Mambo ya kuzingatia katika safari za maisha yako hususani kwa sisi vijana

Ndege Tai

JF-Expert Member
May 6, 2020
4,046
7,453
Hakikisha haya mambo yanakua Siri kwako;

1. Masuala ya mahusiano yako
Hii haikumaanisha kujua status kwamba umeoa au umeolewa,hii imelenga watu ambao wanapenda kuongelea masuala ya mausiano yao mfano mwanaume kutangaza madhaifu ya mke wako kwa watu
2. Hali yako ya kifedha
3. Matatizo ya familia yako
4. Siri zako binafsi
5. Baadhi ya Mipango yako mikubwa na midogo pia
6. Hatua yako inayofuata
Mengine tuendeleze kwenye comment
 
Hakikisha haya mambo yanakua Siri kwako;

1. Masuala ya mahusiano yako
2. Hali yako ya kifedha
3. Matatizo ya familia yako
4. Siri zako binafsi
5. Baadhi ya Mipango yako mikubwa na midogo pia
6. Hatua yako inayofuata
Mengine tuendeleze kwenye comment
Hujafafanua tuyazingatie vipi sasa?! Elezea kinagaubaga ili andiko lako liwe msaada kwa wengine, kwa ulivyoandika sijui kama hao vijana watakuelewa...!!
 
Hali yako ya kiafya.
1. Unywaji wa pombe kupitiliza hasa hiz pombe zisizo na kiwango na za bei rahisi.

2. Ngono zembe na magonjwa ya zinaa.

3 .ulaji wa ovyo hasa wa mavyakula ya wanga na nyama nyekundu kupitiliza.

4. Kujitwika stress hasa za mapenzi na za kujilingalisha na waliokuzid kiuchumi.

5 . Kujali mda na kuwa mwaminifu kwako na kwa wengine.

6 . Kuheshimu ushauri mzuri kuhusu mienendo yako mibovu hasa kwa kutoka kwa wazaz wako na jamii iliyokuzunguka.

7 . Kuhonga mwanamke asie mke wako huku ukijifanya una hudumia wakati hauna mzunguko wa faida ya laki tano kwa siku , hii ni yakuacha haraka sna.

8.kuongeza maarifa kwa kujisomea na hata kwa tembelea maeneo mbalimbali ya hii dunia ili kujifunza .

9. Kuacha kujifanya unajua siasa na kujifanya unaandamna ili kuisaidia tanzania wakati taifa linatatizo kubwa la kimaadili kwanzia ngazi ya familia.
 
Hali yako ya kiafya.
1. Unywaji wa pombe kupitiliza hasa hiz pombe sizizo na kiwango na za bei rahisi.

2. Ngono zembe na magonjwa ya zinaa.

3 .ulaji wa ovyo hasa wa mavyakula ya wanga na nyama nyekundu kupiliza.

4. Kujitwika stress hasa za mapenzi na za kujilingalisha na walikuzid kiuchumi.

5 . Kujali mda na kuwa mwaminifu kwako na kwa wengine.

6 . Kuheshimu ushauri mzuri kuhusu mienendo yako mibovu hasa kwa kutoka kwa wazaz wako na jamii iliyokuzunguka.

7 . Kuhonga mwanamke asie mke wako huku ukijifanya una hudumia wakati hauna mzunguko wa faida ya laki tano kwa siku , hii ni yakuacha haraka sna.

8.kuongeza maarifa kwa kujisomea na hata kwa tembelea maeneo mbalimbali ya hii dunia ili kujifunza .

9. Kuacha kujifanya unajua siasa na kujifanya unaandamna ili kuisaidia tanzania wakati taifa linatatizo kubwa la kimaadili kwanzia ngazi ya familia.
🙏🏾🙏🏾🙏🏾
 
La muhimu zaidi kijana jifunze kuongea na kila mtu ktk lugha itakayokufanya uonekane smart na muaminifu,ujuaji unawaangusha sana madogo.

Kwa sababu huwa nawaona vijana wanajisahau sana,yupo mmoja (tumezoeana kiasi sababu wakati anakua nilikuwa naishi mtaa mmoja na wazazi wake)akanikuta nimekaa mahali napiga story na jamaa yangu mtoa mikataba ya vyombo vya moto kwa vijana kuhusu drivers wa Bajaj na bodaboda wanaoaminika then wakashindwa kupeleka hesabu kwa mabosi zao mwisho kunyang'anywa vyombo,so tukawa tunasema hii yote inatokana na uhongaji na kuwa na wanawake wengi.

Mwanzo alikaa kimya but ghafla akachomekea ”kama mimi mtu anipe chuma yake halafu nihisi kama anataka kuninyang'anya naenda kwa fundi namwambia abadilishe afunge vitu vibovu vibovu vile vizuri naviuza nakula maisha akiichukua akafe nayo mbele kwani yeye huyo boss huwa ahongagi?”,mimi ile kauli sikuichukulia serious sana kumbe dogo alikuwa bench hana cha kufanya mtaani akahangaika akapata # yangu akanipigia ananiambia sasa bro niunganishe basi na yule jamaa yako nina licence imekaa tu mfukoni anipe Bajaj ya mkataba!!!

Nilimwambia subiri nakupigia nikakata simu nikajisemea huyu hata kama ile kauli alipoitoa ningekuwa sipo na muhusika wala nisingehangaika kumtafutia maisha sikumpigia akawa ananisumbua nikamtia block.
 
Back
Top Bottom