Mwanaume: Mpe mkeo tabasamu la milele

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
52,478
70,593
Mpe mkeo sababu ya kuendeelea kutabasamu, tunajua amevumilia mengi mpaka kufikia kuitwa mke wako. Unapoalikwa kwenye harusi na kumuona bibi harusi akitabasamu usijekuangalia na kuwaza ukasema yule mwanamke ana furaha.

Hapana wanawake wengi mpaka kufikia ndoa wanakua wamepitia mengi, vipigo, manyanyaso, usaliti na mambo mengi ya ajabu ambayo wameamua kuyavumilia wakiamini kua labda baada ya kuolewa mambo yatabadilika.

Wengi hawacheki na kutasabasamu kwakua wana furaha, hapana wengi hucheka na kutabasmau kwakua wanamatumaini kua labda mwanaume baada ya kumuweka ndani basi atabadilika na kuwa mwanaume wa ndoto yao.

Wanatabasamu lakini wakiwa na mashaka kama ndoa itadumu huku wakiwa na kibarua si tu cha kulinda ndoa zao bali kulinda heshima za familia zao, kwamba watu wasije kusema kuwa ile familia haiolewi kwakua wana tabia flani.

Hembu kama wewe ni mwanaume najua unajua mambo ambayo umemfanyia mkeo kipindi cha uchumba, hembu leo amua na kusema hapana, sitaki mke wangu ushindane na michepuko yangu, nimeshakuoa wewe sitaki uvumilie mateso bali uvumilie shida na tutavumilia pamoja.

Muambie mkeo nakupenda na hata kama hutaweza kusema nisamehe kwa mdomo sema kimoyomoyo( japokuwa ni vyema zaidi ukamwambia live) na muambie nisamehe huko kichwani kwako, badilika na mpe tabasmau la milele, dumisha lile tabasamu ambalo ulimpa siku ya harusi mbele ya ndugu zenu na marafiki zenu.


Credits: Iddi Makengo
 
Kakaa WiFi yng huwa unampa tabasamu
Ni kweli zamani nilikuwa nampa tabasamu ila sasa hivi angalia hii picha

d16ba9dafc6c3c57f138029445734fa1.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom