Mourinho alifukuzwa Chelsea kwa sababu nyingi na hii ya wachezaji kumgomea inaweza kuwa sababu ndogo sana
1.Ligi ya England competition ni kali sana nafikiri miaka 5 iliyopita hakuna bingwa ambaye ameweza kutetea ubingwa wake timu nyingi zilichukua ubingwa msimu uliofuatia kumaliza top 4 imekuwa challenge (Man City,Man United,Man City ,Chelsea,Leicester).Ushindani wa EPL ukichukua ubingwa hupaswi ku-relax unapaswa kumotivate/kusajili timu iweze kupambana upya.Management ya Chelsea,Mourinho na wachezaji wa Chelsea walirelax sana.Ivanovic,Matic,Fabregas Hazard,Costa walirudi kwenye timu wakiwa off form na walikuwa wamechoka baada kucheza sana
2.Ku-motivate players pia ni kusajili wachezaji wapya ambao watakusaidia kupambana upya,Management ya timu haiku-msapoti kocha kwenye usajili alitaka kuwasajili Stones,Varane na Pogba but hakumpata hata mmoja baada ya mambo kwenda mrama ilibidi kumsajili Pedro karibia na deadline ya usajili.JT,Ivanovic na Cahil umri ulishawatupa na Mourinho huwa anakupumzisha ukiumia tu,nakumbuka JT pamoja na umri mkubwa alicheza mechi zote 38 .Wachezaji waliosajiliwa Baba Rahman ,Djilobodji hawakuwa chaguo la kocha
3.Ule ugomvi wake na daktari ni moja ya sababu kubwa kupunguza morali ya wachezaji,wachezaji karibia wote hawakumuunga mkono kwenye ile kesi hata management ya klabu hawakuipenda so Jose alianza kubaki peke yake kwenye timu ambayo kila mtu alikuwa anampenda
4.Msimu wa 3 huwa ni challenge kubwa sana kwa Mourinho kote alipofundisha