Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Mama mkwe nakupenda sana ila bora uende

Pole sna my dear, mm mwenyewe naishi na mama mkwe ni shida tupu. Mama anajua kupelekeza mpaka mambo ya ndani anataka kuyajua, alafu sasa anamaindi sna msosi utamjazia sahani kubwa Na bado atakwambia niachie ukoko ole wako ujisahau uloweke sufuria utayutraaa ana maneno.

Ila ninacho mshukuru Mungu mume wangu anamsimamo anajua kumpasha mamaake akikosea wala hamuogopi bila msimamo wa huyu mume mbona ndoa ningeiona chungu
 
Sema vyovyote vile unavyojisikia kusema lakini si mama mkwe kuniongezea mwanamke mwingine kwenye ndoa yangu NEVER EVER,kuto kukua kwa mtoto wake si kibali cha yeye kukaa na kumzungumzia mama wa mtoto wa mume wangu,hapa anatuanzishia migogoro ambayo nikiichekea hakika ntakuja kujuta,Mimi sitafutwi kupendwa ndugu yangu naitafuta heshima na utukufu kwa Allah maana dunia hii huwezi pendwa na wote
Hhhhh hamna kingine ni wivu tu nakutokujiamini kunakokusumbua kwani huyo aliyezaa nae mumeo anaundugu na mkweo?? Jishushe ukae karibu na mkweo show her your better than her kww vitendo na kumjali mama wawatu si kuja humu ku complain always sisi wanaume likija conflict ya mama na mke tunaside na mama zetu jitafakari dadangu mana unataka vita ambayo huwezi kushinda.
 
Nimejitahidi Mkuu na nomejishusha sana,ila linapokuja suala la yeye kumzungumzia mwanamke mwingine wa mwanae ndani ya nyumba yangu hakika nakosauvumilivu,na kwa bahati mbaya Mimi huwa sina asili ya kulia lia labda ningekua hivyo ningekua naliia kupoza uchungu ninaousikia
Mweleze mtoto wako kuwa hujisikii vizuri kusikia mama yake akimuongelea X wake. Muulize kama mama yako angalikuja akaanza kusifia X wako (maana hajakutoa utandu) angejisikia vipi? Ila jaribu kumuignore huyo mama mkwe maana ndivyo walivyo. Akikutana na X wa mumeo anaanza kukusifia. Ni wanafiki sana mama zetu na mtoto wa kiume usiposimama kati ya mkeo na mama yako unaunywa wa chuya.
 
Kadri atakavyozidi kukaa ndiyo matatizo yatakavyozidi,na dakika utakayofungua kinywa chako mmeo kama si mwelewa atazusha zogo.
Ila mama bora aende tu
 
Pole sna my dear, mm mwenyewe naishi na mama mkwe ni shida tupu. Mama anajua kupelekeza mpaka mambo ya ndani anataka kuyajua, alafu sasa anamaindi sna msosi utamjazia sahani kubwa Na bado atakwambia niachie ukoko ole wako ujisahau uloweke sufuria utayutraaa ana maneno.

Ila ninacho mshukuru Mungu mume wangu anamsimamo anajua kumpasha mamaake akikosea wala hamuogopi bila msimamo wa huyu mume mbona ndoa ningeiona chungu
Hawa wa mama kwa kweli wanatakiwa kujua sisi ni wanawake kama wao, tunaumia pia binafsi naumia sana mtu mmoja aje kunivuruga !!?? Kwanini, mbona nimekaa na watoto zake wote watatu mume wangu na wadogo zake haikua hivi
 
Hhhhh hamna kingine ni wivu tu nakutokujiamini kunakokusumbua kwani huyo aliyezaa nae mumeo anaundugu na mkweo?? Jishushe ukae karibu na mkweo show her your better than her kww vitendo na kumjali mama wawatu si kuja humu ku complain always sisi wanaume likija conflict ya mama na mke tunaside na mama zetu jitafakari dadangu mana unataka vita ambayo huwezi kushinda.
Hahahaa nimekusikia ila muda mwingine bora vita vya makombora kuliko vita baridi,inaumiza sana
 
Tulisema hapa kwenye mada mojawapo, kwamba sio lazima umpikie mume wako. Delegate hizi kazi kwa mfanyakazi. Mfundishe kupika. Wakaja akina mama hapa wakasema kila siku lazima wao wapike na sio mdada wa kazi.

