Wasitake kutuzengua. Man United walikuwa wanafukuza makocha kama timu nyingine tu kabla ya Ferguson. Kuwa wavumilivu wa makocha ni rahisi kusema kama timu ina mafanikio. Huyo SAF mwenyewe alivumiliwa mwanzoni mwa tenure yake Old Trafford kwa sababu alionyesha dalili ya mafanikio (he finished second on his first full season) alionyesha kuibadilisha timu for the better kwa kuondoa wachezaji wazee na walevi na unprofessional na akaleta overall professionalism na wachezaji vijana. Kuvumilia makocha ni sawa lakini kila timu ina bottom line yake. At United the bottom line is that the style of football shall not be compremised, hata Ferguson mwenyewe alishawahi kusema kocha atakayemfuata lazima aendeleze traditions ya kucheza mpira wakuvitia na mashambulizi. Sasa can they honestly say kwamba huyu Moyes wao ameendeleza hiyo tradition? Hata kama wachezaji alionao sio anaowataka mbona mwenzake Martinez ameweza kuwafanya Everton kucheza mpira wa kuvutia zaidi na wachezaji aliokua nao yeye mwaka jana?
Kitu kingine ambacho kinaniudhi mimi ni Moyes kujaribu kutulazimisha mashabiki tuamini kwamba wachezaji tulionao ni vilaza. Jamani timu hii hii iliyoipelekesha Madrid mwaka jana watu wakawa wanazungumzia future nzuri tuliyonayo na vijana wetu leo hii wote ni vilaza? Kwenye timu ya mwaka jana iliocheza na Madrid labda unaweza kusema Vidic ndo kazeeka (bado ni mdogo kwa John Terry kumbuka) leo hii galfa ni wabovu? Kwahiyo ndani ya mwaka mmoja wachezaji wa Everton wamekuwa wazuri zaidi ya United afu waUnited wamekuwa vilaza zaidi ya Everton? Kwa mfano jana alivyosema kuwa eti hata Ferguson menyewe asingeweza kuipata top-four na timu hii, kama so matusi hayo na kutuona sisi mataahira ni nini?
Huyu jamaa kanidangaya sana msimu mzima. Tunafungwa mechi moja au mbili muhimu mfululizo afu tunashinda moja au mbili against timu za kawaida afu eti ohh "we are turning a corner" ikija timu kamili tunachapwa tena! Akawandangaye hao hao wanaokubali kuendelea kudanganywa as for me Moyes OUT! Unless he wins the Champions League. Yaani kweli sisi tumekuwa watu wakushangilia ushindi dhidi ya West Ham na Aston Villa kama vile ndo tumeshinda Premiership?
Anyways I'm getting to worked up now, ngoja Bayern waje waprove point yangu.