Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,106
Mamlaka za maji nchini zina kiburi sana, hakuna nidhamu ya watendaji. Miradi ya maji wanapiga, kuunganisha watu maji awataki, wanabambikia wenye maji bili, ukienda ofisini kwao hakuna anayekuchukulia kama mteja kila mtu yupo busy na masuala yake, wengi wana elimu ndogo ya uchumi na hivyo wanaamini wao niwadhibiti huduma kuliko kutoa huduma.
Matokeo yake ni nini! Kwa sasa wametengeneza madeni mengi yasiyolipika kutokana na kujipangia bili wanazoona wao zinafaa. Mapato ya mamlaka hizi yanakwenda kushuka na watu wameanza kujiunganisha maji kinyemela mtaani.
Kwenye mamlaka nyingi kwa mujibu wa CAG kuna madeni mengi, maji yanapotea pale mabomba yanapopasuka na response kwenye huduma aidha kupokea simu au kutunza kumbukumbu za malalamiko hazipo.
Ukifuatilia zaidi unabaini ndani ya mamlaka mfano DAWASCO ya huko jijini kwa wafanya biashara wametengeneza vishoka ambao ni watumishi wanaobambikia watu bili then wanapokea rushwa na kuchepusha maji. Kuthibitisha hayo niwatonye DAWASCO wakague idadi ya watu waliokatiwa maji kwa miezi sasa na wametulia, means waliokata maji walifanya mchongo maji yapatikane kwa mgongo mwingine.
DAWASCO wapitie malalamiko ya wateja watabaini kwamba idadi ya wateja wanaojenga mahusiano na watendaji wao inaongezeka kwa kasi means kuna biashara inafanyika. Wapitie response za watendaji wao watabaini kila mtendaji anatumia namba binafsi kutongoza mteja na wanaotonhozeka wanapewa huduma aidha kwa mgongo wa nyuma au mfumo halali.
Kwa msingi huu, endapo waziri utaendelea kuwaacha watu wa DAWASCO na mamlaka nyingine za maji wajiamulie cha kufanya; endapo wateja wataendelea kukatiwa maji mkatulia bila kufuatilia chanzo; na endapo watendaji wataendelea kukalia kimya malalamiko ya wateja nakuhakikishia utaondoka. Mtu mmoja anawezaje kuchepusha mradi mzima wa mabomba ya maji kutoka mtaa A na kupeleka mtaa B bila mamlaka kujua?
Mhe. Waziri, ulichoambiwa na Chongolo Dodoma kikufundishe jambo, tengua teuzi za hawa watu wanaotia doa nchi, la sivyo ukiendelea kukaa ofisini utapoteza V nane unayotembelea.