kwa mwendo huu wa timu yetu ninaoushuhudia tunapocheza na chelsea nimejivunza ya kwamba
- hatuwawezi chelsea kwa jambo lolote lile,miaka iliyopita nimezoea kuona tunafungwa na chelsea ila tunamiliki mpira sana dhidi yao ila sasa ni tofauti wanatufunga na wanamiliki mpira wao.
- bado hatujapata dawa ya kumdhibiti hazard na ataendelea kutusumbua kila mechi, wakati wa Alexander Ferguson alikuwa anamuweka Rafael mlinzi wa kulia na valencia namba 7 kidogo ilikuwa tunapata nafuu
- huu ni msimu wa nne chelsea wana viungo bora kuliko sisi,kutoka utawala wa ramirez,obi,essien,lampard mpaka amekuja matic,fabregas na kante bado wao ni bora kuliko sisi sehemu ya kiungo.
- juzi nilisema ya kwamba hatuwezi kuwafanya mabeki wa chelsea wakawa hawana amani kwa aina yetu ya washambuliaji, kutoka utawala wa super rooney, berbatov, chicharito, van persie mpaka utawala wa used ibrahimovic, poor rooney, rashford tuna safari ndefu sana ya kuweza kuzifunga timu kubwa kwa ushindi wa uhakika na ndio maana hatujawahi kumfunga mtu bao 5.
- huu ni msimu wa nne chelsea bado wametengeneza utatu mtakatifu bora unaotusumbua kule mbele kutoka utawala wa mata +oscar+hazard mpaka pedro+moses+hazard+willian lakini sisi mpaka leo wachezaji wetu hawakui kimpira sasa wamekua hawana tofauti na wachezaji wa arsenal.
- mpaka anapewa kadi nyekundu herrera nafikiri timu yetu ilikuwa haijapiga shoot target hata moja kwa hivyo hii hoja ya kuwa tumefungwa kwa sababu ya herrera ni hoja mbovu tukumbuke tulicheza na bournermouth wakiwa kumi tena uwanjani petu tulishindwa kuwafunga.
kwa mtazamo wangu
- tunapaswa kuelekeza nguvu zetu kwenye kombe la europe league kuliko kuwania nafasi ya 4, kwa sababu tulishapata nafasi mara mbili ya kuwa katika nafasi ya 4 hadi ya 2 ila tumeshindwa tena katika wakati ambao matokeo ya maadui zetu tulishayafahamu jambo ambalo ni mara chache kuwahi kulishuhudia. sifikirii kwa mwendo huu kama tunaweza kuwa na uhakika wa kuwafunga
chelsea - nyumbani (kwa sababu hatuwezi kuwazidi kimpira)
arsenal - ugenini (labda hawa ndio tunaendana nao kwa aina ya wachezaji wao na uwezo wa kufikiri wa kocha wao)
man city - ugenini (wako vizuri kuliko sisi)
tottenham - ugenini (wana viungo na washambuliaji bora kuliko sisi)
southampton - nyumbani (final walituzidi kimpira)
everton - nyumbani (mechi ya mwanzo walituzidi kimpira tukawa tunajihami kwa dakika 30)
middlesborough-ugenini (mechi ya mwanzo walituzidi kimpira kwa muda mrefu tukapata bao la ushindi dakika za nyongeza)
sunderland - ugenini
burnley - ugenini (tulitoa suluhu uwajani kwetu)
tumebakiza timu 3 ili tuweze kubeba ubingwa wa europe na kupata nafasi ya kushiriki UEFA mwakani