Kama kuna siku Mr. ana hamu ya kula kitu fulani au ukiwa free, basi pika lakini sio kujitesa kisa kupika. Mume anapokuwa kazini mchana, anapikiwa na nani? Tamaduni zingine bwana!!

Mimi hayo mambo kwenye nyumba yangu nilishayakataa. Akiwa nyumbani atapika, kama hayupo aliye nyumbani atapika. Unagombana na mama mke bure kwa kisa cha kutodelegate.
 
Pole mamy
Kama kaja kukaa kwa muda mvumilie tu, huyo ni kama mama yako sema kuna kweli wanaudhi... Ongea na mumeo kuhusu hiyo hali, we hata usiuumize kichwa kumfikiria huyo, jifanye hujasikia au jibu kwa utani unaofanana na ukweli ataelewa tuu...
 
[emoji17] [emoji17] pole sana dada mweka mr chinii muyajenge
 
Pole sana, huyu alikuwa na nia ya kukuudhi na labda umkoromee na hivyo kupata nafasi ya kumshawishi mwanae akuache kwa kumdharau mama yake na hivyo kumrudia huyo waliyezaa naye kabla.

Hongera kwa uvumilivu wa hali ya juu kuweza kujizuia kumsemea hovyo. Baadhi katika hali hiyo wangeamua liwalo na liwe na kuamua kuanzisha varangati la kufa mtu.

Nimebahatika kutembelewa na mkwe wangu wiki kadhaa sasa,nilifurahi nikashukuru kwa kupata ugeni mzito ukizingatia kwamba nakaa na shemeji zangu hapa,mmoja anatafuta kazi mwingine yupo chuo anakaa hostel ila huwa anarudi hasa weekend.
Tabia ambazo amenionyesha na hakika niseme wazi tu kua zinanikera na kuukwaza moyo wangu na Mara hii naanza kujihisi unyonge sana ndani ya nyumba yangu
Huyu mwenzangu alizaaga mtoto kipindi cha nyuma huko katika pita pita za ujana na huyu mtoto yupo kwa mama Yake na anasoma boarding school na kila kitu kinalipiwa na baba yake hapa nami wala sina tatizo na hilo,sasa tangu mama mkwe aje akikaa na mwanae hadithi ni kumzungumzia huyo mama wa mtoto wee na kibaya zaidi anasema wazi kabisaa kua huwa anakwenda kumuona na kukaa hapo kwake yaani kwao na mumeo wangu,yaani anamsifu kabisaa kuwa anasaidia sana na anamshukuru!!
Mbaya zaidi baba watoto baada ya ajali mbaya aliyoipata na kupata tatizo La nyonga yupo tu haendi kazini zaidi Zaidi akitoka huwa anakwenda dukani kwetu kusaidia biashara, Mimi hutoka asubuhi kwenda job na kurudi jioni,na kutokana na heka heka za foleni najikuta Mara nyingine nachelewa kufika nyumbani mpaka saa 12 ndio naingia ila kawaida yangu ni ile ile kua chakula cha jioni napika mwenyewe hata Dada wa kazi hapa anafahamu hilo,mama mkwe nikichelewa hiyo kurudi anaanza maneno kua "sasa watakula saa ngapi? mwanae si atachelewa kunywa dawa? Kwa namna hii atapona kweli?" Yaani ni maneno juu ya maneno yeye anamfikiria mwanae mtu mzima hawa wajukuu walio wadogo hawaoni!!? Nifanyeje sasa? Niache kazi ili nimuhudumie mwanae ale saa 12 jioni badala ya saa 2 usiku au??
Nimekosa Uhuru na hamu ya mume wangu kwa kweli maana hata chakula kiwapo mezani nikimpakulia mwanae anakadiria kwa kuuliza "mbona kidogo sana? Atashiba kweli?" Inamaana Mimi nampunja mwanae!!? Mimi nikiyekaa nae miaka yote hii na watoto wote hawa nimpunje mwanae chakula lol!!?
Mama mkwe nakupenda sana,sana sana mamangu ila Tafadhari bila kusubiri siku nitakayoteleza na kufungua kunywa changu Leo ntamwambia mwanao bora uende!!
 
