hiki kitu???
Nashangaa timu kama MUFC imekuja kuwa ya wazee kuja kumalizia soka lao..

Mkuu hueleweki, ila najitahidi kukuelewa ili nikueleweshe, tatizo zaidi ni kuwa u mbishi. Mambo kama haya yapo katika soka, kuna wanakuja kumalizia carreer zao (Hawa mara nyingi huwa ni kwasababu kama sio kibiashara basi ni influence anayoweza kui-induce kwa younger ones) na wapo wale wanaokuja kuanza carrier.
 
So kumbe Ibra hakuja United kumalizia soka lake, ila kupambana. Sasa why ulipost hiki kitu???
Kama wewe unaona Ibra anapambana basi kuna tatizo pahala..

Mkuu hueleweki, ila najitahidi kukuelewa ili nikueleweshe, tatizo zaidi ni kuwa u mbishi. Mambo kama haya yapo katika soka, kuna wanakuja kumalizia carreer zao (Hawa mara nyingi huwa ni kwasababu kama sio kibiashara basi ni influence anayoweza kui-induce kwa younger ones) na wapo wale wanaokuja kuanza carrier.
Ila sio kwa Ibra kuendelea kubaki pale,ilibidi awe na ule msimu mmoja tu aondoke.. ndio maana sijaelewa hadi leo ni kwanini Mou alimtoa Rooney kama anaendelea kukomaa na Ibra!
 
Back
Top Bottom