NetMaster
JF-Expert Member
- Sep 12, 2022
- 1,454
- 4,854
MUHIMU: Ndugu wa karibu awe ni bibi (mama yako) au shangazi (dada yako) unaemwamini.
Kulazimisha mtoto aje kuishi kwako wakati unaishi na mwanamke mwengine ni kumuingiza mtoto huyo uliemleta kwenye tanuri la moto, hii ni nature ndivyo tulivyoumbwa.
Tena hali itakuwa mbaya sana mtoto uliemleta akiwa amewazidi watoto wa mama wa kambo akili, afya, bidii, n.k.
Wanaume tuache mambo ya ubabe wa kuchukua watoto waje kuishi na mama wa kambo, ni heri waende kuishi kwa ndugu zako wa karibu tena ni wale wa familia kabisa sio ilimradi tu ndugu, awe ni bibi (mama yako) au shangazi (dada zako), Ma Shangazi wanaweza kuishi na watoto wa kaka zao ila sio baba mdogo au mkubwa hawa huwa wake zao vipengele.
Mifano ya mateso niliyowahi shuhudia kwa watoto wa kambo niliosoma nao.
kunyimwa chakula kwa maksudi, mama wa kambo anapika chakula cha watoto wake tu, mtoto wa kambo mlo wa usiku tu.
mtoto kupewa kipigo cha mtu mzima (wengine mpaka kifo), kuna rafiki yangu aliwahi kupigwa na stuli kichwani kwa kosa dogo tu, ilipelekea atokwe na nundu kichwani, hizi bakora kachezea sana.
Kufitinisha watoto wake na mtoto wa kambo, mfano watoto wake wanaweza kwenda kucheza na wenzao ila mtoto wa kambo anabanwa ndani
N.k. haya yote yanapotokea mtoto wa kambo anapigwa biti asije kumwambia baba yake kinachoendelea lasivyo atakiona cha moto, baba unarudi unadhani hali ipo sawa ila kivumbi kinaanza ukiondoka tu.
Ushauri kwa wanaume tuwe makini sana kwa wanawake tunaolala nao, kama unaona mwanamke unaelala nae hawezi kuwa mama bora hakikisha unavaa condom na kama huwezi kuvaa tafuta ambae unaona ataweza kuishi na mtoto wenu.