Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Mambo mazito CCM Dodoma: Wajivua gamba?

Ndugu Zangu,

TAARIFA zimetufikia, kuwa Mwenyekitiki wa CCM, Jakaya Kikwete amevunja CC na Sekretariati nzima ya CCM.

Tafsiri yangu; haya ni mabadiliko makubwa ndani ya CCM tangu kuundwa kwake mwaka 1977. Mabadiliko makubwa ya kichama yalifanyika mwaka huo wa 1977, wiki mbili tu baada ya CCM kuundwa.

Kuvunjwa kwa CC na Sekretariati kuna tafsiri kadhaa za haraka. Angalia hapa, ina maana; CCM imeondokana na Rostam na Chenge kwenye CC. Wawili hao hawarudi tena kwenye CC mpya itakayoundwa. Ndio, CCM wana namna zao za ' kufukuzana' wanapoacha ' kulindana'.

Na hiki ndio kile tulichoambiwa; Chama Kujivua Gamba, au labda magamba. Na kuna changamoto kwa Mwenyekiti wa Chama hicho- Unafanyaje na magamba yaliyovuliwa? Unayafukia, au unayaacha yakitapakaa? Na Magamba mengine hayaozi!

Ndio, Uchaguzi uliopita ulikuwa na ujumbe mmoja mkubwa kwa CCM kutoka kwa wapiga kura. Ni huu; MABADILIKO. Ndio, Watanzania wanataka mabadiliko. Kilichotokea Dodoma jana usiku ni jaribio la CCM kujibu matakwa ya wananchi. Je, wamefaulu? Tuna sababu ya kusubiri huku tukipima upepo unavyovuma.

Kuna maswali pia ambayo hatujapata majibu yake. Moja ni hili; Je, Mabadiliko haya ndani ya CCM yana ukubwa na athari gani kwa wakati huu na ujao?

Yepi zaidi yanakuja?
Tegemea - Kuwa asubuhi hii JK atakuwa 'busy' akishauriana na ' wazee' akina Msekwa, Mwinyi, Malecela, Mkapa na hata Spika Makinda. Wamsaidie mawazo katika kupendekeza majina kama 26 hivi yatakayopelekwa kwenye NEC ili yapigiwe kura na kupatikana wajumbe 18 wa CC.

Tegemea- Kuwa mengi ya majina hayo yakayopendekezwa yatatokana na wajumbe vijana wa NEC.

Nani atakuwa Katibu Mkuu?
Tegemea - Kuwa Katibu Mkuu atakuwa ama kijana au ana sura ya kijana. Jina kama Emmanuel Nchimbi si la kulibeza, William Lukuvi si ana sura ya kijana?

Kwa yanayotokea Dodoma CCM itakuwa imemaliza kazi ya ' kujibua' au kujivua gamba?

HAPANA. Kazi hiyo lazima iendelee. Kwa vile Sekretariati itaundwa upya, basi, kutakuwa na sura nyingi mpya. Tegemea, kuona vijana wengi zaidi wakipewa nafasi kwenye Sekretariati. Makatibu Wakuu wengi wa Mikoa na Wilaya watapanguliwa. Na vijana wenye fikra za ' kizamani' nao watapotea, na hapa, Tambwe Hizza laweza kuwa ni jina la ' vijiweni' kule Temeke Mikoroshini. Na kuna wengi ndani ya CCM wanaofanana na Tambwe Hizza.

Na upi ni mtihani mgumu kwa JK kwa sasa?
KATIBA MPYA, KATIBA MPYA, KATIBA MPYA….. ! Ndio, Watanzania wengi wa sasa na hususan vijana wanataka MABADILIKO, na Katiba kwao ni sehemu muhimu ya mabadiliko hayo. Watanzania wameshaamka na kubaini, kuwa KATIBA yao ya sasa nayo ni ' Maghumashi'. Neno hilo la mitaani lina maana ya mambo ya kiini macho na ubabaishaji.

Kwa vile JK ameshawajengea matumani ya kuwasaidia kupata Katiba Mpya itakayokidhi matakwa ya wakati uliopo na ujao, basi, nao wanataka iwe hivyo. Na kama JK atataka abaki akikumbukwa hata na vizazi vijavyo, basi, awe na ujasiri wa kuwasaidia Watanzania kupata KATIBA MPYA itakayolifanya taifa hili liwe la kisasa na lifanye mambo yake ikiwamo chaguzi katika mazingira ya kistaraabu. JK ana lazima ya kuacha kuiangalia kwanza CCM na bendera yake, badala yake aingalie kwanza Tanzania na bendera yake. Maslahi ya Nchi Kwanza. Maana, tunakokwenda, hata ndugu wa JK wanaweza wasiipigie kura CCM.

