Waziri Jumaa Aweso, mulika Mamlaka ya maji safi na maji taka Mbeya, wanabambikiza bili kwa wateja waaminifu

Mpingamkoloni

Member
Feb 14, 2021
13
32
Ingawa hili ni tatizo la kitaifa, lakini Idara ya maji mbeya ni tatizo kubwa.

Wanatesa sana walipaji bili wazuri. Huwa wanapandisha bili taratibu hadi wanafikia sehemu ambayo wanaona wao ndio stable na ajabu wenye malalamimo matumizi ya nyumbani huwa ni yaleyale, lakini bill zinabadirika. Kila wakati wanapotuma bili si rahisi kushuka chini.

Familia za watu watatu hadi wanne, utashangaa zinachajiwa bili kama za shule, wauza maji, wafyatuaji wa tofali au uwatengeneza maji ya chupa. Lakini ukiangalia wote wanaobambikiwa bili utagundua ni wale walipaji wazuri wa bili za nyuma.

Huwa wana tabia ya kupandisha bila kila mwezi hadi inapofika kuwa juu. Mfano utaona bili ya mwezi huu sh. 16,000/= bili ya mwezi ujao inakuwa 28,000/=, bila inayofuata 39,000/= kama waendeleza kulipa watapita 100,000/=. Wote wenye malalamiko haya, matumizi yao huwa yaleyale kila siku.

Kuwaita waje waangalie meter unapaswa ulipie, halafu mara zote hawaoni matatizo ya leakage lakini watasisitiza una leakage ndani. Kipindi mheshimiwa Rais alipokemea kubambikiza bili za matumizi ya kawaida karibu zote zilishuka chini ya sh. 20,000/=

Watu wa ndani wanasema kuna namna wanachezea bili kwa wateja waaminifu, ili kupunguza hasara ziletwazo na wateja wasumbufu.

Mheshimiwa Waziri wa Maji hebu mulika Idara ya Maji Mbeya. Angalieni wanaobambikiziwa bili kila wakati ni walipaji wa aina gani na inakuwa familia ya watu labda 4 inaambiwa ilipie zaidi ya laki moja, halafu familia yenyewe muda wote wapo Sido dukani, wanatumia maji usiku tu, meter imeangaliwa haina shida, mabomba ya nyuma yameangaliwa hayana leakage yoyote, nyumba ina ulinzi hakuna mtu anakuja kuchota maji muda familia isipokuwepo.

Hizo ni picha halisi kwa watu wengi.
 
Hii imetokea kwa Mzee wangu yupo Nzovwe. Nyumbani wapo watatu baba, mama na mfanyakazi. Bili mwezi huu 39,000 haya ni maajabu
 
Back
Top Bottom