Nakubaliana na wewe unataka kusema enzi za Kenyon na David Gill waliweza kuvunja record kuipita Madrid !!!!!?? ...
Sir Alex furguson na CE's wake wote Tangu mwaka 1986 transfer zao zote zilijikita kwenye tecnical demand kuliko marketing demand.... Japo Kuna Vipindi alimwaga hela ila hiyo hela ilirudi kwa mafaniko tulioyaona uwanjani....
1. Wayne Rooney alivunja record ya kusajiliwa kwa fedha nyingi akiwa na umri mdogo... Tunaona mafanikio yake uwanjani ... Amecheza fainali tatu za uefa na moja tukabeba ndoo.. Najua unaukumbuka usiku wa Moscow vs Chelsea ....
2. Dimitry Berbertov alisajiliwa kwa hela ndefu akitokea Tottenham .. Nina imani unajua vikombe vingapi ametuwezesha kubeba..
3. Rio Ferdinand alisajiliwa kwa hela ndefu na kuwa beki ghali duniani kwa muda ule.. Hakuna shabiki wa utd anaejua mchango wa huyu MTU pale utd... Kacheza fainali tatu za uefa akipacha na Komeo Nemanja Vidic...
Hii ni mifano michache ya transfer za utd enzi za David Gill zikivyokuwa zimejikita kwenye Technical demands kuliko market demands ambapo wachezaji wanaosajiliwa na CEO wetu mpya wanakuja kuiwezesha Manchester utd kung'aa zaidi sokoni kwa kuuza jezi na bidhaa zingine za timu...
Woodward sioni kama Nafasi ya kuwa CEO inamfaa. Jamaa ni mzuri sana kwenye soko ... Ila coordination yake na kocha kuleta vyombo uwanjani sijaiona..
We usituzingue. Upo Sub Saharan Africa tena Third World Country ambayo hata haifahamiki kwahiyo huna haki ya kujudge uCEO wa Ed wakati waliomchagua wanafanya nae kazi kila kukicha na wanajua uwezo wake.
Kuwa na impact kwenye transfer market ni jambo la muhimu kwa timu kubwa kama Manchester United. Kuvunja rekodi sio lazima iwe Madrid au Bayern.
Technical demand ipi unaiongelea? Toka wakati wa SAF timu ilikuwa na tatizo la midfield, makocha wote waliofuata baada ya SAF bado hilo eneo liliwasumbua.
Morinho amekuja ameanza kuleta uhai kwenye timu kuanzia beki hadi midfield. Tatizo la ushambuliaji limejitokeza msimu huu pamoja na kumleta Zlatan still tatizo lipo na ndo kazi ya kocha kumwambia Ed anamtaka mchezaji yupi kuziba hilo pengo.
Pobga amekuja ndo kwanza amemaliza msimu wa kwanza, unamlinganisha na kina Rio, Rooney, Berbatov waliokaa na kuonesha matokeo baada ya misimu mitatu na kuendelea.
Management, Board na Benchi la Manchester sio wajinga kutoa hela zile kwasababu wanajua uwezo wa Pogba na wamekaa nae msimu mzima.
Sasa inakuaje unaanza kulalamika hakuna Usajili wa Technical? Unadhani Ed anaamka kwenda sokoni bila kupewa list na Morinho?
Manchester United ni club kubwa duniani, hatujazoea kuishi kimasikini. Mambo ya kununua wachezaji kama Arsenal na timu ndogo tumeshaacha nao.
Pesa ipo, mchezaji analeta matokeo, jezi anauza, na TV rights zinaongezeka.
Unakua kama hujui biashara?
Pogba alirudisha hela ndani ya week, sahivi tunakula faida tu na uwanjani anadeliver.
Midfield ya Herera, Pogba imeanza kutulia, tumebaki kuongeza nguvu kidogo kuwe imara zaidi. Ushambuliaji nako kuna tatizo, tunahitaji washambuliaji wawili wa kuziba hiyo nafasi. Beki nako kuna nyufa za Smalling zinatakiwa kuzibwa.
World class strikers wapo wachache sana kwahiyo sitashangaa hata huyo Griezman akauzwa £100M na utanunua tu kwasababu huna option na hakuna timu ya kueleweka ambayo watakuuzia strikers. Ni sawa na mkulima akuuzie ng'ombe anayemletea maziwa kila siku.
Hadi hapo Morinho na Ed wamefanya kazi kubwa.