Jamani eeh.. Greath THinkers... Naona mada imekuwa stori za kijiweni.. Kwanini tusijaribu ku-analyse sababu za JK kufanya hivi. Ndio tunafahamu kuwa alisema anatoa 'gamba' lakini je madhumuni hasilia ni nini...? Je nguvu ambayo upinzani umeipata na haswa CDM ndio umemtishia kupatwa na yale ya KANU? au ni mambo yaliyotokea bondeni kwa MADIBA hapo... ANC overthrow of Mbeki by ZUMA... Je Kikwete anarespond to Lowassa's attempts to take control of CCM's decision making bodies so that he could secure his presidential nomination 2015? Ama ni nini? Kwa hakika kesho majina mapya yatakapo pendekezwa ndipo nia na madhumuni yatajulikana.... Swali la kwanza ni je EL atarudi? tunajua kabisa RA ndio basi (at least in hatokuwepo jikoni directily), je wale wanaojiita wapiganaji kina Kilango, Mwakyembe n.k wataingia? je JK atawapoteza viongozi wengine waliochafuka kama Chenge (most likely in my opinion), na Je atataka kuwadhibiti wale ambao wako kambi ya Lowassa (makinda, et al.) na je wale wengine wanao imezea mate 2015 kama Samwel Sitta watatupiliwa choo cha shimo au ? Ingekuwa vizuri jukwaa la GREAT thinkers likawa mstari wa mbele kuchambua mambo haya kwakua yanatabiri hali ya nchi yetu katika siku za usoni itakuaje... tupunguze ushabiki na uchama katika haya... Nimejaribu kuangalia mawazo mbali mbali tuliyochangia humu nimeona yapo mawazo yamsingi lakini pia ushabiki mwingi (mara ccm wafe tuu..atakama wafe sawa vizuri labda, lakini tunaomba uchambuzi tafadhali...jukwaa hili lirudie hali yake ya miaka ya nyuma.) UCHAmbuzi MAKINI tafadhali jamani.
KK
Wana CCM naomba mnisaidie, maana naona kuna watu wanaweza kuwa wanashangilia mafisadi kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya Chama na kumbe uvuliwaji huo umefanyika kimakosa.
Kulingana na Katiba ya CCM ni nani au kikao gani chenye maamuzi ya kumvua kiongozi wa CCM uongozi kwenye ngazi ya Kamati Kuu au NEC?
Chenge alikuwa Mjumbe wa CC kwa kigezo kwamba alipata kura nyingi kwenye uchaguzi wa wajumbe wa NEC kupitia vile viti 20 vya Bara. Je, replacement yake itafanyika vipi?
RA aliingia kwenye CC kwa njia ipi? AU ndio wale wateule wachache wa Mwenyekiti?
Kama Kamati Kuu imevunjwa, je ilivunjwa baada ya kuwavua uongozi hao watuhumiwa?
Mantiki ya kuvunja CC iko wapi? Maana wajumbe wengi wanaingia huko kwa Nyadhifa zao mfano, wenyeviti wote wa Jumuiya za Chama, Spika, Makamu Mwenyekiti Bara na Visiwani, Katibu Mkuu, nadhani na manaibu wake wa Bara na Visiwani. Waliobaki wengine akina Mkapa, Mwinyi na wengineo kibao wanaingia kwa kuwa walishawahi kuwa viongozi wa kitaifa wa CCM.
Je, kuvunja CC sasa hivi ina maana kwamba Kikwete ataleta sura mpya ndani ya CC? Atazipataje na ilihali uchaguzi wa CCM ni mwakani?
Hapo sioni kama JK ametatua mgogoro wa CCM, tatizo siyo Lowassa, RA na Chenge, tatizo ni kundi zima lililo nyuma ya hao mafisadi na hao ndio wamekuwa vinara wa kuongoza utetezi dhidi ya mafisadi na hao ndio waliojaa kwenye NEC. Ngoja tusubiri kesho.
Kama NEC ikibariki hayo maamuzi, basi tusubiri vita kuu ndani ya CCM, hakuna atakayepona. Vita vya panzi ni furaha ya kunguru, wapinzani kazeni buti Ikulu inazidi kuwa wazi na hili limetokea kipindi kizuri sana, inawezekana kabisa wabunge wa CCM wanaweza kuungana na wabunge wa upinzani kuupinga mswaada wa Katiba Mpya, maana hawajui kesho watakuwa wapi.
Kikwete aliingia madarakani kwa siasa za makundi akisaidiwa na ufisadi wa EPA ambao ulimpa fedha za kampeni. Ni makundi hayo hayo na ufisadi huo huo ndio ambao utasababisha CCM imfie mikononi mwake.
Jamani eeh.. Greath THinkers... Naona mada imekuwa stori za kijiweni.. Kwanini tusijaribu ku-analyse sababu za JK kufanya hivi. Ndio tunafahamu kuwa alisema anatoa 'gamba' lakini je madhumuni hasilia ni nini...? Je nguvu ambayo upinzani umeipata na haswa CDM ndio umemtishia kupatwa na yale ya KANU? au ni mambo yaliyotokea bondeni kwa MADIBA hapo... ANC overthrow of Mbeki by ZUMA... Je Kikwete anarespond to Lowassa's attempts to take control of CCM's decision making bodies so that he could secure his presidential nomination 2015? Ama ni nini? Kwa hakika kesho majina mapya yatakapo pendekezwa ndipo nia na madhumuni yatajulikana.... Swali la kwanza ni je EL atarudi? tunajua kabisa RA ndio basi (at least in hatokuwepo jikoni directily), je wale wanaojiita wapiganaji kina Kilango, Mwakyembe n.k wataingia? je JK atawapoteza viongozi wengine waliochafuka kama Chenge (most likely in my opinion), na Je atataka kuwadhibiti wale ambao wako kambi ya Lowassa (makinda, et al.) na je wale wengine wanao imezea mate 2015 kama Samwel Sitta watatupiliwa choo cha shimo au ? Ingekuwa vizuri jukwaa la GREAT thinkers likawa mstari wa mbele kuchambua mambo haya kwakua yanatabiri hali ya nchi yetu katika siku za usoni itakuaje... tupunguze ushabiki na uchama katika haya... Nimejaribu kuangalia mawazo mbali mbali tuliyochangia humu nimeona yapo mawazo yamsingi lakini pia ushabiki mwingi (mara ccm wafe tuu..atakama wafe sawa vizuri labda, lakini tunaomba uchambuzi tafadhali...jukwaa hili lirudie hali yake ya miaka ya nyuma.) UCHAmbuzi MAKINI tafadhali jamani.
KK
Wacha, inamaana hujui kuwa kamati ya mzee Mwinyi imeshatoa majibu? Unaweza kujiliza kwanini Mwakyembe na Sitta wamepelekwa serikalini? Kwanini CCM wamebadilisha Spika? Na kwanini leo hii kina RA, Makamba na EL wanang'oka. Ulitegemea jibu la moja kwa moja?Msipoteze usingizi wenu kusubiri ati habari kutoka Idodomia, mafisadi wataendelea kula tu kwa sababu fisadi papa aliyeiba kura bado yupo ni sawa na kufikiri Ngamia atapita kwenye tundu la sindano. Hawawezi kubadilika hawa kwa sababu wamekwisha kula damu ya walipa kodi. Dawa yao ni kuwang'oa tu wapende wasipende. Hizi zote ni zuga zuga zao tu. Na ushahidi wa zuga yenyewe waulizeni ile kamati waliyomkabidhi Mzee Rukhsa kuishughulikia imefika wapi?
Mkishituka mtasikia Dowans wamekwishalipwa na mambo yanendelea kama kawaida.
Wana CCM naomba mnisaidie, maana naona kuna watu wanaweza kuwa wanashangilia mafisadi kuvuliwa nyadhifa zao ndani ya Chama na kumbe uvuliwaji huo umefanyika kimakosa.
Kulingana na Katiba ya CCM ni nani au kikao gani chenye maamuzi ya kumvua kiongozi wa CCM uongozi kwenye ngazi ya Kamati Kuu au NEC?
where's field marshall es when you need him?!
Kuna wengine humu kazi yao kuchungulia kuna users wangapi online na wanapost kwa mbwembwe, na wengine sio great thinkers but great suckers! Hiki kijiwe cha chadema kikiendelea hivi haya ya Dodoma yatatokea CDM hivi karibuni. FUTURE haionekani kwa macho yenye miwani bali macho ya KI-FIKRA.
mbona yupo anachungulia tu, zile kamba zake zimekatwa sasa atawezaje kuleta habari?
Mbona yupo anachungulia tu, zile kamba zake zimekatwa sasa atawezaje kuleta habari?
21. Kumsimamisha Mwenyekiti wa CCM au Makamu Mwenyekiti wa CCM iwapo mwenendo na utendaji wake wa kazi vinamwondolea sifa za uongozi. Hata hivyo Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itafikisha mapendekezo yake mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM wa Taifa kwa uamuzi wa mwisho.
22. Kumwachisha au kumfukuza Uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake
wa mwisho ulifanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa.
Kumsimamisha uongozi kiongozi yeyote isipokuwa Mwenyekiti wa CCM na
Makamu wa Mwenyekiti wa CCM endapo itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uongozi.
