Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Confirmed, Kikwete kavunja CC na Sekretarieti muda si mrefu. Nimeithibitisha toka kwa source mmoja ndani ya CCM

haisaidii kitu,its too late to decide...aliambiwa mapema hakuelewa,sasa maji yashamwagika,adeki tu coz hayawezi kuzoleka..vidonda,maumivu,hasira na mipango mikakati ya makundi baada ya huu mkutano ndio mapambio ya kifo cha CCM kuelekea 2015..
 
Bahati gani kama Lowasa atawania u rais na W.S wa CDM. CCM ANAZO SIFA ZINAZOWAGUSA WATZ WOTE hata watoto wa chekechea wanamjua. Wanamapinduzi tunamtaka Lowasa 2015.

Usijidanganye. Ikitokea Lowassa akatumia njia yoyote ile kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM, lazima atashinda uchaguzi mkuu. Sio kwa sababu namkubali, bali namfahamu. Kwa hili ninaweza ku-bet hata nyumba yangu, maana najua akiteuliwa atapita na mimi nitakuwa na nyumba mbili.
 
Lipo! Kuachana na ufisadi kwa vitendo.

Wangekuwa wanataka kuachana na ufisadi basi wangeshafanya hivyo. Ndio maana mafisadi (Akina Mkapa, Rostam, Chenge, Karamagi, Yona, Makamba, Lowassa na wengineo wengi) ndani ya chama hicho bado wanapeta na wataendelea kupeta kwa miaka mingi ijayo.
 
Inamaana mwenyekiti ndiye mwenye mamlaka ya kuunda/kuvunja CC?.....kazi ipo, acha tu amwage ugali wenzake watamwaga mboga!

Kweli kikwete ana mamlaka makubwa sana bado tu hajaamua kuwa dikteta!!! CC wenzake wako ok na hii pawa ya mwenyekiti? Hawatamwag mboga?
 
Hamna lolote huko!!!!!!!!! Sana sana ni kuhamisha mvinyo wa zamani kwenye chupa na label mpya ila ukakasi na mchachuko ni ule ule!!!!!!!!!!!!!!!!

Acha CCM wakajifariji nafsi zao wenyewe mbele ya macho ya umma tusiodanganyika kitu teeeena.

JK kishaivunja Sekretarieti na muda si mrefu ataivunja kamati kuu na kuiunda upya
 
Mhhhh!...
There are currently 404 users browsing this thread. (108 members and 296 guests)
 
Wangekuwa wanataka kuachana na ufisadi basi wangeshafanya hivyo. Ndio maana mafisadi (Akina Mkapa, Rostam, Chenge, Karamagi, Yona, Makamba, Lowassa na wengineo wengi) ndani ya chama hicho bado wanapeta na wataendelea kupeta kwa miaka mingi ijayo.

Na ndio maana napata tatizo na heading ya hii thread; hakuna maamuzi yoyote mazito yaliyochukuliwa bali ni kubadilishana ofisi tu miongoni mwa watendaji wa CCM.

Maamuzi mazito yangekuwa pale ambapo kina RA, EL et al wangezuiwa kabisa kutia timu katika vikao husika. Uamuzi mwingine mgumu ambao Kikwete anapaswa kufanya ni kuomba radhi kwa madudu ya uongozi wake hadi sasa na aweke ahadi thabiti ya kubadilisha mwendo.

Haya ndiyo maamuzi mazito taifa linayoyahitaji.
 
Tunasubiri kuona gamba litakalovuka! Wote tunajua ni kazi nzito kama kweli ccm ina mpango wa kujivua gamba!
 
Nimefurahi sana tena sana, kama mh. mwenyekiti kaliona hilo, basi huo ndiyo mwisho wa matapeli ndani ya ccm.
 
Confirmed, Kikwete kavunja CC na Sekretarieti muda si mrefu. Nimeithibitisha toka kwa source mmoja ndani ya CCM
Haya....siye yetu macho na masikio tu. Lakini najua hakuna mabadiliko yoyote watakayofanya hapo zaidi ya usanii tu....sanasana mbuzi wa kafara atakuwa Makamba tu. Kama anaubavu amng'oe Lowasa na Rostam....hapo Jk nitamuona kidume
 
yawe mabaya tu,,,, chama kifariki,tumkabidhi dr. Wa ukweli nchi,, akina majimshindo, kobello, na wengine wote cjui watakimbilia wapi kwa aibu...
Hiyo kitu nakuhakikishia haitatokea!!...hii nchi ni replica ya China,with multiparty system ambayo watu hawakuitaka anyways....nguvu ya umma? Please!.....let's clean our party and we'll talk about this in 2015,we are ready for yall!!
 
Ishi, hivi kujua kwanini CCM ilishindwa mpaka waka-amua kuchakachua matokeo ya uchaguzi mkuu ilihitaji kuajiri consultant? Hata mwenye uelewa mdogo wa darasa la 7 angetoa jibu hilo hilo! "KUKUMBATIA UFISADI na MAFISADI". Sasa kama CCM hawakujua hilo mpaka waka-ajiri consultant basi hakuna wenye hekima CCM.
 
Sidhani kama kuna lolote ambalo ccm inaweza kufanya kujiokoa.

.
Lipo moja tu mkuu wanaloweza kufanya:
Kuikabidhi serikali kwa chama kingine makini na chenye kujali maslahi mabana ya watanzania wote kwa ujumla.
.
 
Usijidanganye. Ikitokea Lowassa akatumia njia yoyote ile kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM, lazima atashinda uchaguzi mkuu. Sio kwa sababu namkubali, bali namfahamu. Kwa hili ninaweza ku-bet hata nyumba yangu, maana najua akiteuliwa atapita na mimi nitakuwa na nyumba mbili.

mkuu, labda ungetoa ufahamu wako juu ya lowassa, hii ingelisaidia wana jf na wengineo kwa ujumla kujua undani wake haswa,,, pliz help us with the info about him
 
Back
Top Bottom