Na walioandaa Muswaada wa Sheria ya Kuanzisha Mchakato wa Katiba kimsingi wamechangia kumpunguzia JK heshima yake. Muswaada ule ni wa kiwango cha chini sana. Na JK akikubali kuasisi mchakato wa Katiba kwa kufuata ' ramani' ile tulioletewa juzi na kuambiwa tuitolee maoni, basi, nahofia, kuwa kuna watakaosema mitaani; " Na JK naye ni Maghumashi!"

Maggid
Iringa,
Jumapili, Aprili 10, 2011
0788 111 765http://mjengwa.blogspot.com
 
Duh Six kaingia ulingoni, hapo patamu maana huyu anadunda kama Tyson, sema neno moja tu na roho yangu itulie. Fukuzeni mafisadi, hawamo kabisa katika kundi la wakulima na wafanyakazi.:hug:

Fisadi mmoja mwenye akili kasepa mapema wenzake vipofu hawakumwelewa kabisa anaheri yeye aliyesadiki na kuamini manabii wayasemayo!
 
walioko kwenye ma baa pombe zote zimewatoka, walioko nyumbani usingizi umeisha, kesho makanisani ni fujo tu. Kuna watu wanahofia kama EL na RA wanaona watashugulikiwa basi watatumia influence yao yote , bora Mwamunyange awashe vifaru tayari kwa kutuliza fujo....ikishindakana tu kodishe wale ma-bouncer walioenda tegeta, na hao wakishindwa basi wakazi wa kule tegeta, inaonekana hao hawashindwi kitu!

Umeamua Kutuchekesha
 
Hivi watu wa vijijini ambako Ccm ina wanachama wengi wanajua kuwa chama chao kina mipasuko na hakina dira ya kumkomboa Mtanzania? Ni jukumu letu sisi kuwahamasisha watu wa vijijini na kuwaonyesha ni kwa jinsi gani ambavyo Ccm si mkombozi wao wa kweli.
Saa ya ukombozi ni sasa.
hata sasa hivi hawajui kuwa CC na NEC wamekaa dodoma na wala hawajui maana ya CC na nec wanaijua ccm tu basi.
 
Pengine hansemi MAGHUMASHI huko Kalenga ,sisi huku kwetu watu walishasema MAGHUMASHI siku nyingi!!
 
Hivi watu wa vijijini ambako Ccm ina wanachama wengi wanajua kuwa chama chao kina mipasuko na hakina dira ya kumkomboa Mtanzania? Ni jukumu letu sisi kuwahamasisha watu wa vijijini na kuwaonyesha ni kwa jinsi gani ambavyo Ccm si mkombozi wao wa kweli.
Saa ya ukombozi ni sasa.
wanachunga ngombe sa ivi na kupalilia waiting for r next 2015 election to get makofia yao na t shirt
hata kikwete alipaswa kujizamisha mwenyewe na wala asisubiri kuzamishwa.........
not in Tanzania, even history cant judge this
 
Mkuu hawa jamaa hata wafanyaje maji yameshafika shingoni wameshafanya permutation na combination za kutosha lakini hakuna anweza kubadilisha mawazo ya watanzania wengi hasa wasomi kuhusu chama tawala ccm wameprove failure na kama ni waungwana wangekubali kustep down kistaarabu sio mpaka tupigizane kelele
 
ni mwanzo mzuri wa mageuzi ya kweli ndani ya chama tawala, hatua hii imewafurahisha wengi,sasa kinachosubiriwa na wananchi ni kuhakikisha wale wote wenye kashfa hawarudi kwenye nafasi za uongozi. Baada ya hapo iwe ni kujenga nchi kwa kutekeleza yote yaliyosemwa kwenye ilani ya chama. kwa kufanya hivyo,mambo yatakuwa safi sana CCM na kinyume chake itakuwa aibu aibu aibu aibu sana.
 
Lazima ccm ijuvie gamba otherwise mambo yataendelea kuwa machungu
 
Umewataja nchimbi na lukuvi. Hawa kaka ni mawaziri. Wasimamia sera na ilani yao iliyowaweka madarakani. Wasipofanya hivyo kwa umahili mkubwa chama kiwabane. Sasa kwa nafasi ya ukatibu mkuu watabanwa vipi. Hili pia ni kosa linalokitafuna chama. Mawaziri hao hao,nec hao hao, cc hao hao!
 
