KILICHONIJIA FIKIRANI NILIPOSOMA HII
Kitendo cha kuja kumsifia mwanamke mwingine wa mume wako, ukae ukijua ana jambo anataka litimie ila hawezi kutumia lugha ya moja kwa moja kulifikisha. Anahitaji mwanae arejee kwa mzazi mwenzie, kusifia huko anajaribu mwanae aone wema wa binti yule arudishe moyo nyuma. Sidhani mtu mzima kama huyo asitambue alama za nyakati, wala mahali pa kuchunga ulimi wake kwani aliolewa anajua mbivu na mbichi.
Hawezi kumshawishi moja kwa moja, kwani yupo ndani ya ndoa yenye amani na pia mwanae ni mtu mzima. Anachokifanya hapo ni kukunyima amani ya ndoa, kupitia maneno yake ya kuudhi. Ukiathiriwa na maneno yake basi kinachofuata ni kutokuwa na hamu na jamaa, naye atakinai penzi lako.
Ukose hamu ya kuwa na mumeo, mwishowe uje kukinaiwa na mume wako. Huu ni mwanzo wa huyo mama kuwakutanisha karibu, ninaweza nikawa nipo tofauti kifikra maana Mwanadamu daima hawezi kuwa sahihi. Ila jaribu kufikiria ukaribu wa huyo mzazi mwenzie mumeo na mkwe wake, jumuisha na hizo sifa za kumsifia, ongezea na hayo maneno yake ya kukuudhi utajua nilichokifikiria ni kipi.
Hapo ndipo ndoa yako itaingia shimoni, unapaswa uamue maamuzi ya busara zaidi. Kosa moja unaweza kuwafanya wanao wadogo wakose malezi ya wazazi wote, tumia busara mume asichukie wala ndugu zake. Anza kushinda nguvu za maneno yake, ukikubali uathiriwe nayo utaingia pabaya, ndiyo ulitatue hilo kwa ustarabu wa hali ya juu bila kuacha ugomvi kwa shemeji na ndugu wengine wala mumeo. Akibaki na chuki zake ni yeye tu,