Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Chiligati pia aliongeza, "Jamani, ufisadi ndio unatumaliza kama chama na wenzetu tunao humuhumu ndani"
 
CDM wanawekeza kwa vijana ccm wanajaza safu za mafisadi. Nape kama unajipenda toka huko utetee taifa lako. Maana hoja za vijana cdm ndo zimekufikisha hapo( ulidesa hoja za Mwita Mwikwabe Waitara)
 
Baada ya kikao, RA alisema "They won the battle but the fight is still on"

Naitafsiri kauli hii Kama RA haoni wa kumtisha, anajua anachotarajia au anachotaka kufanya karibuni.
 

Suala siyo kusafisha suala ni kuleta maendeleo, kufanya kazi with primary objective of helping poor and young people to get employment. CCM ikitaka kuvunja nguvu za CDM, haitoshi kuishia kwenye kuwastaafisha mafisadi bali iwe ni pamoja na kuwashitaki na kuwafilisi mali zote walizopata kwa njia ya kifisadi wakati huohuo isiwe tu inafanya kazi na maamuzi yake kwa faida ya Tanzania na vizazi vijavyo bali ionekane inafanya hivyo na starting point iwe ni kuwaongoza watanzania kujipatia katiba yao mpya bila ya ku-impose CCM's will on that. Anything short of that is same old same old.
 
Nani kateuliwa idara ya mambo ya nchi za nje? Hiyo iliyokuwa chini ya membe.
 

kama wewe unasitahili kuona machinga complex 5 dsm, hospital kama Muhimbili dar tano, na ujinga mwingine wa kikwete ni sawa. Lakini cement 5000/= nongwa, mbona kikombe kwa babu ni 500/=
 
Wilson Mkama kaukwaa ukatibu mkuu wa CCM, Makamba nje!

Ni kama ilivyotabiriwa na mwana JF mmoja January 12, 2011 hapa ~ https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...lson-mukama-anaandaliwa-kumpokea-makamba.html

namshukuru mungu kile nilichokuwa nimekisema kupitia jukwaa hili kimekamilika na hili jina na WILSON MUKAMA nilichukulia pale kwenye hoteli ya moven pc , watu humu hawakuniamini ila sasa nadhani watakuwa wananiamini pindi nitakapo kuwa na ripoti humu, na sihili tu nilisharipoti mengi humu nikashambuliwa ila yakatokea nikaamua kukaa kimya, kwakuwa ukiwa kiongozi mwenye busara ya uongozi hutakiwi kubishana na wasiyo jua, unawaacha ukweli utawaambia kama leo ulivyo waambia thanks god......
 
Huyu jamaa alikuwa na Keenja Jiji la DSM,baada ya hapo nkumbuka kama alikuwa katibu mkuu wizara moja wapo ya awamu ya nne.

Yah. Akawa katibu mkuu wizara ya afya then maji alikostaafu. Baadaye kwa sasa ni mwenyekiti wa bodi yao ya TSN. Pia nasikia ni mwenyekiti wa bodi ya mradi wa maji wa ziwa victroria. Kuna mamlaka nadhani inaitwa KASHUWASA. Ni mjanja mjanja hivi huwa nashindwa nimweke kundi lipi
 
1.nchimbi waziri?
2.meghji ubunge na uccm ataweza kweli?

hapo dogo nape imetulia.
 
Wanajamvi nakumbuka kuna kipindi makamba aliwahi kumlaani nape na kusema hata samehewa mbinguni na ahera, duh kweli siasa ni mchezo mtamu sanaaaaaaaa, tetesi zinasema makamba jana alitaka kuondoka arudi tanga baada ya kujizuru watu wakamzuia
 
Yaap, yaap. Kwa kawaida ya Y.Makamba nae atakuwa anasubiri vikao kutoa maoni yake au ndo ataharibu zaidi?
 

Wananchi wanaandamana kwa kuwa hawana ajira. Wananchi wakafanye kazi gani?, wakati wakilima huko vijijini mazao yanaozea shambani?, wakija mijini hali ni ngumu wakati watawala waliopewa dhamana ya kuweka mazingira hayo wakiwa wamelala usingizi na kufikiria jinsi yakutengeneza mikataba feki ili wachote fungu wanaloliona lipo idle?.

Watanzania si wavivu kama ufikiriavyo, uchumi si kutoa takwimu tu bali kuwezesha watu kuwa na matumaini ya kuuza mazao yao kwa wakati kutoka mashambani, CCM hilo hawalioni wao uchaguzi mmoja ukiisha wanaanza kufikiria kupata pesa ya uchaguzi mwingine. Adui namba moja wa maendeleo yetu ni CCM na (viongozi wake ambao wengi wanaishi kwa matumaini kwa kukosa maadili na kupata magonjwa sugu - Mch Mtikila), hebu fikiria mtu mwenye terminal desease kama HIV ndiyo kiongozi wako atakuwa na mawazo ya future generation kweli?, atakachofanya ni kujilimbikizia ili mungu akimuita wanawe na nduguze waendelee kutumia alichoiba si kutafuta vyao kwa kuwa kawaachia mazingira mazuri ya wao kufanikiwa kwenye nchi yao if they work hard.
 
:redfaces: Wanajamvi wenzangu kwa nini watu wanapoteza muda kujadili CCM kuvua gamba? Kwa kauli ya Mh. JK kuhusu kujivua gamba alimaanisha CCM ni nyoka na tayari ameshatuuma kiasi kikubwa kupitia IPTL, Deep Green, Meremeta, Richmond a.k.a. DOWANS, EPA na mengine kibao. Gamba jipya litusaidie kumwona Nyoka huyo hata kama atajificha gizani.
Kwa sasa ndiyo inabidi tukaze buti zaidi maana Makamba alikuwa mwanamipasho lakini aliyetumia pesa za Kagoda si yeye. Anayewalinda wahalifu kama Rostam, Karamagi na wengine ni JK mwenyewe na tabia hii imemfanya awe mzito hata kuwakemea watumishi wengine wa serikali wanaofanya ufisadi wa kufuru (lakini kwa kuwa vyombo vya habari haviwafuatilii sana wengi wao hawajulikani).
​
Kwa makosa ambayo CCM wameyafanya hakuna msamaha wowote unaofaa kuwaacha madarakani. WanaJF tusiishie kujadili hapa jamvini bali tujitahidi kuwaelimisha wenzetu ambao kwa bahati mbaya hawapewi taarifa za kutosha kuhusiana na uchafu wa Chama hiki kilichoamua kwa makusudi kujiita Nyoka kwa kuwa nia hatari sana.
 
Mukama mwenyewe ndiye huyu..........
 
Last edited by a moderator:
Mwizi ni mwizi tu ndugu, hawezi ridhika...kama ameshaiba vyakutosha kama unavuo muambie akatulie ale hizo hela na sikutaka kuwaibia wadanganyika tena
 
Baada ya kikao, RA alisema "They won the battle but the fight is still on"

Naitafsiri kauli hii Kama RA haoni wa kumtisha, anajua anachotarajia au anachotaka kufanya karibuni.

bado yumo kwenye system, kama ni kwenye kompyuta basi wame-unistall halafu wamesahau baadhi ya values kwenye registry
 
Wanajamvi nakumbuka kuna kipindi makamba aliwahi kumlaani nape na kusema hata samehewa mbinguni na ahera, duh kweli siasa ni mchezo mtamu sanaaaaaaaa, tetesi zinasema makamba jana alitaka kuondoka arudi tanga baada ya kujizuru watu wakamzuia

Ha ha ha! Alitaka kuondoka kabla sooo halijaisha huyu vipi? Hivi kumbe na huyu mzee anaonaga aibu. Ha ha ha!!!
 
Watu wamekaa tangu jana wanamuangalia kinyonga anavyojaribu kubadilika rangi, wanaombea kuwa atageuka kuwa kambale!!.. Tuna moyo.
 

Mkurugenzi wa habari:

Wakati wa kampeini za uchaguzi 'Mhariri' wa gazeti la serikali aliandika kuwa mgombea wa CDM hatashinda.......jambo ambalo lilionyesha dhahiri vyombo vya umma kutumiwa na chama tawala katika kampeni jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu. Bwana "Mukama" hakusikika kumkemea Mhariri huyo.

Ilani ya CCM 2010-2015:

Amehusika kutunga ilani ambaye mwenyekiti wa Chama kashasema haitekelezeki..... wakati akijibu hoja za CDM

Ni mtu wa system:

System inatuhumiwa kuvuruga matokeo ya uchaguzi uliopita.

Mimi nadhani kuhusu Mukama kutunga ILANI ya CCM 2010-2015 isiyotekelezeka ilitosha kutompa nafasi ya Ukatibu wa CCM, huo ni mtizamo wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…