Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Tanga kuna uozo mkubwa, Serikali imulikeni

shamzugi

JF-Expert Member
Feb 28, 2021
493
996
Kwanza nianze kwa kuwapa salam.

Muende moja kwa moja kwenye malalamiko yangu. Ni jumanne ya wiki hii nyumba tunayoishi Mimi pamoja na wapangaji wenzangu tulikatiwa maji kutokana na baadhi yetu kulimbikiza malipo ya Ankara za Kila mwezi. Siku ya jumatano tulifanikiwa kulipa bili pamoja na faini, wakatuambia siku ya alhamisi tutarudishiwa maji.

Alhamisi hawajarudisha maji, tukawapigia simu wakadai mafundi wao walikua bize Sana ila ijumaa watakuja mapema. Ijumaa Napo Hadi kufikia saa sita mchana hawakua wamefika.

Tukawapigia simu Tena akapokea mdada naye hakutoa ushirikiano mzuri, Mana baada ya kupokea simu alijitambulisha nami nikajitambulisha na mtaa ninaotoka, akaniuliza namba ya mita ghafla akakata simu. Nikapiga simu Tena haikupokelewa.

Leo ijumaa nafika hapa namkuta mdada Ana nyodo ananijibu kwa kujiskia Sana anasema mafundi watafika hapa saa sita mchana kwahiyo watakuja kurudisha maji. Kama siku mbili za kazi hawajarudisha maji, he watarudisha maji ndani ya hizi saa mbili zilizobaki.

Mheshimiwa Aweso tunakuomba ututatulie kero ya huduma ya maji sisi wakazi wa jiji la Tanga. TANGA UWASA imeoza ndugu zangu, yaani Ni kero tupu.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom