Jana tulikuwa na moment kadhaa za intensity za kuutaka mpira Kwa nguvu na Kwa haraka sana, hii ni ishara nzuri. Kwa jinsi system ilivyo Inahitaji kujitoa sana, kama umezoea kucheza nusu uwanja basi pole sana, Kwa jinsi back three zinavvyofanya kazi lazima timu nzima muwe tayari kukimbizana. Tunatakiwa misimu miwili mbele timu iwe na intensity ya Hali ya juu Kwa maeneo yote.
Lazima tuongeze kiungo ya kazi kweli kweli wa kusaidiana na Ugarte, huyu punda (ugarte) anakimbia na fiziki yake ipo vizuri, asije akaumia kipindi hichi tutakuwa exposed sana kwani Bado hatujajipata.
Mount anafaa kabisa Kwa system ya jamaa, kitakachomuua ni majeruhi tu daah. Tunahitaji kiungo mkali wa kusaidia pale kati. Muda huu ni wa kuwakimbiza wachezaji na kuhakikisha wanasuffer kweli kweli Ili tuondoe wachovu na wavivu wote watakao kuwa exposed na hii system.
Kwa system ya jamaa ni rahisi kujua wachovu ni akina nani maana unawaona kirahisi in training na kwenye game, tukiingia sokoni unajua kabisa huyu Kwa system yetu hatufai. Hatutaki wachezaji makobe na wavivu.