DAWASCO Wanakata maji bure wanaorejesha kwa kati ya 15,000 hadi 150,000 bila kutumia control number;

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Naungana na ACT wazalendo kwenye hoja yao waliyoelekeza kwa Waziri mwenye dhamana na masuala ya maji: wateja wanaolipia kuunganishiwa maji ni wengi lakini hakuna vifaa. Ukiuliza unaambiwa serikali haijatoa vifaa. Wateja wenye mifumo ya maji isiyotoa maji ni wengi na hakuna sababu za kwanini maji yamekatika.

Wateja wanaobambikiwa bili za maji ni wengi sana na huu ni mradi uliobuniwa na viongozi na watendaji ambapo wanachezea mita za maji ili bili ziwe kubwa, wakileta bila kubwa wanatuma watendaji wao waende kukata; ukiomba kurejeshewa kufanyika kwa uchunguzi wa mita hakuna anayekusikiliza na lazima ulipe. Cha zaidi wanachosema ni kwamba serikali ndiyo inabambikia watu bili na siyo wafanyakazi hivyo malalamiko peleka kwa wanasiasa.

Kwa sababu maji unayahitaji ni aidha ulipe deni au utoa rushwa kati ya 15 hadi laki na nusu kulingana na ukubwa wa bili yako. Fedha hizi hazina control na number na hata waziri akifanya kuunda tume leo ikaenda kuangalia wateja waliokatiwa maji kwa mwaka huu, sababu za wao kukatiwa maji na njia walizotumia kurejeshewa maji watathibitisha kwamba bilioni za fedha zinalipwa kwa maafisa wa DAWASCO lakini haziingizwi serikalini.

Kama sisi tuliokaa vijiweni tunasikia haya malalamiko unataka kusema waziri hana taarifa? Kwanini hakuna hatua anazochukua? Kwa wingi wa hizi fedha nani atatuaminisha zinaishia mifukoni mwa maafisa wadogo? Kwamba kila msoma mita akifanikiwa kurejesha maji kwa watu wawili kwa siku kwa 15,000 kila nyumba ukazidisha kwa mwezi means anajioipa kati ya 600,000 hadi 900,000 the zidisha kwa idadi ya wasoma mita how much will it be per month

Kwamba hizi fedha vibarua wanajilipa bila wenye taasisi kujua? Madhara ya wizi huu ni kwamba DAWASCO imegeuka wakata maji siyo watoa huduma tena; wakikata maji wanapata fedha za mifukoni kwanini wasiwekeze kwenye kukata zaidi kuliko kuboresha huduma?

Mhe. Waziri haya mambo yanamchonganisha Mhe. Rais na wananchi. Lakini haya yote yanatokea wabunge wamekaa kimya; wakuu wa wilaya kimya; wakuu wa mikoa Kimya. Hii nimeunga mkono hoja ya ACT lakini huku Mwanza haya ni mbaya zaidi
 
Ndio maana huwa wanakata maji hovuo, kwasababu wanajua hiyo pesa ya kurejesha itaingia mifukoni mwao, wacha wale kwa urefu wa kamba zao, hili taifa limeshapotezwa muelekeo na kiongozi wake bubu.
 
Mtu akimuona mtumishi wa idara ya maji,anamchukulia poa,ila kiukweli kuna maokoto sana,halikadhalika na Tanesco,daaah! acha wale kulingana na urefu wa kamba zao.
 
Ndio maana huwa wanakata maji hovuo, kwasababu wanajua hiyo pesa ya kurejesha itaingia mifukoni mwao, wacha wale kwa urefu wa kamba zao, hili taifa limeshapotezwa muelekeo na kiongozi wake bubu.
Juzi home walikata, bimkubwa akasema wacha, kesho atakuja yule mzee (fundi) ataachia tu
 
Back
Top Bottom