Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Exactly huyu Carrick anaendelea kujifunza taratibu, Makosa lazima afanye hakuna namna, kinachohitajika ni kumpa wachezaji wenye profile sahihi na sio kumrundikia mizigo isiyoeleweka...

Tatizo linalokuja INEOS wanampa mzigo wote Carrick wakitegemea maajabu wakati mpira hauko hivyo sasa hivi, ili ushindane lazima uwe na jicho la kuona vipaji na kibunda kiwe mfuko wa shati...
Kumbuka mlimsajili Anthony kwa pound 100m, Pogba 85 shida sio kutoa pesa nyingi unatoa pesa kwa nani? Sisi tumemsajili Palmer kwa Pound 45 tu tena alikuwa benchi maker pale City angalia sasa anavyokiwasha, tumemsajili Mosses Caicedo kwa Pound 100 thamani yake ya Sasa ni zaidi ya hiyo tukimkosa tu unaona Kuna pengo, tukatoa pound mil 60 kwa Joao Pedro wakati kabla yake tumesajili strikers wengi wa Bei kubwa lakini wengi wameflop kama Lukaku kwa 95. Nimekutolea mfano hiyo uone wapo tuliwasajili kwa Bei ndogo na kubwa na wote wakatulipa nyinyi mnachokosa jicho zuri la kuona wachezaji issue hapo sio kutoa pesa nyingi unaweza ukatoa pesa nyingi akawa hafit mfumo wa kocha au akawa mbovu
 
Kwa jicho la haraka utagundua wachezaji wana mgomo na hari ya uchezaji imeshuka sana. Kwa mtazamo wangu nadhani matajiri wa timu wamechangia na m Carrick pia kachangia.

Ikumbukwe mwaka jana utd ilianza upya kusukwa kwa kununua wachezaji wapya hasa safu ya ushambuliaji na Amorim alifanya kazi kubwa sana ya kuwaondoa wazembe na wachezaji wasio na impact kwenye timu. Ule muunganiko wa Sesko, Mbeumo, Cuhna na Amad ulishafanya kazi vizuri tu na ulielewana. Leo INOES wakaamua kumrudusha Rashford haikuishia hapo Carrick naye kaamua kumuanzisha kikosi cha kwanza huku akiwaweka bench wachezaji waliomopigania msimu uliopita. Kikawaida tu nilazima wachezaji morali yao ishike kwa vyovyote vile.

Hao wachezaji sio wajinga. Ni nani asiyejua kuwa utd ilikuwa inaharibiwa na wachezaji kama Pogba, Martial na Rashford? Hawa wawili walishaondoka akabaki Rashford, alipokuja
Amorim akamhmuondoa eti leo Carrick anakuja kumuanzisha kikosi cha kwanza kila mechi kwa impact ipi aliyonayo?

Binafsi naamini utd hatutashinda mechi yeyote kuanzia sasa na hata tukileta kocha mwingine hatuwezi toboa shida yetu ni Morali ya wachezaji imeshuka sana baada ya baadhi ya wenzao kula bench ili muingereza acheze.

Huu unaweza kuwa msimu mbaya wa utd kuwahi kutokea na huenda tukashuka daraja ikiwa Carrick hata ongea na wachezaji wake na ikiwa hatomuweka Rashford bench. Kwa sababu ili Rashford aanze ni lazima kati Mbeumo, Cuhna au Seski aanzie bench hii inawakatisha tamaa kwa hawa vijana waliopigania timu.
Kubalini tu kwa Sesko mmepigwa huyo ni Kocha wa pili Sesko anaendelea kukaa benchi hujiulizi??
 
#Tielemans

'MIDO' ya Manchester United wanayoitegemea iwape kikombe chochote msimu huu 😆 nakumbuka hii 'MIDO' iliishusha daraja Leicester City na baada ya kuishusha mkataba wake ukaisha akagoma kuongeza kwasababu ya tetesi za magazetini kuwa Arsenal inamtaka kumsajili. Lakini Arteta akatupilia mbali 'MIDO' hii iliyokua ya bure, ikaenda zake Aston Villa ambapo Manchester United wakaona ndio 'MIDO' ya maana sokoni wakajifanyia 'SUPRISE' wenyewe kwa wenyewe