Tulisema hapa kwenye mada mojawapo, kwamba sio lazima umpikie mume wako. Delegate hizi kazi kwa mfanyakazi. Mfundishe kupika. Wakaja akina mama hapa wakasema kila siku lazima wao wapike na sio mdada wa kazi.

Kama kuna siku Mr. ana hamu ya kula kitu fulani au ukiwa free, basi pika lakini sio kujitesa kisa kupika. Mume anapokuwa kazini mchana, anapikiwa na nani? Tamaduni zingine bwana!!

Mimi hayo mambo kwenye nyumba yangu nilishayakataa. Akiwa nyumbani atapika, kama hayupo aliye nyumbani atapika. Unagombana na mama mke bure kwa kisa cha kutodelegate.
Kaka kama hapa tu najituma kuamka saa 11 alfajiri ni kazi tu mpaka SAA 2 hadi 3 usiku na maneno ni mengi mno, hayo ni machache sana je niliacha kupika kabisaa siku mzima itakuaje? Kila nyumba inautaratibu wake to me kwa kua ndoa ni yangu na nimeolewa Mimi na si Dada wa kazi,jukumu la kupika linabaki kua langu hasa muda ninaokuwepo nyumbani natimiza majukumu yangu kwa wanangu na kwa shemeji yako, haya ndio maisha yetu ya kila siku hapa ndani Dada ananiandalia vya kupika tu na nikirudi nasikia jikoni kwa ajili ya kukamilisha mlo wa familia yangu miaka yote tumeishi hivi na nimezoea
Labda kama anataka niache kazi aseme
 
Hahahaa nimekusikia ila muda mwingine bora vita vya makombora kuliko vita baridi,inaumiza sana
Nimekuelewa shida yako ni kitendo cha mamamkwe kumzungumza X Wa mumewako so cha msingi ongea na mumewako mwambie asiendeleze jambo hilo unajisikia vibaya atakuelewa
 
Tanga kitu gani wewe dada unaonekana huna busara umesahau ya kuwa mtoto kwa mama hakui ama?? Na wewe umesema mumeo ni mgonjwa sasa kama ni mgonjwa anapaswa kuwa na huruma na mwanae mara kumi zaidi sasa what is your point kuhoji huduma unazompa mwanae?? Ukweli ni kuwa wewe huna mahusiano mazuri na mkweo since day one na haya unayafanya kama sababu ya kutoa makucha yako
Ohoooo!!!
 
LadyAJ nikushauri kitu, achana na huyo mama mkwe ndivyo walivyo. Weka nta masikioni kwako na muonyeshe upendo utakuwa umeonyesha usomi wako. Usipigane na ukuta katika maisha yako. Usisahau hata sisi mama zetu wakiwa na wake zetu wanatuona ni watoto wadogo ingawa tuna wajukuu.
If only it was that simple.
 
Nimekuelewa shida yako ni kitendo cha mamamkwe kumzungumza X Wa mumewako so cha msingi ongea na mumewako mwambie asiendeleze jambo hilo unajisikia vibaya atakuelewa
Hiyo ni moja ya shida yangu,zipo nyingi tu ikiwamo kukulizwa mbona nampa chakula kidogo mwanae,wakati Mimi naishi nae miaka yote hii naujua ulaji wake, inamaana Mimi nampunja mwanae hahahahaa haki ya Mungu, M/Mungu anijaalie kuto fungua mdomo
 
Back
Top Bottom