Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Nimebahatika kutembelewa na mkwe wangu wiki kadhaa sasa,nilifurahi nikashukuru kwa kupata ugeni mzito ukizingatia kwamba nakaa na shemeji zangu hapa,mmoja anatafuta kazi mwingine yupo chuo anakaa hostel ila huwa anarudi hasa weekend.
Tabia ambazo amenionyesha na hakika niseme wazi tu kua zinanikera na kuukwaza moyo wangu na Mara hii naanza kujihisi unyonge sana ndani ya nyumba yangu
Huyu mwenzangu alizaaga mtoto kipindi cha nyuma huko katika pita pita za ujana na huyu mtoto yupo kwa mama Yake na anasoma boarding school na kila kitu kinalipiwa na baba yake hapa nami wala sina tatizo na hilo,sasa tangu mama mkwe aje akikaa na mwanae hadithi ni kumzungumzia huyo mama wa mtoto wee na kibaya zaidi anasema wazi kabisaa kua huwa anakwenda kumuona na kukaa hapo kwake yaani kwao na mumeo wangu,yaani anamsifu kabisaa kuwa anasaidia sana na
Pole sana na mitihani,ila hata kwenye familia zetu watu kama hao pia wapo,tujifunze kuwastahmilia wakwe zetu sisemi kua anachofanya ni sawa ila jitahidi sana kwani simkaaji hapo mda mwingi, akiongelea kuhusu mwanamke mwengine ni bora zaidi yako wala usimuonyeshe umekasirika mwanamke tumepewa kipaji chakuhimili mengi moyoni,
Nashukuru Mungu mkwe wangu tunaelewana SANAAAA,utakapo mwambia mumeo mama arudi kijijini italeta picha mbaya kua humpendi muombe sana mwenyezi mungu azidi kukupa moyo wa subra,kwenye Ndoa hua na mitihani ya kila aina...
 
Please, keep in mind pia, not all the time ntasacrifice furaha yangu kisa mama yako, Hell No. Kila mtu ana level ya Uvumilivu ambayo anytime inaweza kuexpire. Sasa sio kina mama wakwe waharibu ndoa zetu tuwangalie tu kisa ni mama wa mume, hapana kwa kweli. Na wenyewe wawe na utu na sisi pia, wanavyotutreat sisi ndo wanavyowish mabinti zao wawe treated na wakwe zao huko walipoolewa?. Uvumilivu uwe wa pande zote mbili, kwa sababu wote tuna mapungufu. Mimi siwezi kulingana na mama yake, na mama yake hawezi kulingana na mimi pia, so kila mtu ajue nafasi yake na mipaka yake ni ipi, then tugawane ustaarabu. And yes wapo wanaume ambao wanasimamia ukweli daima, mama akikosea anaambiwa na mke ukikosea unaambiwa tu, sio tu muda wote achekewe kisa ni mama while analeta uharibifu. Mama ana umuhimu wake, na mke ana umuhimu wake pia.
Ameeeeen!
 
Ukweli mchungu ni kwamba kuna wamama wengi tu wanawish watoto wao wa kiume labda wangezaaga tu huko nje bila kuoa afu wawaletee watoto waishi pamoja (mama, mtoto na wajukuu) mali za kijana wake zisiende mbali eti mweeh. Wewe unatamani uishi milele na mwanao, hao wajukuu zako hawatamani kuishi na mama zao? Ubinafsi tu na roho za kimaskini
Basi wawazuie watoto wao kuoa na kuzaa pia.
 
Hlf ajabu moja mbona mamako wewe haji kumkera yeye.... cjaelewaga hii makitu ya mama wa mwanaume kukiona ana rights za kufanya atakavyo... mfyuuu zao
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Nimecheka hapo ulivyomalizia.
 
