Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

nimebahatika kuangalia mechi zote mbili tulizocheza nchini marekani ila ninashangazwa na suala la mourinho kumtumia fundi andreas perreira kama ni deep play maker,kiukweli bado nimebaki najiuliiza masuali mengi sana kuhusiana na mustakabali wa kijana huyu
DFC0g9sXkAEVqp2.jpg

  1. je ina maana jose mourinho anataka kutuonesha sisi mashabiki na wapenzi wa manchester united ya kwamba perreira ndio mrithi wa michael carrick?
  2. au anataka kutuonyesha ya kwamba hizi kelele zetu tunazopiga juu ya kutaka amsajili nainggolan ambaye ni kiungo wa AS ROMA kwake yeye si kitu na anamuona andreas perreira anaweza kuwa ni bora zaidi ya nainggolan?
  3. au ameamua kuachana na mpango wa kumsajili kiungo wa ulinzi kama matic na dyer kutokana na soko la usajili kuwa ni gumu sana?
  4. au ni kwa sababu itakuwa ni vigumu kwa perreira kupata namba kama kiungo mchezeshaji kutokana na kuwa na wachezaji kama pogba, mata, mkhitaryan, lingard, herrera.
  5. au anataka kumfanya awe strong kama alivyomfanya herrera msimu ulopita?
mkuu perreira ni backup ya herrera, uchezaji wao almost unafanana,

kama unamfuatilia mou timu zake akicheza 4-2-3-1 wale wachezaji wawili wanaocheza namba 6 mmoja ni mkabaji na mwengine anaanzisha mashambulizi toka chini.

mfano kikosi chake cha chelsea walichotwaa ubingwa matic na fabregas, wote ni midfield wakabaji maeneo yao wanayokaa ila faby anaanzisha mashambulizi toka chini

hivyo midfield mkabaji anatakiwa aje ili tuweze kuwafungua pogba na herrera wakashambulie, na perreira sasa atakuwa ni kama patner wa kiungo mkabaji ambae anashambulia toka chini.

wapo wachezaji wakubwa kama pirlo, veratti, pep guardiola, alonso, xavi (zamani mwanzo wa uchezaji wake), etc wote hawa walikuwa deep lying playmaker aka regista.
 
Mpe mkeo sababu ya kuendeelea kutabasamu, tunajua amevumilia mengi mpaka kufikia kuitwa mke wako. Unapoalikwa kwenye harusi na kumuona bibi harusi akitabasamu usijekuangalia na kuwaza ukasema yule mwanamke ana furaha.

Hapana wanawake wengi mpaka kufikia ndoa wanakua wamepitia mengi, vipigo, manyanyaso, usaliti na mambo mengi ya ajabu ambayo wameamua kuyavumilia wakiamini kua labda baada ya kuolewa mambo yatabadilika.

Wengi hawacheki na kutasabasamu kwakua wana furaha, hapana wengi hucheka na kutabasmau kwakua wanamatumaini kua labda mwanaume baada ya kumuweka ndani basi atabadilika na kuwa mwanaume wa ndoto yao.

Wanatabasamu lakini wakiwa na mashaka kama ndoa itadumu huku wakiwa na kibarua si tu cha kulinda ndoa zao bali kulinda heshima za familia zao, kwamba watu wasije kusema kuwa ile familia haiolewi kwakua wana tabia flani.

Hembu kama wewe ni mwanaume najua unajua mambo ambayo umemfanyia mkeo kipindi cha uchumba, hembu leo amua na kusema hapana, sitaki mke wangu ushindane na michepuko yangu, nimeshakuoa wewe sitaki uvumilie mateso bali uvumilie shida na tutavumilia pamoja.

Muambie mkeo nakupenda na hata kama hutaweza kusema nisamehe kwa mdomo sema kimoyomoyo( japokuwa ni vyema zaidi ukamwambia live) na muambie nisamehe huko kichwani kwako, badilika na mpe tabasmau la milele, dumisha lile tabasamu ambalo ulimpa siku ya harusi mbele ya ndugu zenu na marafiki zenu.


Credits: Iddi Makengo

Nilifikiri soccer is a fairplay and non racism game, au lile bango la FIFA la No racism ni kwa ajili ya wazungu tu.?
Nilikuwa nakuona mwanamichezo mwenzetu kumbe ni hovyo kabisa we jamaa. Umenibore sana we jamaa.

Nawaomba ndugu zangu wote wapenda michezo uwe mshabiki wa Man utd au timu yoyote ile ila hupendi ubaguzi tumpinge huyu jamaa, tumu=ignore kwa kila atakachopost ili ajue kuwa alichofanya sio kizuri maana lugha aliyotumia sio ya kiuanamichezo.

Mods pia kama mtasoma hapa naombeni huyu jamaa apigwe ban ili ajifunze ustaarabu.
Hajaonyesha uugwana labda mzungu ila tujue mpira unachezwa na binadamu yeyote, tusibaguane sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilifikiri soccer is a fairplay and non racism game, au lile bango la FIFA la No racism ni kwa ajili ya wazungu tu.?
Nilikuwa nakuona mwanamichezo mwenzetu kumbe ni hovyo kabisa we jamaa. Umenibore sana we jamaa.

Nawaomba ndugu zangu wote wapenda michezo uwe mshabiki wa Man utd au timu yoyote ile ila hupendi ubaguzi tumpinge huyu jamaa, tumu=ignore kwa kila atakachopost ili ajue kuwa alichofanya sio kizuri maana lugha aliyotumia sio ya kiuanamichezo.

Mods pia kama mtasoma hapa naombeni huyu jamaa apigwe ban ili ajifunze ustaarabu.
Utoto unamsumbua,akikua ataacha mkuu!
 
Kwa huu ubaguzi uliouonyesha hapa jukwaani haufai kabisa kupewa ushirikiano na mwanamichezo yeyote yule, hata wa kutoka katika timu unayoishabikia..

Wakuu, wadau wa uzi huu na wapenzi wa soka mnaoutembelea uzi huu tukianza na Idimi Rutashubanyuma kisu cha ngariba Nzi Damushin The Bodmas mkurya org. ze-dudu Na wengine ambao sijawamention..

Tumpuuze huyu mbaguzi mpaka atakapokua na kuacha utoto!
Huyo ni wa kum-ignore tu. Mimi yumo kwenye ignore list yangu. Cha ajabu anayemwita chimpanzee hata hamfahamu, na anaweza kuhudumia ukoo wao wote mpaka kiama. Akili za kimaskini na chuki za mafanikio ya Lukaku!
 
Morata huyu huyu kwenye miaka minne kafunga goli 40 tu au mwingine?
Ungekuwa na akili hata ya kuvukia Barabara tuu ungegundua kitu, hizo goli 40 kwa miaka 4 amecheza mechi ngapi??? Na huyu romelu likuku amecheza mechi ngapi kwa hiyo miaka 4????

Pogba wa tz nchi imekushinda!
 
Kwa hiki wanacho kifanya MADRID sio kitu kizuri kabisaa. Sisi tuliwapa CR7 wenyewe wanatunyima MORATA.
Tumeamua kumchukua ROMELU AMBROSI LUKUMBESA BOLINGO LUFUFU. Bila ya kupenda lilikuwa chaguo la Z.
Wallah kuanzia leo tunasema tunahamia BARCELONA.

Asee watu bhana
😛 😛 😛 😛 😛 😛 lukumbesa 😛 😛 😛 😛 😛 😛 😛

Pogba wa tz nchi imekushinda!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI 20.07.2017
Paris Saint-Germain wanajiandaa kuzungumza na Barcelona kuhusu uhamisho wa pauni milioni 196 wa Neymar, 25. (Guardian)
PSG wapo tayari kumpa Neymar pauni milioni 45, za kukubali tu kujiunga nao, na mshahara wa pauni 596,000 kwa wiki (baada ya makato ya kodi) na mkataba wa miaka mitano. (Daily Mail)
Barcelona wanapanga kuzungumza na Monaco kuhusu kumsajili Kylian Mbappe, 18. Barca wanatarajia kupata fedha za kutosha kumsajili Mbappe baada ya kumuuza Neymar, 25. (Daily Mail)
Chelsea wanataka pauni milioni 44 kutoka kwa Atletico Madrid kwa ajili ya Diego Costa, 28, baada ya kukamilisha usajili wa Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid. (Independent)
Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amesema hakuna uhakika thabiti iwapo Diego Costa atakwenda Atletico Madrid. (Mirror)
Chelsea, Tottenham na Manchester United huenda zikaingia katika mapambano ya kumgombania kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. (The Times)
Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, baada ya dau la pauni milioni 66 kukataliwa. (Mirror)
West Ham wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier ‘Chicharito’ Hernandez, 29, kutoka Bayer Leverkusen. (Sky Sports)
Arsenal wamewaambia West Ham kuwa watalazimika kutoa pauni milioni 20 ikiwa wanamtaka kiungo Jack Wilshere, 25. (Daily Star)
Paris Saint-Germain wamemtuma mkurugenzi wao wa michezo kwenda London kujaribu kumshawishi Alexis Sanchez, 28, ambaye pia anasakwa na Manchester City. (Sun)
Everton wamepata matumaini zaidi ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30. (The Telegraph)
Kiungo wa Arsenal Mohamed Elneny amekataa kuhamia Leicester City waliokuwa tayari kutoa pauni milioni 10 kumsajili. (The Sun)
Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Real Madrid Danilo, 26, kwa pauni milioni 26.5. (Guardian)
Manchester city wanakaribia kukamilisha usajili wa beki Benjamin Mendy, 23, kutoka Monaco. (Times)
Manchester United wanahusishwa na kutaka kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain, Marco Verratti, 24, baada ya mchezaji huyo kumfanya Mino Raiola kuwa wakala wake mpya. (Sun)
Manchester United na Chelsea zilitazama uwezekano wa kumsajili Neymar, lakini timu hizo mbili zilikatishwa tamaa na bei ya pauni milioni 196 ya mchezaji huyo, 25, kutoka Brazil. (Independent)
Inter Milan wamewaambia Manchester United lazima wamjumuishe Anthony Martial, 21, katika mkataba wowote utakaohusu uhamisho wa Ivan Perisic, 28. (Independent)
AC Milan wamesema kiungo mshambuliaji wao Suso, 23, anayenyatiwa na Tottenham, hauzwi. (Tuttomercato)
PSG watamuuza kiungo Blaise Matuidi, 30, iwapo dau zuri litatolewa. (L’Equipe)
Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom