Mama wa kambo hawezi kuwalea sawa watoto wake na wa mwengine, tuwaache watoto waishi na mama zao ama kwa ndugu wa karibu ila sio vinginevyo

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
MUHIMU: Ndugu wa karibu awe ni bibi (mama yako) au shangazi (dada yako) unaemwamini.

Kulazimisha mtoto aje kuishi kwako wakati unaishi na mwanamke mwengine ni kumuingiza mtoto huyo uliemleta kwenye tanuri la moto, hii ni nature ndivyo tulivyoumbwa.

Tena hali itakuwa mbaya sana mtoto uliemleta akiwa amewazidi watoto wa mama wa kambo akili, afya, bidii, n.k.

Wanaume tuache mambo ya ubabe wa kuchukua watoto waje kuishi na mama wa kambo, ni heri waende kuishi kwa ndugu zako wa karibu tena ni wale wa familia kabisa sio ilimradi tu ndugu, awe ni bibi (mama yako) au shangazi (dada zako), Ma Shangazi wanaweza kuishi na watoto wa kaka zao ila sio baba mdogo au mkubwa hawa huwa wake zao vipengele.

Mifano ya mateso niliyowahi shuhudia kwa watoto wa kambo niliosoma nao.

kunyimwa chakula kwa maksudi, mama wa kambo anapika chakula cha watoto wake tu, mtoto wa kambo mlo wa usiku tu.

mtoto kupewa kipigo cha mtu mzima (wengine mpaka kifo), kuna rafiki yangu aliwahi kupigwa na stuli kichwani kwa kosa dogo tu, ilipelekea atokwe na nundu kichwani, hizi bakora kachezea sana.

Kufitinisha watoto wake na mtoto wa kambo, mfano watoto wake wanaweza kwenda kucheza na wenzao ila mtoto wa kambo anabanwa ndani

N.k. haya yote yanapotokea mtoto wa kambo anapigwa biti asije kumwambia baba yake kinachoendelea lasivyo atakiona cha moto, baba unarudi unadhani hali ipo sawa ila kivumbi kinaanza ukiondoka tu.

Ushauri kwa wanaume tuwe makini sana kwa wanawake tunaolala nao, kama unaona mwanamke unaelala nae hawezi kuwa mama bora hakikisha unavaa condom na kama huwezi kuvaa tafuta ambae unaona ataweza kuishi na mtoto wenu.
 
Kulazimisha mtoto aje kuishi kwako wakati unaishi na mwanamke mwengine ni kumuingiza mtoto huyo uliemleta kwenye tanuri la moto, hii ni nature ndivyo tulivyoumbwa.

Tena hali itakuwa mbaya sana mtoto uliemleta akiwa amewazidi watoto wa mama wa kambo akili, afya, bidii, n.k.

Wanaume tuache mambo ya ubabe wa kuchukua watoto waje kuishi na mama wa kambo, ni heri waende kuishi ndugu zako wa karibu kama wazazi wako, dada zako, n.k.
Nakazia, na tunawafinya haswa
 
IMG_4403.jpg
 
Mtoto kama mama yake yupo aishi na mama yake labda awe amefariki na bibi yake hayupo
Sio tu mama wa kambo wabaya pia hata ndugu hawawezi ishi na mtoto wa ndugu nikuambie tabu ipo pale pale
Yani ndio maana nimekazia kwenye ndugu hapo iwe tu ni wanafamilia wa karibu kwa mama yako mzazi ama dada zako auu wadogo zako wa kike,,, kwa upande wa wanafamilia wa kiume nao wakiwa na wake zao inakuwa stori ile ile.
 
Ma Shangazi wanaweza kuishi na watoto wa kaka zao ila sio baba mdogo au mkubwa hawa huwa wake zao vipengele.
Hii kitu nimeshuhudia kwa macho yangu mwenyewe, nikiwa shule ya msingi niliwahi kwenda likizo kwa mashangazi watatu vipindi tofauti, nili enjoy sana... Hali ilikuwa tofauti nikienda kwa kina ba mkubwa na ba mdogo, yani wakiwepo labda ndio wake zao wanazuga kuwa wakarimu lakini wakiondoka kwenda makazini wake zao wanakuchulia poa tu.
 
Wewe umeshuhudia ila mie nimekulia kwenye hayo mazingira, bi mkubwa alikuwa mnafiki na mchoyo isipokuwa mda mzee yupo ndio anazuga kama anakupenda au wageni wakija. Ila wakishaondoka ni stress mwanzo kati na mwisho.

Kuna mshangazi unamtesa kinoma mtoto wa mdogo wake. Mshangazi ule wa kichaga umejaaliwa roho ya upendo wa kutoa tunda kwa vijana wadogo lakini anakosa upendo kwa mtoto wa mdogo wake.
Huyo shangazi mchaga chenga roho mbaya tu, mie nina bahati ya mashangazi wazungu wa roho tu. Sijaona kipengele kwa mashangazi 😀😀😀
 
NDUGU?! 😳😳😳😳😳😳

HAPANA!... sishauri mtoto kulelewa na ndugu... kuna uzi humu uliwahi kufunguliwa unahusisha watu kutoa experience zao za kuishi kwa ndugu. Soma yaliyomo ndugu mleta mada alafu utapata kuwafahamu ndugu vizuri.
 
Wewe umeshuhudia ila mie nimekulia kwenye hayo mazingira, bi mkubwa alikuwa mnafiki na mchoyo isipokuwa mda mzee yupo ndio anazuga kama anakupenda au wageni wakija. Ila wakishaondoka ni stress mwanzo kati na mwisho.
Bi mkubwa hapo alikuwa mama wa kambo au mke wa bamdogo / bamkubwa au ?
 
Back
Top Bottom