Mkuu ukisema Mata hauwezi mziki wa wa kucheza uwanja mzima utakuwa umeamua kudanganya tu au umeamua tu kusema hivyo kutokana na kwamba tunaongoza bao tatu mpaka sasa...
Ila mimi binafsi uniambie Lingard amtangulie Mata kwasababu yoyote ile naona wazi kwamba unanidanganya (ni mtizamo wangu)
Ukiangalia sana kwa mchezo wa leo kiukweli unakuta kwa namna fulani bahati imecheza kwa nafasi kubwa kulinganisha na ufundi na mipango ya timu. Angalia kuanzia goli la kwanza mpaka la tatu. Hapo mwanzo uliongea kitu cha msingi sana kwamba Watford wanacheza mchezo wa kushambulia hivyo kutuwia rahisi sisi kufanya mashambulizi ya kushitukiza hii ni kwa Magoli yote matatu ukijumuisha na goli la pili ambalo limetokana na Pogba kukokota toka katikati ya uwanja mpaka mpaka karibu na box la Watford alipowekwa chini...
Hii ndiomaana nasema kwa sehemu kubwa mechi hii imechezwa na bahati kwa upande wetu ukilimganisha na mipango na ufundi wa timu.
Yote kwa yote ushindi ni muhimu kwetu