Huku unalofanya unapunguza tu stress LA Msingi ongea Na Mumeo achague moja kumweleza mama ake anachotakiwa kufanya ikiwezekana aondoke ama mshauriane otherwise
 
Haha na usemi wao "mimi ndo mama ake, nimembeba tumboni miezi 9, sijui nimemsomesha kwa tabu, hapa ni kwa mwanangu na mali za mwanangu" woiii. Mtu anakazania nimemsomesha kwa tabu, sasa sijui alitaka mke ukutane na mumeo akiwa mdogo uchangie kumsomesha pia ili uwe na right juu ya mumeo pia? Na akifika kwa mwanae afanye anavyotaka bila kuulizwa so far mali zote ni za mwanae (they wish), Yani mke unaonekana kama kizuizi cha wao kuenjoy na watoto wao. Nafikiri from tunavyoanza kulea watoto wetu, let us prepare ourselves mentally/psychologically and spiritually kwamba watoto tunaowalea, siku moja hawatokuwa watoto wetu tu, bali watakuwa waume na wababa kwa watoto wao. We can't ignore their sacrifices and tunawashukuru milele wametuzalia na kutulelea waume na baba bora kwa wanetu, but watuache na sisi basi tuplay part zetu kwenye maisha ya watoto wao peacefully. It's too much, Abeg
Alimbeba tumboni kwani mke alibebwa mgongoni!! Na mama za wakwe wakianza kutetea watoto wao patakalika!!!

Yeye mbona aliacha wazazi wake akaambatana na mumewe,mbona hakuambatana na mamaye?
Watoto wao nao ni tatizo, pale wanaporuhusu mama zao waongoze ndoa zao,hapo mke anakuwa na waume wawili(of which haiwezekani).
 
huchepuki kweli?kama mume nyonga mbovu maanake haki yako ya msingi unakosa..
kuwa na busara na uvumilivu wa kutosha biblia imenena "mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe" sijajua ww dini gani ila Mungu wa waislamu na wakristo ni mmoja na mafunzo yale yale hata kama yanatofautiana kidogo.. huwezi mridhisha binadamu asilimia mia moja utakosea mara moja asilimia 99 ya mema yote huondoka na husahau..Ongea na mumeo mwambie nae upate sikiliza mtazamo wake ukoje na kama unaendana na wa mamake basi inabidi umuweke sawa ndipo ataweza ongea na mamake.
Haya mafundisho its about time na mama wakwe wapewe kwakweli.
 
Alimbeba tumboni kwani mke alibebwa mgongoni!! Na mama za wakwe wakianza kutetea watoto wao patakalika!!!

Yeye mbona aliacha wazazi wake akaambatana na mumewe,mbona hakuambatana na mamaye?
Watoto wao nao ni tatizo, pale wanaporuhusu mama zao waongoze ndoa zao,hapo mke anakuwa na waume wawili(of which haiwezekani).
I can't imagine mama za mabinti nao siku moja waanze kutetea mabinti zao. Kwa sababu hata na wao wamezaa na kuwasomesha kwa shida binti zao so wana haki ya kuenjoy matunda ya jasho la watoto wao. Na yeye akija kwangu awe tu na authority kwa sababu ni kwa mwanae. Hapana jamani, em tumuombe Mungu atupe hekima na busara za kudeal na hizi changamoto. Maana tukisema tuanze kukomeshana itakuwa tafrani
 
Hawa wakuitwa wakwe hawabebeki hawakosi sababu hawana shukrani Kama jipu la kwapa.
 
I can't imagine mama za mabinti nao siku moja waanze kutetea mabinti zao. Kwa sababu hata na wao wamezaa na kuwasomesha kwa shida binti zao so wana haki ya kuenjoy matunda ya jasho la watoto wao. Na yeye akija kwangu awe tu na authority kwa sababu ni kwa mwanae. Hapana jamani, em tumuombe Mungu atupe hekima na busara za kudeal na hizi changamoto. Maana tukisema tuanze kukomeshana itakuwa tafrani
Amen.
 
Tuanze kupinga baadhi ya mila zinazobagua watu. Ni ajabu sana kuona mama wa mke wangu(mkwe wangu) kukataa kulala kwangu eti kwa vile mila hairuhusu yeye kuishi kwangu.

Hizi mila ndio zinaharibu mara nyingi. Mfano, mama mzazi akija kwetu anajisikia yupo kwake, ana authority kama vile ni nyumba yake, lakini mama wa mke akija anajihisi yupo ugenini, hana usemi wowote na akikaa siku mbili tu ndugu zake wanaanza kumsema aondoke.

Ni mila potofu ndio zimeleta haya.
 
Back
Top Bottom