Baada ya kamati kuu na secretariat ya ccm kuvunjwa (magamba kuvuliwa) sasa ccm lazima wawe makini kuweka watu ambao wanapiga vita ufisadi si kuweka mafisadi
 
watu wa vijijini wanajua ccm ni safi kwa jinsi alivyoiacha nyerere! Ambaye alikuwa ni bingwa wa kuzima mipasuko iliyowahi kujitokeza enzi zake,mfano Aboud Jumbe alivyowajibika ili kunusuru chama, muungano na taifa.Kwa sasa hiyo kitu hamna ! Utawala wa sasa unawajibika pale ambapo tayari magazeti yameshaandika sana.Mimi najiuliza je ingekuwa ni chama kimoja tu wananchi wangekuwa na hali gani? Kiwango cha ufisadi kingekuwaje? Ikiwa hivi sasa wapinzani na vyombo vya habari vinapiga kelele lakini watu wenye dosari za waziwazi wanaachiwa washike nyazifa za juu kwenye chama na hata serikalini.
 
Katibu mkuu wa CCM na Sekretarieti nzima ya CCM imelazimishwa kujiuzulu. Hapa nipo Dodoma na mambo ni mazito. Uchaguzi kesho....Ila huyu mzee, lake kubwa ilikuwa ni kumfikisha mwanaye wa kiume kwenye uwaziri na Bintiye wa Vodacom Ukuu wa Mkoa au Viti maalum.

Mpango mzima ni kwamba, wajinadi sana kwenye vyombo vya habari, wanaonekane wachapakazi na kisha kuzawadishwa. Kwenye kura za maoni, wengi ndani ya chama walilalamika kuhusu Makamba kuingilia maswala na taratibu nzima za kura za maoni lengo lake kubwa likiwa ni kumuingiza mwanaye kwenye ubunge.

Kwa sasa huyu mzee ana bifu za kichinichini na JK kwa maana JK hakumchagua mwanaye kuwa Waziri. Basi hapo, akajiingiza kwenye mtandao wa RA na EL ili mwanaye awepokwenye baraza lijalo.


JK alifika kumuuliza YM ni kwa nini mwanaye anamdhalilisha hasa baada ya taarifa kutoka Usalama kumfikia kwamba February Makamba kamtishia binti wa Rockefeller...Ama kweli CCM imefika mwisho..kuna mengi sana na hizi habari ni za ndani mno, Nyeti

Ukweli Makamba ameigharimu sana CCM na Uraisi wa Mh. JK. Mwaka jana alichukua hela za wagombea sana na kubadilisha matokeo na alimtumia mtoto wake mmojawapo pale kwenye makazi yake Morogoro.

Pia amechukua sana hela za watu aliowaahidi kuwa watapatiwa vyeo vya UKUU WA WILAYA na wengi wao ni wale waliogombea Ubunge wakakosa mwaka jana. Ukweli Makamba ni mtu wa vibahasha na Usalama wa Taifa walishapeleka taarifa nyingi naona busara za JK alikuwa anaamini atajirekebisha.

Asiishie hapo ajitahidi kufanya uteuzi wa watu wanaoeleweka sasa na Usalama umsaidie maana wanaweza mpindua kama Zuma alivyofanya Afrika ya Kusini. Awatumie vijana kama zamani, vijana wenye maono si type ya lumbilumbi kama akina Shigela na Malisa. Shigela alikuwa kijana mzuri sana lkn alipokubali kutumikia kundi la mafisadi amebadilika sana na mi kwa ushauri wangu hata yeye pale ang,olewe.

Watu wanawataja Lukuvi, Nchimbi na Wasira nakwambieni hawa hawafai bado ni watu wa makundi na Nchimbi ana ndoto pia za urais na Lukuvi anajiona nafasi ya Ukatibu Mkuu haimfai atafutwe mtu mwelewa msikivu na ambaye anaweza shuka chini kuona matatizo ya wananchi. Kuna balozi mmoja amepata kuwa mkuu wa mkoa jina limenitoka angefaa huyo nikipata jina nitawapatieni. tuwe na siasa za kiushindani na zenye muelekeo wa kuthamni zaidi maslahi ya taifa.
 
Ndio, Uchaguzi uliopita ulikuwa na ujumbe mmoja mkubwa kwa CCM kutoka kwa wapiga kura. Ni huu; MABADILIKO. Ndio, Watanzania wanataka mabadiliko. Kilichotokea Dodoma jana usiku ni jaribio la CCM kujibu matakwa ya wananchi. Je, wamefaulu? Tuna sababu ya kusubiri huku tukipima upepo unavyovuma.

urongo wa mchana huu!!

watanzania hawakupiga kura kutaka mabadiliko kwenye nec wala cc za ccm. huu ni uwongo mtakatifu na upotoshaji uliotukuka na wala hautakubalika popote na watu wanaojua mambo.

wajivue ama wavae gamba........who cares?

to hell with them!!!!
 
