KOCHA wa Manchester United, Alex Ferguson ataomba mbinu za mpinzani wake wa zamani Jose Mourinho kuhusu jinsi ya kuweza kuifunga Barcelona kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuichakaza Schalke 04.
Ushindi wa jumla wa mabao 6-1, Jumatano usiku unaifanya United kucheza fainali ya tatu ya mashindano hayo mkubwa ya Ulaya katika kipindi cha miaka minne na Ferguson hataki kubweteka baada ya kuteua timu dhaifu dhidi ya Wajerumani na kupata ushindi wa kishindo.
United itakuwa na kibarua mbele ya Barca kwenye Uwanaj wa Wembley hapo Mei 28 wakirudia fainali ya 2009 ambayo vigogo hao wa Hispania walishinda 2-0.
Japokuwa Ferguson hakuonyesha kuficha kwamba anakaribosha ushauri kutoka kwa kocha wa Real Madrid, Mourinho ambaye timu yake iliwafunga vijana hao wa Catalans kwenye Kombe la Mfamle.
Tunazungumza mengi. Wiki iliyopita tu tuliwasiliana, Ferguson aliwaambia wanahabari wakati walipomuuliza kuhusu Mourinho, ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Mscotland huyo alipokuwa akifundisha Chelsea.
Tunatejitegemea wenye kuhusu ufahamu wetu juu ya Barcelona, si kama timu ambayo hatujawahi kukutanayo. Lakini wakati wote nimekuwa nikipokea taarifa mbalimbali kutoka kwa Mourinho kwa sababu amekuwa akinisaidia wakati wote.
Mourinho na Real walicheza na Barca kwenye nusu fainali na kuondolewa Jumanne, lakini waliweza kuonyesha soka nzuri katika mechi za ligi za ndani ikiwa na kuwafunga mchezo moja.
Sifikiri kwamba tutaenda pale tukiwa hatujiamini... Tunatakiwa kutumia uwezo wetu, alisema Ferguson.
Kazi yetu ni kutafuta mbinu sahihi ya wakati tutakapocheza nao.
Ferguson amekuwa wa kwanza na mtu wa pili kuongoza timu kucheza kwenye fainali sita za Ulaya ya kwanza akiwa na Aberdeen na sasa ni mara ya tano akiwa na United kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa. Mtaliano Giovanni Trapattoni ndiye mtu pekee aliyeweka rekodi ya kuziongoza timu zake saba kucheza fainali za michuano hiyo.
Huku Ferguson akikitumia kikosi cha pili kwenye mchezo wake dhidi ya Schalke, kwa kuwapanga wachezaji tisa tofauti na waliocheza mchezo wa kwanza bado anasuka na jinsi ya kuzuia mchezo wa pasi nyingi wa Barca.
Tulienda kwenye fainali ya 2009 tukipewa nafasi kubwa ya kuwa mabingwa, alisema Ferguson. Tukiwa na kikosi kilichokuwa na uzoefu, lakini waliweza kutuyumbisha.Uzoefu unaonyesha kwamba timu iliyokuwa kwenye kiwango kama cha kwetu katika mechi hizi za Ulaya ndiyo inayokuwa na nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye fainalil.