Wivu wa wanaume kwenye ndoa ni sababu ya wake zao kuhamisha mapenzi kwa watoto

Pamba Anord

New Member
Nov 25, 2023
4
8
Wanaume wengi hawaelewi uhusiano uliopo kati ya mke wake na watoto wako (mama na mtoto), na hivyo huwaonea wivu wake zao baada ya kujifungua .(kupata mtoto)

Watu wanapooana, miezi ya mwanzoni huona ndoa kuwa tamu sana ila sababu za ugomvi mwingi katika ndoa ni pale mtoto anapopatikana, wanaume wengi huwa na wivu kwa wake zao.

Huona mke wake anatoa muda mwingi kwa mtoto na siyo kwake kama ilivyokuwa zamani kipindi hawana mtoto (mahaba yanapungua). Anakuwa anataka kushindana na mtoto sasa, yaani anajihisi kuwa hathaminiki tena!

Anakuwa na wivu, yaani anakuwa anapenda majukumu ya kuwa mume ila kukubali kuwa yeye sasa ni baba pia inakuwa ngumu!

Utafiti wa Mwanasaikolojia Daniel Stern unaonesha kuwa, asilimia kubwa ya wanume huwaonea wivu watoto wao na wengi wao huwa hawasemi ila huumia ndani kwa ndani na kumaliza hasira zao kwa kuwafokea wake zao kuwabembeleza watoto usiku wanapolia au hata kukataa kuwabeba watoto wao.
 
Back
Top Bottom