Wakaenda na Chelsea kuchukua Andrey Santos 😆 ila aisee kuna timu zimerogwa

Mpaka sasa msimu wa Manchester United umeshaisha, hawawezi kubeba EPL point nane wapo nyuma na bado wanakumbana na vipigo. Carabao Cup ndio byeBye hahahaha Uefa Champions League wabaki kuropoka 'TUNA UEFA' tu na FA Cup kuna Brighton bado

Kiufupi msimu wa Manchester United umeshaisha na sasa waingie studio kuimba kaWimbo kao kaKila msimu ".. ARSENAL HABEBI", Kwenye wimbo watasindikizwa na ndugu zao Chelsea
 
Wachezaji wa Manjesta wameshachoka hata ligi haijaanza

Mbaya zaidi wakamsajili Santos kibonge na Teleman ambaye ni abiria uwanjani .

Mancity hata wangekuwa 8 uwanjani Bado Manjesta wange struggle kuwafunga

HSbPWigWwAAgDzK.jpg
 
Kumbuka mlimsajili Anthony kwa pound 100m, Pogba 85 shida sio kutoa pesa nyingi unatoa pesa kwa nani? Sisi tumemsajili Palmer kwa Pound 45 tu tena alikuwa benchi maker pale City angalia sasa anavyokiwasha, tumemsajili Mosses Caicedo kwa Pound 100 thamani yake ya Sasa ni zaidi ya hiyo tukimkosa tu unaona Kuna pengo, tukatoa pound mil 60 kwa Joao Pedro wakati kabla yake tumesajili strikers wengi wa Bei kubwa lakini wengi wameflop kama Lukaku kwa 95. Nimekutolea mfano hiyo uone wapo tuliwasajili kwa Bei ndogo na kubwa na wote wakatulipa nyinyi mnachokosa jicho zuri la kuona wachezaji issue hapo sio kutoa pesa nyingi unaweza ukatoa pesa nyingi akawa hafit mfumo wa kocha au akawa mbovu
Chelsea yenyewe ni Tia maji Tia maji hawana mchezaji mwenye consistency hata mmoja maybe kidogo Kwa mbali Caicedo. Timu isiyo na Identity kama Chelsea haiendi mbele, hatua moja mbele hatua kumi nyuma, ni sawa na united haina clear structure so inabeba Tu wachezaji kama kubahatisha...
 
Manjesta bado hawajaonja joto ya jiwe,last season Kuna kipindi walikaa mwezi bila mechi, wakija kucheza wanakuwa fresh ,safari hii Kuna mechi kila baada ya siku 3,

Kuna ratiba ngumu huko mbeleni ,

Naona kabisa Manjesta yanited wakipiga yowe na v
HSXegE2WoAE809f.jpg
ilio
 
Cha ajabu Kuna mashabiki wa Manjesta wanaamini watabeba EPL,UCL na FA Cup

Wachambuzi huru tuliposema Manjesta waachane na mawazo ya ubingwa ,wajenge timu kwanza ,tuliitwa majina ya kila aina .
HSV-p06XIAARQu0.jpg
 
Unazunguka tatizo badala ya kulisema.

Timu mbovu.

Sesko tangu asajiliwe anakaa benchi haiwezi kuwashangaza leo.

Maino ailkua anawekwa bench siku hizi anaanza kwanini wachezaji wasimpende kocha badala yake mgomo uje kisa Sesko? Ambaye kuanzia benh ni kawaida yake.

Na angalau Carrick anamuanzisha baadhi ya mechi.

Hii timu ni mbovu mkipata matokeo mnasahau ukweli. Kama umeangalia mechi ya jana na hitimisho ni wachezaji wana mgomo basi na mashabiki mnachangia hii timu kutoenda mbele
Kwa hiyo wewe kwa akili yako ujio wa Rashford na kuingia moja kwa moja kwenye kikosi unaona ni sawa yaani alazimishwe yeye kuanza right wing ambayo kiuhalisia hiyo ni number ya Cuhna kisha Cuhna aanze false number 9 na number 9 halisi Sesko aanxie benchi unaona ni sawa?
Yaani kuna watu huwa ni waajabu sana mmoja wapo ni wewe. Ubovu wa timu upo wapi wakati tumeona timu hii hii msimu uliopita ilifanya vibaya chini ya Amorim kisha kulazimisha mfumo wake, akaja Carrick timu ikapaform vizuri na kufunga big six wote hadi kumaliza nafasi ya tatu.