Sijaona kitu kabisa. Kama ndo hao basi CCM itakuwa imepaka rangi gamba lake na siyo kulivua. Upande wa wapinga ufisadi ndo unatakiwa kuongoza chama siyo remotely contrelled na mafisadi kama Nchimbi. Asipoaangalia JK, mafisadi watamchezea pele hapa kwa kuweka watu wao.
 
Rais Jakaya Kikwete anaonekana kuchukua hatua kuwahi kuwafukuza mafisadi kwenye chama kabla ya wao kumuwahi na kumfukuza. Yaliyoandikwa na KULIKONI la Ijumaa ndiyo yaliyotokea Dodoma kwenye kikao cha Kamati Kuu baada ya mjumbe mmoja kuibuka na hoja ya JK kuachia uenyekiti wa CCM. Matokeo yake ni kwa Kikwete kuivunja Kamati Kuu yote pamoja na Sekretariat. Tuone sasa mchezo wa NEC utachezwa vipi leo...



Mafisadi wapanga
'mapinduzi' CCM



  • Lengo ni kuzuia kufukuzwa kwao kwenye chama

  • Mbinu zasukwa kumwengua JK kama mwenyekiti wa CCM

  • Mabilioni ya shilingi yatengwa kukiteka chama

MWANDISHI WETU
Dar es Salaam

KUNDI hatari la wanachama waandamizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
ambalo linajumuisha watuhumiwa wakubwa wa ufisadi nchini sasa
linapambana usiku kucha ili kujaribu kuzuia chama hicho kuwatosa katika
kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya chama tawala (NEC) wiki ijayo,
KULIKONI limeelezwa.

Mkakati wa kuwaengua watuhumiwa wa ufisadi umeelezwa kuwa ni sehemu ya
utekelezaji wa kauli ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ambaye
alisema ili kukabiliana na upinzani chama hicho tawala ni lazima
kiwatose wanachama wake ambao ni mzigo kwao.

Katika hotuba yake ya hivi karibuni, Rais Kikwete, alitumia msemo wa
kuiga nyoka wanaojivua gamba na kwamba ikibidi ni lazima CCM nayo
‘kujivua gamba’ na kubaki chama kisafi kisicho na doa.

Habari zinaeleza kwamba, baada ya kauli hiyo ya Kikwete, baadhi ya watu
ndani ya chama hicho walianza kujipanga kupendekeza kutoswa kwa
watuhumiwa wa ufisadi walio ndani ya uongozi wa chama hicho ili
kukiepusha chama hicho na tuhuma zilizoelekezwa kwao.

Tuhuma ambazo zimetajwa wazi wazi katika vikao vyama chama hicho,
ikiwamo vile vya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM), ni pamoja na
kashfa ya mradi wa umeme wa dharura uliokabidhiwa kampuni ya Richmond
na baadae mrithi wake Dowans.

Pia vigogo wa CCM waliohusishwa na tuhuma ya ufisadi wa rada nao ni
miongoni mwa 'magamba' ambayo makada wa chama tawala wanataka
kuondokana nayo.

"Unajua kuna kundi moja hatari sana CCM ambalo ni mtandao unaojumuisha
vigogo wenye tuhuma kubwa za ufisadi ikiwemo kashfa ya Richmond, rada,
Kagoda, Meremeta na tuhuma nyingine chafu," alisema kada mmoja wa CCM.
"Kundi hili limetenga mabilioni ya shilingi ili kinara wake ndiye awe
Rais ajaye licha ya kuchafuka sana kwa tuhuma nyingi za ufisadi na
kujilimbikizia mali ndani na nje ya nchi."

Tuhuma hizo zimeelezwa kuwa chanzo kikubwa cha kushuka kwa umaarufu wa
chama hicho na mjumbe mmoja kutoka mkoa wa Arusha, Mrisho Gamba,
alikiambia kikao cha Baraza Kuu la UVCCM, mjini Dodoma hivi karibuni
kwamba hakuna sababu ya ‘kuuma maneno’ kuhusu hilo.

Kauli hiyo ya Gambo ambayo imeelezwa kuungwa mkono na vijana wengi na
hata baadhi ya wazee kutoka bara na visiwani, imeelezwa kujikita katika
vichwa vya baadhi ya wajumbe wakiwamo viongozi wastaafu.

