Kinachotakiwa ni kukomaa Tu, mechi ilikuwa ya kwetu kabisa. Yaani Arsenal utadhani walitoka Bar Kwanza ndo wakaja Old Trafford, kiuchezaji tuliwazidi lakini kwenye matokeo ambacho ndio muhimu zaidi wametuweka.
Tushapata funzo tayari, tuache papara , tutulie kwenye boksi magoli yatapatikana tu...Yule kipa toka msimu uliopita kwenye mipira ya Aina Ile hayuko vizuri. Lazima tupate kiungo box to box with legs, hatari niliyoiona ni kwamba tukikutana na timu zinazokimbia Sana basi soon tutamtukana Casemiro maana Combo na Bruno inaifanya timu sometimes haina balance japo hili huwezi kuliona Leo vizuri.
Wala tusiwe wanafki Leo timu ilikuwa unaona kabisa ina improvements kubwa Tu, kinachohitajika tuongeze intensity, tucheze Kwa nguvu mechi zote.