Aliokuambia timu ikiwa na majina au usajili wa bei gali ndio inafanya vizuri ni nani? Kuna timu imefanya usajili EPL kama spurs? Je wapo nafasi ya ngapi? Hadi sasa kweny mechi tano za ligi na EFL wana goli moja.

Unachopaswa kuelewa ni kwamba wachezaji ni kama wanajeshi, huwezi kushinda vita au kupigana vita yeyote morali ikiwa chini. Na siku zote wachezaji huwa wanampambania kocha na timu, hilo unapaswa ulifahamu. Kitendo cha Carrick kusema yupo tayari kufanya kazi na Rashford hapo nilishajua anakwenda kuigawa timu. Narudia tena kusema kwa hali ilivyo sasa chini ya Carrick na uwepo wa Rashford utd hawatashinda mechi yeyote ile labda akae na wachezaji na akubali kumweka Rashford benchi.
 
#Tielemans

'MIDO' ya Manchester United wanayoitegemea iwape kikombe chochote msimu huu 😆 nakumbuka hii 'MIDO' iliishusha daraja Leicester City na baada ya kuishusha mkataba wake ukaisha akagoma kuongeza kwasababu ya tetesi za magazetini kuwa Arsenal inamtaka kumsajili. Lakini Arteta akatupilia mbali 'MIDO' hii iliyokua ya bure, ikaenda zake Aston Villa ambapo Manchester United wakaona ndio 'MIDO' ya maana sokoni wakajifanyia 'SUPRISE' wenyewe kwa wenyewe

Wakaenda na Chelsea kuchukua Andrey Santos 😆 ila aisee kuna timu zimerogwa

Mpaka sasa msimu wa Manchester United umeshaisha, hawawezi kubeba EPL point nane wapo nyuma na bado wanakumbana na vipigo. Carabao Cup ndio byeBye hahahaha Uefa Champions League wabaki kuropoka 'TUNA UEFA' tu na FA Cup kuna Brighton bado

Kiufupi msimu wa Manchester United umeshaisha na sasa waingie studio kuimba kaWimbo kao kaKila msimu ".. ARSENAL HABEBI", Kwenye wimbo watasindikizwa na ndugu zao Chelsea
Kwa akili yako kabisa timamu ulikuwa unaamini Man U msimu huu anawania ubingwa????
 
Chelsea yenyewe ni Tia maji Tia maji hawana mchezaji mwenye consistency hata mmoja maybe kidogo Kwa mbali Caicedo. Timu isiyo na Identity kama Chelsea haiendi mbele, hatua moja mbele hatua kumi nyuma, ni sawa na united haina clear structure so inabeba Tu wachezaji kama kubahatisha...
We jamaa mpira unajua kweli unataka kuniambia kuwa Palmer, Joao Pedro, Morgan Rogers hawana Consistency???
 
Kwa hiyo wewe kwa akili yako ujio wa Rashford na kuingia moja kwa moja kwenye kikosi unaona ni sawa yaani alazimishwe yeye kuanza right wing ambayo kiuhalisia hiyo ni number ya Cuhna kisha Cuhna aanze false number 9 na number 9 halisi Sesko aanxie benchi unaona ni sawa?
Yaani kuna watu huwa ni waajabu sana mmoja wapo ni wewe. Ubovu wa timu upo wapi wakati tumeona timu hii hii msimu uliopita ilifanya vibaya chini ya Amorim kisha kulazimisha mfumo wake, akaja Carrick timu ikapaform vizuri na kufunga big six wote hadi kumaliza nafasi ya tatu.

Aliokuambia timu ikiwa na majina au usajili wa bei gali ndio inafanya vizuri ni nani? Kuna timu imefanya usajili EPL kama spurs? Je wapo nafasi ya ngapi? Hadi sasa kweny mechi tano za ligi na EFL wana goli moja.

Unachopaswa kuelewa ni kwamba wachezaji ni kama wanajeshi, huwezi kushinda vita au kupigana vita yeyote morali ikiwa chini. Na siku zote wachezaji huwa wanampambania kocha na timu, hilo unapaswa ulifahamu. Kitendo cha Carrick kusema yupo tayari kufanya kazi na Rashford hapo nilishajua anakwenda kuigawa timu. Narudia tena kusema kwa hali ilivyo sasa chini ya Carrick na uwepo wa Rashford utd hawatashinda mechi yeyote ile labda akae na wachezaji na akubali kumweka Rashford benchi.
Lazima pia ujue msimu uliopita ni kwa sababu mlikuwa hamshiriki mashindano yoyote ya Ulaya kwahiyo nguvu kubwa mkawekeza kwenye ligi ndio maana mkafanikiwa kuingia big 4 Sasa hivi mnamashindano mengi, depth ya squad ni ndogo, Bruno Fernandes kachoka katumika sana World cup pia na umri unachangia na huyu akiwa kwenye ubora na Man u inakuwa kwenye ubora. Unaweza kutetea lakini Usajili mlioufanya sio wa kuimprove kikosi wachezaji mliowaleta ni wa kawaida na baadhi ya maeneo mmeshindwa kuleta kabisa watu kama LB, RB na Striker mmoja.
 
Kocha na Legend aliesema mabeki wazuri (good defence) itakupa mataji. Anaitwa sir alex ferguson

Hii hapa chini ndio Timu aliefundisha kwa muda mrefu, angalia inavyofanywa
Screenshot_20260917_151113_FotMob.jpg

Hiyo picha inaonesha Wastani wa mechi nyingi wakicheza
 
Kwa hiyo wewe kwa akili yako ujio wa Rashford na kuingia moja kwa moja kwenye kikosi unaona ni sawa yaani alazimishwe yeye kuanza right wing ambayo kiuhalisia hiyo ni number ya Cuhna kisha Cuhna aanze false number 9 na number 9 halisi Sesko aanxie benchi unaona ni sawa?
Sesko kaanzia bench tangu anasajiliwa. Kwa Carrick ndiyo anapata minutes za kuanza

Yaani kuna watu huwa ni waajabu sana mmoja wapo ni wewe. Ubovu wa timu upo wapi wakati tumeona timu hii hii msimu uliopita ilifanya vibaya chini ya Amorim kisha kulazimisha mfumo wake, akaja Carrick timu ikapaform vizuri na kufunga big six wote hadi kumaliza nafasi ya tatu.
Unaongelea timu ambayo ilikua inacheza mechi moja kwa siku 9. Ikawa inacheza counter zaidi na assists za set pieces za kapteni wenu. Huo mfumo wa Amorim ndiyo Brighton wamekupiga nao, ndiyo Milan unawaweka mjini Italy na sasa mnamtaka Conte, muumini wa mfumo huohuo. Punguza hasira dogo.
Aliokuambia timu ikiwa na majina au usajili wa bei gali ndio inafanya vizuri ni nani? Kuna timu imefanya usajili EPL kama spurs? Je wapo nafasi ya ngapi? Hadi sasa kweny mechi tano za ligi na EFL wana goli moja.
Hakuna sehemu nimeongelea usajili. Mimi nimesema timu yenu mbovu.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba wachezaji ni kama wanajeshi, huwezi kushinda vita au kupigana vita yeyote morali ikiwa chini. Na siku zote wachezaji huwa wanampambania kocha na timu, hilo unapaswa ulifahamu. Kitendo cha Carrick kusema yupo tayari kufanya kazi na Rashford hapo nilishajua anakwenda kuigawa timu. Narudia tena kusema kwa hali ilivyo sasa chini ya Carrick na uwepo wa Rashford utd hawatashinda mechi yeyote ile labda akae na wachezaji na akubali kumweka Rashford benchi.
Hujui kitu wewe. Hakuna cha mgomo kisa Rashford wala nini, timu ilitembelea kupumzika muda mrefu na upepo wa Amorim kwenye utimamu wa kimwili.

Juzi zimekuja takwimu zinaonyesha mpo nyuma kwenye ground coverage, nyuma kwenye kukimbia na Tielemans anasema mazoezi ya Villa ni magumu kuliko hapo united.

Wewe shabiki unasema tatizo ni Rashford
 
Makombe mengi aliyochukua nyumbu kipindi cha ferguson yalikua ya dhuluma

Ata unbeaten ya arsenal, nyumbu waliivunja kwa dhuluma. Unaambiwa hiyo siku vilitembea viatu sio mchezo

With advanced science and technology, nyumbu hana tena kichaka cha kujifichia.
IMG-20260918-WA0005.jpg

Kipindi nyumbu anakimbiza ligi kwa dhuluma 👆
 
Back
Top Bottom