Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Consultant aliyepewa kazi ya kufuatilia sababu ya JK kupata ushindi mwembamba kawasilisha ripoti nayo imetoa pendekezo la watuhumiwa wa ufisadi kutoswa kwani ndo njia pekee ya kurejesha imani kwa wananchi

Huyo consultant atakuwa alipewa hadidu ya rejea moja.

Ukweli ni kuwa ushindi kiduchu wa JK ni kwa sababu ya uwezo wake mdogo. Huo uwezo mdogo unafanya ashindwe kushughulikia mambo mengi ikiwemo ufisadi. Na wananchi wanamwona kama msanii fulani tu. Hivi ulishawahi kusikia nchi ina ambulance za bajaji, zimamoto za bajaji na matrekta ya power tillers sijui huku viongozi wakitesa na magari yenye thamani ya shs milioni 200 kila moja ikaendelea? Unategemea kiongozi wa namna hiyo atapendwa na wananchi wake?

Ni kwamba wananchi wamechoka
 
Kuna mapya yamejiri punde, naomba muda nifuatilie niwafahamishe.
 
Tunayasubiria kwa hamu mzee. Hivi Kikwete alipata kura nyingi katika majimbo yapi? Isije ikawa alipata kura nyingi kwenye majimbo ya mafisadi.
 
It's either hakuna wa kutoswa au watatoswa waliokuwamo na wasiokuwamo, yaani mafisadi na wanaowapinga wote watatoswa ili kuweka amani, atabakisha mandumilakuwili tu humo ndani. Bado kitambo kidogo. Kama ligi kuu inavyomalizika kifitna leo hii, ndivyo hivyo CCM watakavyomaliza yao kifitna hivyohivyo
 
na yule mbunge ambaye alifungwa kwa kukiibia chama cha michezo naye hachafui hali ya hewa? yaani ccm na wakazi wa sehemu hiyo wameona huyo ndio anaye wafaa?
 
Kwa utetezi wa Rostam na wenzake ni kuwa mbona majimboni mwao walishinda kwa ushindi wa Tsunami na JK alipata ushindi mzito sana? Anadai si sahihi wao kudaiwa kuwa chanzo cha kupungua kura za JK uchaguzi uliopita

Jimboni kwake kuna watu wangapi? Alitumia mbinu gani kupata kura? Yawezekana hawamjui vizuri kwani Igunga ni vijijini mno.
 
Huyo consultant atakuwa alipewa hadidu ya rejea moja. Ukweli ni kuwa ushindi kiduchu wa JK ni kwa sababu ya uwezo wake mdogo. Huo uwezo mdogo unafanya ashindwe kushughulikia mambo mengi ikiwemo ufisadi. Na wananchi wanamwona kama msanii fulani tu. Hivi ulishawahi kusikia nchi ina ambulance za bajaji, zimamoto za bajaji na matrekta ya power tillers sijui huku viongozi wakitesa na magari yenye thamani ya shs milioni 200 kila moja ikaendelea? Unategemea kiongozi wa namna hiyo atapendwa na wananchi wake? Ni kwamba wananchi wamachoka
Wabunge wenu wangerudisha magari basi tuuone mfano!
 
Hakuna la maana kutoka huko fisadi no. 1 ni baba riz1 kwaiyo naye atoswe 2ingie kwny uchaguzi au?
 
Wabunge wenu wangerudisha magari basi tuuone mfano!

Unajua Kobello ukiliangalia hili kwa mtazamo wa CCM vs CDM utakuwa hujalitendea haki. Suala hapa ni CCM inavyojaribu kurudisha mvuto kwa wananchi. Mtazamo wangu ni kwamba wamepoteza mvuto kwa sababu wana viongozi wabovu.

Jukumu la kuhakikisha kuwa pesa nyingi zinaenda kwenye uzalisha na siyo ulaji ni la serikali na hivyo Kikwete anawajibika moja kwa moja. Au yeye aliwapa wabunge marupurupu makubwa ili wanyamaze au apate kisingizio? CCM wanatakiwa kutofautisha kati ya Campaigning na Governing.

Ukishachaguliwa unaoondoka kutoka kwenye kukampeni na unaenda kugovern watu pamoja na resources.
 
Mi naipenda sana CCM. Sipendi atoswe mtu.
Meli imeng'oa nanga, kwa nini utose baharini, si usubiri pwani 2015.
Sipendi atoswe JK,EL, RA, Karamagi, Chenge, Sumaye, mramba, Makamba. Kwa nini?
Muwe na subira wanaCCM
2015 mnatoswa en bloc. Na Tanzania yenye mafisadi-free generation itazaliwa.
 
Msamaha wanini wakati muomba msamaha bado anamiliki mali za wizi na huku anaendelea kuhujumu uchumi? Mpaka dakika hii anapigana kulifilisi shirika letu pekee la umeme kwa kulidai bil 94 kupitia Dowans ambayo yeye mwenyewe alilazimisha wapewe mkataba, mpaka sasa anakula hela ya taifa kupitia TICTS kwa mkataba mbovu, mpaka sekunde hii Kagoda na pesa nyengine nyingi mno ya EPA haijarudi na madudu mengine mengi tu. Msamaha umpe wa nini? Ukiona mtu mzima anaomba msamaha kwenye mazingira kama haya ujue amewadharau na kuwaona wajinga na wapumbavu wote wanao ombwa mshamaha. Tangu lini mtu anaomba msamaha huku bado anamiliki mali ya wizi na anaendelea kuiba?
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom