Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Exactly huyu Carrick anaendelea kujifunza taratibu, Makosa lazima afanye hakuna namna, kinachohitajika ni kumpa wachezaji wenye profile sahihi na sio kumrundikia mizigo isiyoeleweka...

Tatizo linalokuja INEOS wanampa mzigo wote Carrick wakitegemea maajabu wakati mpira hauko hivyo sasa hivi, ili ushindane lazima uwe na jicho la kuona vipaji na kibunda kiwe mfuko wa shati...
Hakika mkuu, nitashangaa sana kama Manchester united wataingia sokoni kumtafuta kocha mwingine.
 
Arteta hakupata miaka 3 kwa sababu tu Arsenal waliamua kumuamini kipofu. Alionyesha progression 8→5→2→2→2→1. Sasa Carrick apewe miaka 3 kwa msingi gani? United waanze kwanza kuonyesha hiyo progression, si kuomba miaka 3 kabla hata ya kujua kama project inaelekea popote.
 
INEOS hawajui wanachokitaka, Yani wanategemea Carrick awavushe wakati Carrick naye anajifunza kazi so inabidi apewe muda kidogo sasa unapoleta profile za wachezaji wasioeleweka kazi ndio inakuwa ngumu Sana, ni kweli Kocha ana Makosa Yake but makocha wataendelea kutolewa kafara Hadi lini wakati management ipo ipo Tu, Management lazima iwe very clear na sio kutoa matuamini hewa....
Huyu Berrada naye sioni kitu alichokifanya hadi sasa, pale City alikuwa anatembelea upepo wa Guardiola tu.
Hadi sasa miaka 2 huoni direction ya project kuanzia usajili, mfumo zaidi ya kuboresha akaunti za akina Glazers na tajiri mwembamba.
 
Back pass kwenye half yetu zimekuwa zikitugharimu sana tukikutana na mpinzani mwenye high press.

Hapa tutamlaumu sana Carrick ila wachezaji kwa asilimia kubwa wanashiriki kupoteza alama 3 kwenye mechi zetu.
 
Back
Top Bottom