Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewaita kazini vijana 1,453 kati ya 2,100 baada ya kupata kibali cha Rais Samia

Hiyo ni nyingi sana kwa mtanzania masikini, aliyemaliza chuo na kujishikiza kwenye vibarua vya hapa na pale ilimradi mkono uende kinywani. Hongera kwa wote hasa wale watoto wa kimasikini muende mkalitumikie taifa kwa weledi na uadilifu bila kusahau walio nyuma yenu family zenu na rafiki ikibidi.
Natabiri! Wewe kama ni mzee na una watoto,,basi wamepata baba bora sana. Najua umenizidi umri, shikamoo mzee wangu!
 
Ubaya wa kufanya kazi TRA ni mmoja tu watu wanakuoverate una pesa nyingi ngoja ndugu na jamaa wasikie utajuta hayo matatizo
Na ndivyo majority ya familia zetu za kiafrika zilivyo, yaani akitoboa mmoja tu wote wanamuangalia yeye. Ni upuuzi upuuzi tu.
 
Hongereni sana wapambanaji.

Hakika kila mtu ana riziki yake,Sisi ambao hatujabahatika huenda riziki yetu bado, kwahiyo hatuna budi kukomaa.

Inshallaaah!! Kila mpambanaji Mungu atampa riziki yake..

Oya mtaani sio poa wazee..🥱
Kauli ya kipuuzi, mtaani sio poa kwako tu.
 
We acha tu unakuwa tegemezi ndo maana hatuendi mbele kijana akioa tu matatizo yanazidi hapo
Kuna jamaa yangu yuko hapo tra, ila huwa ananikopa mara kwa mara wakati me mwenyewe naunga unga tu life.sema maisha yetu waafrica ni ngumu kuwakwepa ndugu,labda uwe unatoka familia za akina kikwete huko
 
Kuna jamaa yangu yuko hapo tra, ila huwa ananikopa mara kwa mara wakati me mwenyewe naunga unga tu life.sema maisha yetu waafrica ni ngumu kuwakwepa ndugu,labda uwe unatoka familia za akina kikwete huko
Ukiwa na kazi mtihani san
 
Back
Top Bottom