“Utashangaa kuona kwamba hiyo ajenda inaungwa mkono na wazee ambao
huwezi kuamini, japo nao wanapingana na baadhi ya hoja zilizotolewa na
UVCCM, lakini hilo la kutoswa mafisadi halina mjadala,” alisema
kiongozi mmoja wa UVCCM.

Habari zinaeleza kwamba Rais Kikwete amekuwa makini katika kukubaliana
na mkakati huo wa ‘kujivua gamba’ kutokana na “sababu za kisiasa na
kiusalama” kuepuka mpango huo kutumika vibaya kumjengea maadui ama
kuwaingiza watu ambao hawahusiki na kashfa zozote bali wamekuwa
wakiisaidia CCM ionekane nayo si chama cha mafisadi.

“Rais anakwepa watu wasioitakia CCM mema kutumia nafasi ya kujivua
gamba kuwahujumu viongozi ambao wamekuwa mstari wa mbele katika
kupambana na ufisadi na hivyo kukifanya chama chetu kujitenga na
watuhumiwa wa ufisadi walio ndani ya chama chetu,” anasema mjumbe wa
NEC kutoka Zanzibar.

Imeelezwa kwamba wajumbe wa Zanzibar wataweka wazi kuhusu kuutaka
uongozi wa juu wa CCM kuchukua hatua dhidi ya watu ambao wamesababisha
chama hicho kupoteza baadhi ya majimbo na hata kupungua kura za mgombea
urais wa CCM.

“Kuna watu ambao wamesababisha wapinzani na hasa CHADEMA kupata ajenda.
Walisababisha Mwenyekiti wetu akasirikiwe na watu kwa kuwanadi. Watu
kama hao si wa kuachwa, ni lazima watoswe,” anasema mjumbe huyo wa
Zanzibar kwa sharti la kutotajwa.

Mbali ya kushughulikia watuhumiwa wa ufisadi, imeelezwa kwamba vijana
ndani ya UVCCM ambao wameelezwa kupingana na dhana ya kujivua gamba nao
watashughulikiwa kwa maelezo kwamba itakua ni hatari kwa vijana kuanza
kutumika.

Kundi hilo la mafisadi ndani ya CCM sasa linadaiwa kufadhili mapinduzi
baridi yenye lengo la kumwengua Kikwete kama Mwenyekiti wa Taifa wa
CCM.

"Mtandao huu wa mafisadi unataka kugeuza kauli ya Rais Kikwete
mwenyewe ya kuleta mabadiliko kwenye chama kwa kumuengua kama kiongozi
wa chama," alisema mjume mmoja wa NEC ya CCM.

"Wajumbe kadhaa wamepangwa kuleta hoja kwenye vikao vya Kamati Kuu na
NEC kuwa ni bora Rais Kikwete aachie nafasi yake ya Mwenyekiti wa
Taifa wa CCM ili aweze kupata muda mwingi zaidi kushughulikia matatizo
ya taifa kama Rais."

Inadaiwa kuwa kundi hilo la mafisadi linatembeza pesa nyingi kwa
wajumbe wa NEC, Kamati Kuu na Mkutano Kuu wa chama ili kufanikisha
mapinduzi hayo.

"Pia baadhi ya wazee maarufu wa chama wako kwenye listi ya watu
watakaopewa rushwa ili kuunga mkono mapinguzi haya baridi," alisema
kada mmoja wa CCM.

"Ni mkakati mpana sana umepangwa. Watadai kuwa mabadiliko hayo ni kwa
nia njema ili Rais apumzike na majukumu ya chama na badala yake
ateuliwe kiongozi waliompanga ili awe mwenyekiti wa CCM na hivyo basi
Rais wa 2015."

Vyanzo vyetu ndani ya CCM vinasema kuwa wanachama wengi wanapendelea
kuwa Katibu Mkuu wa chama tawala, Yusuf Makamba, ang'atuke ili
apatikane kiongozi mwingine atakayeleta ufanisi zaidi.

Taarifa zinadai kuwa kuna baadhi ya makada wa siku nyingi wa CCM
tayari wamemshauri Makamba kusoma alama za nyakati na kujiuzulu yeye
mwenyewe.

Wajumbe kadhaa wa UVCCM wameweka bayana kuwa ni lazima mafisadi
watimuliwe kwenye chama na Makamba astaafu ili kuleta uhai mpya kwenye
chama kuelekea 2015.

(Source: KULIKONI, Aprili 8, 2011)
 
Back
Top Bottom