I think it is a bit too late. The CCM ship is sinking.Natofautiana na wewe mkuu, nadhani kama hatawarudisha mafisadi wanaweza kujiokoa
tatizo la ccm siyo lowasa,ra na mafisadi wengine waliojaa huko. tatizo ni mfumo ambao umekigeuza hicho chama kuwa chama dola! bila kupambana na huo mfumo ccm haiwezi safishika. na wala haitafishika ikiwa madarakani. tutakapowaondoa hawa watu madarakani ndipo watapata muda wa kujisafisha.maana wengi wa viongozi wao ambao wako huko ili kupata pesa na madaraka watawakimbia pindi chama kitakapoondolewa madarakani.kwamba eti mwenyekiti wao anaweza fanya mageuzi ya maana hizo ni ndoto za mchana.
Bullshit.lowassa ndiye rais 2015 full stop! Ni makini jasiri na mchapa kazi. Si kama huyo anayejiita matoto wa mkulima.
Siku ya kufa nyani miti yote huteleza.
Kama wadau wengi walivyochangia hapa tatizo si hao watatu RA, EL na Chenge, bali mfumo uliowaingiza hadi kujiona wako ndani ya peace of heaven. Wakati umelishwa na kukua halafu huyo yaya unamtema wakati ameshajua siri na madhaifu yako, siku atakapoyaibua utaomba inchi ifunuke ikufiche.
Kwa tafsiri rahisi Mwenyekiti hajatumia busara kwa muda mrefu na sasa ni zima moto tu na kwa aliyofanya ni dhahiri ameongeza crack ndani ya chama kuwa makundi mawili ingawa hayaonikani kimfumo bali kinadharia.
Huu utaratibu wa rais na mwenyekiti kutaka wenye madaraka wafanye kama robot si rahisi maana hata robotical incording system inahitaji programmer specialist. Wasifu wa Rais Kikwete ni kukaa ikulu kila kitu kitajiendesha chenyewe kwa kuwa tumeweka watu, yeye mguu majuu kukagua mahoteli bora duniani.
Kazi kwelikweli.
Technically speaking,but it's the president who did that,I've no doubt about it.Katiba ya Chama cha Mapinduzi inasema wazi kuwa majukumu ya kuleta nidhamu yako kwa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC)katika ngazi mbalimbali za uongozi kitaifa. Katiba hiyo inasema hivi (Ibara ya 107 inayoshughulikia na Kazi za Halmashauri Kuu ya Taifa):
Kwa hiyo kwa vifungu hivyo viwili tu tunaweza kuona kuwa NEC inaweza kufanya mambo mbalimbali ikiwemo "kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake uifanywa na NEC".
Ibara ya 109 inaweka mojawapo ya mjukumu ya Kamati Kuu ya Taifa ni:
Halafu inabidi tuangalie kuwa Sekretariati ya CCM wajumbe wake wote wanaingia kutoka na nyadhifa zao. Hii ina maana hakuna ambaye anaingia kwa kuteuliwa na Mwenyekiti. Mwenyekiti wa CCM Taifa hana madaraka ya kumuondoa au kumsimamisha kiongozi yeyote wa CCM. Hata kama Mwenyekiti huyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hii ina maana gani?
Ina maana ya kwamba lolote lililofanyika Dodoma litakuwa ni tendo la Kamati Kuu au Halmashauri Kuu ya Taifa. Tukumbuke kuwa Mwenyekiti ana kura ya turufu pale tu endapo kura za wajumbe zinalingana katika vikao visivyo husiana na vya uchaguzi - kwani huko ana kura moja.
Ina maana:
a. JK hakuvunja Sekretariati ya Halmashauri Kuu kwani hana madaraka hayo
b. JK hakuvunja Kamati Kuu kwani hana madaraka hayo
c. JK hakumuondoa mtu yeyote uongozi
Hii ina maana kuwa lolote lililotokea Dodoma limetokana na NEC au CC; na hii ina maana ya kwamba wale watu waliokuwa wanaonekana ni vigogo kweli na wana influence ndani ya Chama inawezekana hawana influence ambayo walidhania wanayo. The only x-factor katika hili lote ni kuwa Mwenyekiti wa CCM ndiye Rais vile vile na Katiba ya CCM haitoi maelekezo ya M/Kiti atumie madaraka yake vipi endapo ndiye Rais? Hivyo kama hana nguvu fulani kama mwenyekiti anaweza kutumia madaraka ya Urais kutimiza mambo mbalimbali.
Na hicho ndicho ambavyo kitakuwa kimetokea.
Hasira za mkizi.Kuna wengine humu kazi yao kuchungulia kuna users wangapi online na wanapost kwa mbwembwe, na wengine sio great thinkers but great suckers! Hiki kijiwe cha chadema kikiendelea hivi haya ya Dodoma yatatokea CDM hivi karibuni. FUTURE haionekani kwa macho yenye miwani bali macho ya KI-FIKRA.
Ajenda ya mswada wa mabadiliko ya katiba ndo ajenda kuu hatuiachi hiyo ndo ya muhimu kuliko hayo ya CCM, acha wafu wazike wafu waodu chadema cjui watakuja na ajenda gani!