Naijua Man Utd haiwezi kurudi level itachukua miaka hata kumi au zaidi. Kwani nyota kusajiliwa ni tatizo. Kama ni biashara hata arsenal wanafanya hawana loss wamejaza pesa tu jiulize nini kinafanyika. Itabaki story tu.
Bro unaongea kama shabiki wa Mpira anayeujuwa mpira au unataka tujaze Sever tu hapa,any way kwa faida yako na wengine acha tuendelee na mjadala na hivi leo ni sabasaba so we're free.
Mafanikio ya Timu Yeyote yanategemea Vitu Vinne, Moja historia au ukubwa wa timu kiasili sifa hii nadhani timu hizi zote mbili zinazo Liverpool ndio wanaongoza kuchukua UEFA champion Zaidi ya Man U lakini wakifatiwa na Man United lakini katika historia Man United ndio mbabe kwa kuchukua makombe pale EPL,mbili uwezo wa kocha kwa misimu Zaidi ya mitatu tulikosa World class kocha,Moyes hakuwa top cocher duniani wakati anasajiliwa kuja kufundisha Man United,uwezo wa wachezaji binafsi,baada ya Ufalme wa Sir Fegurson ambaye aliweza kuwatengeneza wachazaji wa kuwa kuja kuwa World Class top player,aliopondoka waliomfatia walishindwa kuwa na uwezo huu na kufanya kuona vipaji halisi vya wachezaji wetu, na thamani ya timu katika kuvutia Wawekezaji, kulipa na kununua wachezaji wapya Wenye uwezo,Moyes na Van Gaal hakujuwa ukubwa wa Man United hawajuijuwa thamani halisi ya Man United na ndio mana uliona usajili wa kwanza wa Mou na Wenye thamani ni kumchukua Fellain ambaye hakuwa mchezaji Mkubwa Ulaya.
Van Gaal yeye katika utawala wake aliuza wachezaji wengi wazuri kama Chicharito na kutuletea wapaka Poda wake.
Any way tulikuwa ni kipindi cha Mapito na Mabadiliko now timu ipo kwa kocha mwenye kujuwa Vyote hivi na nzuri Zaidi anajuwa Kiu ya Mashabiki wake.
Bodi ya Man United inakiri kuwa ilifanya makosa makubwa sana kukubali timu kuachiwa Moyes na ndio tulipoanza kuyumba,Van gaal ni top class kocha alitusaidia kutengeneza barabara lakini alipishana na Falsafa ya timu.
Sasa Mou ni mtu sahihi pale Man United anaendana na Falsafa ya timu,ni kocha Mkubwa hivyo anahitaji na timu iwe kubwa na ndio mana aliweza fanya usajili wa uhakika na Mkubwa kurudisha hadhi ya Club Yetu.
Asernal wanakosa baadhi ya Sifa hapo kaka,Asernal sio timu kubwa Ulaya ni timu kubwa England so sio vizuri kuifananisha na Man United,Yes wanafanya vizuri sokoni lakini sio timu yenye kulipa wachezaji mishahara mikubwa sio Wenye kutoa pesa ndefu kwenye usajili.
Asernal imesajili nadhani ni wachezaji wawili top class players kwa misimu miwili ya hivi karibuni lakini sio timu kubwa kuifananisha na Man United na ndio mana wanakosa mbinu za kuchukua makombe.
Nimekwambia tumerudi katika ukubwa wetu au Level Yetu, Man United ni Mabingwa wa Uropa Legue,Kombe kubwa la pili bara ni Ulaya sasa hiyo miaka kumi ipi unayosema.
Kutwaa EPL msimu wa 2017/2018 tusubiri sina shaka na hili,mana hata msimu uliopita zile droo zingebadilika tungeongea mengine.