Tupate Darasa kidogo kutoka kwa
Geoffrey lea
Kwenye mpira mfumo lazima uwape wachezaji wa kila nafasi faida kulingana na kile wanachoweza kukifanya kwa ubora katika majukumu yao, lakini pia mfumo unatakiwa kuwarahisishia wachezaji wanachofanya uwanjani na sio kufanya kazi yao kuwa ngumu zaidi!!!
Kwa sababu Amorim anaanza mechi na 6 defensive minded players tena bila point of play kwenye attack (jinsi alivyoanza bila mshambuliaji asilia) maana yake timu inawatesa sana wachezaji kama Matheus Cunha na Bruno kwa jinsi ambavyo anaanzia chini sana kama mmoja wa wachezaji wawili wa kiungo
Hizi picha 3 hapo chini zinaonyesha jinsi Cunha alivyolazimika kuanzia safari yake mbali bila Teammate Karibu ambaye wangesaidiana either pasi au kuwaoccupy mabeki na kutengeneza njia nyepesi ya kupita lakini angalia amezungukwa na wapinzani wangapi,
Matokeo yake Cunha na Mbeumo walilazimika kutumia sana uwezo binafsi kushambulia kwa sababu mfumo haujawasaidia,
Katika mfumo kama wa 4-3-3 au 4-2-3-1 mbeumo cunha na Bruno watakuwa wanaanzia karibu na goli na kuspend muda mwingi wa mechi karibu na final third, Changamoto kubwa ya Amorim ni hii hata zile nafasi za kipindi cha kwanza zilikuja kutokana na uwezo binafsi zaidi kuliko mfumo.
Tofautisha na Arsenal ambao walikuwa wakishambulia wana options mbili au tatu kwa jinsi timu ilivyopangwa, System ya Amorim haiwezi kufanya kazi kwenye EPL tena especially dhidi ya Timu ndogo ndogo ambazo zinajua kucheza kwenye low block na kushambulia kwa counter.
View attachment 3445096View attachment 3445097View attachment 3445098